Je, kama haki za kuishi na kuendelea ziko juu ya haki nyingine zote za binadamu?

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
70
110
Ni jambo lisilopingika tukisema kuishi vizuri na kupata maendeleo ni msingi wa binadamu kufanya shughuli nyingine. Mtazamo huu uliosisitizwa na rais Xi Jinping wa China sio tu unalingana na hali halisi ya nchi yake, bali pia unafaa kwa nchi mbalimbali za Afrika, hasa janga la Corona linapoendelea kuenea na kuondoka na roho za watu kote duniani.

Virusi vya Corona vimefanya binadamu waingie kwenye hatari ya kunyimwa haki yao ya kuishi wakati wowote. Katika vita dhidi ya virusi vya Corona nchini China, rais Xi ameagiza kuokoa maisha na kulinda afya ya watu bila kujali hasara yoyote. Kwa mujibu wa waraka wa “mapambano ya China dhidi ya COVID-19”, hadi kufikia tarehe 31, Mei, kiwango cha kupona kwa wagonjwa wa Corona nchini China kilikuwa kimefikia asilimia 94.3; gharama za jumla zilizotumiwa kuwatibu wagonjwa zilifikia Yuan bilioni 1.35, sawa na dola za kimarekani milioni 192 na zote zilitolewa na serikali.


Wakati huohuo, kutoka kupeleka vifaa tiba, kutuma vikundi vya madaktari hadi rais Xi kuahidi kuzipatia kwanza nchi za Afrika chanjo za China dhidi ya virusi vya Corona zitakapotengenezwa, China imekuwa ikijali afya na uhai wa watu wa nchi za Afrika mbele ya janga la virusi vya Corona. Kwani wachina husema “kuna matumaini kama watu wakiwa hai”, halafu matumaini yanaweza kuleta maendeleo.


Kama nchi za Afrika, China nayo pia ina historia ya kuvamiwa na wakoloni kwa muda mrefu. Kutokana na juhudi kubwa, nchi zetu zote zilijipatia uhuru na kujenga nchi, lakini mateso haya yamesababisha hasara kubwa kwa maendeleo ya uchumi na kutishia maisha ya watu wa nchi nyingi zinazoendelea. China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Mnamo mwaka 1950, watu walioishi kwa chini ya dola moja kwa siku walikuwa ni zaidi ya asilimia 40 ya watu wote walio maskini kupita kiasi duniani. Hata hivyo katika miongo saba iliyopita, Wachina milioni 800 wameondokana na umaskini na kuchangia asilimia 70 ya shughuli za kuondoa umaskini duniani. 2020 ni mwaka wa kutimiza lengo la watu wote maskini waishio vijijini nchini China kuondokana na umaskini. Licha ya changamoto zinazotokana na janga la Corona, rais Xi Jinping ametilia mkazo kuwa lengo hilo ni ahadi iliyotolewa na Chama cha Kikomunisti cha China kwa wananchi, hivyo ni lazima kutimizwa bila mjadala.


Wakati huohuo, katika sehemu zilizo kusini mwa Sahara, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, mwaka 2019, kiwango cha umaskini kilitarajiwa kufikia asilimia 48.4, na pato la mtu mmoja mmoja lilikuwa ni dola za kimarekani 1585.4 tu, kiasi ambacho hakijafikia asilimia 15 ya kiwango cha wastani cha dunia, na Kenya ikiwa nchi yenye pato kubwa zaidi kwa mtu mmoja mmoja ilikuwa ni dola za kimarekani 1816.5 tu. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa janga la virusi vya Corona limeleta hasara kubwa zaidi kwa uchumi wa nchi mbalimbali za Afrika kuliko ugonjwa wenyewe, na kwamba malighafi zimeshindwa kuuzwa nje na nchi ambazo zinategemea zaidi uchumi wa kitalii zimekosa watalii. Hii imesababisha watu wa nchi za Afrika ambao maisha yao tayari yamekuwa magumu, waishi kwa umaskini zaidi. Umaskini uliokithiri umewazuia watu kutumia ipasavyo haki zao, hivyo kupunguza na kutokomeza umaskini mara moja ni jukumu kuu zaidi kwa nchi za Afrika.


Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa sisi binadamu tutavishinda virusi vya Corona na watu wa China na Afrika nao hakika wataishi maisha bora zaidi. China ina nia njema na uzoefu wa kuzisaidia nchi za Afrika ili kupunguza kadri iwezavyo athari mbaya zinazotokana na janga la Corona dhidi ya haki za kuishi na kuendelea za watu wa Afrika.
 
Back
Top Bottom