balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,374
- 13,771
Enzi za Nuhu safina lilitengenezwa kabla ya mvua kunya juu ya nchi,watu wakimshangaa mjenzi huyu wa safina.Kuna waloenda kuinyea na kuitia kila aina ya uchafu,wakidhani Nuhu alikuwa mwendawazimu lakini hali ilipobadirika uchafu ule ndo ikawa tiba yao.Je tuifananishe mvua hii na ile ya gharika,je nina ni Nuhu wa kizazi hiki? Nuhu mziwanda namfahamu lakini si mjenzi wa safina,mvua hii imekunya siku kumi na mbili sasa mfululizo ya Gharika ilikunya siku arobaini,ukipiga hesabu bado siku ishirini na nane,je huo ndo uelekeo? Nani kaleta balaa hili? Wanasema hili ni bando tu la HAIKATI ina maana leo kila kitu ni bando? Tulianza na kupatwa ikaja tetemeko,ajali ya watoto A town na sasa mvua inafanya yake ,je tutapataje kuponaaaa?Kila kitu bando tuu mwanawane,halikati,halichachi nk yaani hatari tupu.Hivi wakati wa Nuhu kulikuwa na dhambi kuliko leo? Mimi nakataa,kama gharika lilikuja sababu ya dhambi basi leo yatakuja mara mbili.Hata hivyo tunasema yote yalikwisha pale Calvary,je mbona matatizo bado yapo?