Je kama nchi tunajiandaa vipi ili watoto wetu na vijana wetu waweze kushindana kimataifa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Maendeleo ya Tanzania na maswali muhimu. Haya maswali si ya kisiasa ni kwa nchi kwa ujumla

  • Tanzania ni nchi ya vijana na watoto. Asilimia 67% ya Watanzania ni chini ya miaka 25. Je kama nchi tunajiandaa vipi ili watoto wetu na vijana wetu waweze kushindana kimataifa tukizingatia Dunia inazidi kuwa ndogo na technologia inazidi kuwa kubwa
  • Je tutabadilisha vipi mifumo yetu ya kwenda kwenye uchumi wa mtaji bila kuleta michafuko na migongano. Mfano sharia ya sasa ya Ardhi haiendani na uchumi wa mtaji kwasababu Ardhi yote ni ya serikali na inasababisha ugumu kwenye kukopesa na kutafutia mitaji na vilevile uhakika wa uwekezaji kwenye Ardhi.
  • Tutakuza vipi demokrasia, hazi za binadamu bila kuleta machafuko na muonekano wa sasa wa kuminywa kwa demokrasia.
  • Kwasababu pesa inahitajika nyingi kwenye ujenzi tutaingiza vipi mitaji binafsi kwenye miradi bila kuhatarisha usalama wan chi. Hii na maana kama umiliki wa sehemu za barabara toll freeways, line nyingine za train. Mfano fikiria mfano kampuni binafsi ijenge rail kutoka Nairobi mpaka Arusha je inawezekana kwa sharia za sasa? Je tufanyaje kuleta project za hivi wenzetu wanafanya hivi sasa
  • Je tutakuza vipi elimu na kuingiza technologia kwenye elimu yetu ili tuweze kushindana. Technologia imerahisisha mambo mengi lakini Tanzania bado haitumiki vizuri mashuleni mfano mtoto wa miaka 11 Texas kwa sasa anasoma vitabu 50 kipindi cha mapumziko ya kiangazi miezi mitatu kwasababu technologia inaruhusu. Siku hizi mfano unaweza kusikiliza mafunzo kwenye komputa au hata kusahihishwa homework yako na mtu yupo nchi nyingine. Je tunafanya nini kukuza technologia. Technologia ndiyo kitu kikubwa kimefanya elimu yetu ionekane imeshuka ukienda miaka ya 1990’s watoto wetu walikuwa hawako nyuma sana kielimu kama sasa.
  • Je tutapunguzaje gharama za data bila kupunguza kipata cha serikali? . Maelezo zaidi serikali kwa sasa inashidwa kupunguza kodi ingawa ingenufaisha watu sana kwenye data ebu fikiria miji yetu ingekuwa na free wifi ingesaidia vipi biashara, elimu etc. Data Tanzania haitakiwi kuwa juu hivi ni kodi ndiyo sababu
  • Je tutabadilisha vipi tabia za Watanzania na utamaduni wa kufikiria na kusubiri serikali kufanya karibu kila kitu? Mfano wenzetu wa Kilimanjaro kuna sehemu watu binafsi wanachangia barabara za vijijini kwao kupigwa greda hata kuweka lami, huu ni utamaduni ambao sehemu nyingi haupo. Hii ni kwenye shule na shughuli nyingine za maendeleo. Kuna sehemu zina miti lakini huwezi kuona watu wa pale wamejikusanya na kuomba misimeno ya umeme wajenge nyumba zao nzuri zaidi au watoe vipato kwenye kilimo waweke tank kubwa la maji pamoja ni mpaka serikali ifanye.
  • Je tutabadilisha vipi mfomo wa Afya na kutoa elimu ya kupunguza magojwa badala ya kuwa na sera za kutibiwa tu. Kisukari, magojwa ya moyo, malaria yote haya yanaweza kupunguzwa na elimu.
 
Pascal Mayalla ,Zitto nime copy watani wangu hapa
 
Back
Top Bottom