Je kama rais nimpita njia ama baba ni sahihi kumlaumu kwa kutotimiza sera zake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kama rais nimpita njia ama baba ni sahihi kumlaumu kwa kutotimiza sera zake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by munguatubariki, Aug 21, 2009.

 1. m

  munguatubariki Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Kama leo tunasema raisi ni mpita njia ama baba yetu ni kwanini tunamlaumu kwa kutotimiza sera yake ya maisha bora kwa kila mtanzania ama hii sera ametimiza ama hakutuahidi hili ili tumpe kula?
  Nilitoa hii hoja binafsi ya Rais kumzawadia mototo maskini pipi kwa kusema Rais na wala sio Baba ama kikwete, sijasema mpitanjia wala sijamtaja mtu yeyeote binafsi ni maswali nikiojiuliza mimi binafsi juu ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuiona hiyo picha na nikaamua kushirikiana na wazalendo wenzangu. Naomba mnisamehe kama mawazo yangu yalikuwa ya kipuuzi kuyaleta katika hili baraza lakini nilifanya hivyo kwa kuamini hili ni baraza la The Home of Great Thinkers.
  Sikupenda kuuliza kuhusu uhusiano wa huyo mototo na hiyo gari kwa kuwa naamini Rais wa nchi si ajabu kutembelea hilo gari
  Sikupenda kuhoji kuhusu usalama wake kwa kuwa ni mambo ambayo yanamuhusu yeye binafsi na watu wake wa karibu na ukizingatia Tz ni nchi ya amani sikutaka kabisa kuhoji kuhusi suala la kukaa kiti cha mbele cha gari. Zaidi mimi ni mkeleketwa wa maendeleo ndo maana niliuliza yale maswali ya kimaendeleo.

  napenda kuwakumbusha ya kuwa sijamuongelea mpita njia wala baba , bali nimemuongelea rais wa nchi ambaye tumempigia kura kutokana na sera zake, na ikubukwe ya kuwa Rais alitoa pipi hiyo akiwa ziarani Lindi kikazi na sio katika mapumziko binafsi wala sio siku ya jumamosi wala jumapili.
  Na ikubukwe ya kuwa raisi anamajukumu yake ambayo anatakiwa kuyafanya juu ya wananchi yake kutokana na sera zake wakati wa kampeni.
  Kikumbwa nilichoona hapa ni kwamba, kutokana na uchaguzi mkuu upo karibu basi kunawatu wamepandikizwa sehemu mbalimbali ili kumsafisha Rais ili aendelee kuongoza , lakini mimi naamini ya kuwa kutokana na kuwa na mamluki kila wakati na kila sehemu basi Tz haita endelea hata kidogo.
  Pia nasema sio mbaya kumkosoa Rais kwani kwa kumkosoa na yeye kukubali hayo makosa ndo tunaweza kumchagua kwa moyo safi na kupata maendeleo na sio kufunika madudu yanayoonekana waziwazi.
  Kiukweli mimi simpingi Rais ila najaribu kutumia katiba kuona mapungufu yake ili uchaguzi ujao niwe na imani nae na nimchague tena kwa ajiri ya mapinduzi ya kweli na vita hasa zidi ya ufisadi ulio uchi.
  Ikumbukwe ya kuwa mandeleo ya kweli katika nchi yetu hayata letwa na sisi bali na watoto wetu ambao tutakuwa tumewalea na kuwapandikiza roho za kimapinduzi, fikra za umoja bila matabaka na ubinafsi wa kutojilimbikizia mali. Na sio watoto tulio walea kwa kuwadekeza na kuwambembeleza na kulazimiha upendo toka kwao kwa kuwahonga pipi na vitu vifananavyo…. Kama walivyo fanya wakoloni kwa mapadri kutupa pipi ili tuende makanisani na kuwaamini wao ili watuibie urithi wetu wa asili ambao tunachangamoto ya kuukomboa hii leo ndo maana kutwa tunabishana.

  Nashukuru kwa wote walio changia, walio kubaliana na Raisi kugawa pipi kama baba ama kama mpitajia na pia wale wote walio kupaliana na kitendo hicho cha Rais kwa kuwatukana wezao hasa kwa kusema wanamitizamo finyu na wameishiwa. Na pia napenda niwapogeze walio pinga tendo hili katika mtizamo wa maendeleo na nafasi ya Rais katika jamii wakizingatia sera zake wakati wa kampeni zilizofanya tumpigie Kura na kumuamini kwa kiasi kikubwa,
  Je kama Rais ni Mpita njia ama ni baba ni sahihi kumlaumu kwa lolote? Tujiulize hili swali kwa kuwahusisha marais wote kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa mpk Kikwete.
  Harafu katika kupambanua haya naomba kibisa tusichanganye marekani ama nchi yoyote iliyoendelea na Tanzania yaani Obama na kikwete ni watu wawili tofauti na wanaongoza nchi mbili tofauti na anayefananishwa haya mataifa ama hawa marais si dhani yu mtimirifu wa kuwaza na kupambanua mambo.
  Harafu kumbukeni watanzania wenzangu zawadi kama hizi zimekuwa zikitolewa mara kwa mara ambazo hazisaidii maendeleo ya nchi wala maendeleo binafsi sasa kunahaja ya viongozi wetu kuendelea nazo? Na mwaka ujao ni uchanguzi je kama pipi ndo hizozimeanza je pilau, khanga, kofia n.k…
  Pia naomba motto huyo asihukumiwa kwani muonekano wake ni umri chini ya miaka tisa na mtu anaye deal nae ni Rais harafu anamiaka zaidi ya 50.. nani anatakiwa kuwa na wajibu hapo? Mototo ama mtu mzima? Harafu vp sera ya mototo ni wa wote na ni taifa la kesho hapo haifai ama?
  Changia kwa upeo sio kukulupuka tu na ushabiki… niwakati wa vitendo na sio majungu yasiyo na kikomo…
   
Loading...