Je, John Pombe Magufuli ataweza kuwa Vladimir Putin wa Tanzania?

Joined
Jun 19, 2012
Messages
26
Likes
5
Points
5

franz

Member
Joined Jun 19, 2012
26 5 5
Endapo John Pombe Magufuli atafanikiwa kushinda uchaguzi hapo Oktoba 2015, basi safari yake ya kuelekea ikulu
itashabihiana sana ile ya bwana Vladimir Putin kwenda Kremlin mwaka 2000.

Hebu tujikumbushe hali ya URUSI kati ya mwaka 1996 na 1999, ikiwa ni kipindi cha pili cha utawala wa Boris Yeltis.
Kipindi hiki kilikua cha majanga makubwa nchini Urusi kwani rasilimali za urusi zilishikiliwa na mabepari wachache
alimaarufu "The oligachy", wakati jumuia kubwa ya raia wa Urusi wakiishi katika dimbwi zito la umaskini.

Hali hii ilisababishwa na rais Boris kukumbatia wafanyabiashara wakubwa waliopata mali kwa njia za kifisadi na
kukwepa kodi iliyopelekea kufilisi uchumi wa nchi kwa kujilimbikizia mali kwenye mabenki ya ughaibuni.

Mwishoni mwa mwaka 1998 Boris alikuwa na afya mbaya hivyo ililazimika kuandaa mapema mtu atakayerithi nafasi
yake kwa masharti ya kumhakikishia Boris usalama atakapostaafu na kulinda interest za mafisadi wake.

Jukumu halikuwa dogo maana aliyewahi kuwa waziri wake mkuu bwana Yevgeni Primakov alionesha nia ya kugombea
na alikuwa akiungwa mkono sana na wananchi wa Urusi kwa sera zake za kupinga ufisadi ili kuleta Urusi mpya tofauti na ile ya bwana Boris.

Ili kumdhohofisha bwana Primakov, Boris na wafuasi wake wakiongozwa na mshauri wa karibu wa rais Boris bwana
Boris Berezovsky, walisuka mpango madhubuti kumuondoa kwenye ramani ya siasa za Urusi.

Kwanza walimtafutia skendo mbaya bwana Primakov, pili Boris akamteua bwana Vladimir Putin kuwa Waziri mkuu.Ikumbukwe bwana Putin alikua mtu asiyefahamika kabisa kwenye siasa za urusi, kwani alikuwa ni afisa usalama wa urusi (KGB).

Putin alikuwa amewekwa kwa makusudi kwanza apate umaarufu wa kisiasa,pili amlinde Boris na wafuasi wake mara tu atakapo kuwa Rais.

Baada ya muda mfupi Borisi alikasimu madaraka ya uraisi kwa Putin Baada ya yeye kujiuzuru rasmi December 1999. Putin alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kufanikiwa kumaliza propaganda ya vita vya CHECHNIA na akafanikiwa kujilikana ndani URUSI.

Wakati wa uchaguzi, Boris na washirika wake walitumia pesa nyingi ili kuhakikisha Vladimir Putin anashinda kiti cha urais na walifanikiwa adhma yao maana baada ya uchaguzi Putin aliibuka kidedea akawa raisi wa URUSI mwaka 2000.

Baada ya Putin kuwa Rais, ilitarajiwa Boris na wafuasi wake wangeendelea kupeta kwa ufisadi wao.Lakini haikua hivyo, kwani Putin aliwageuka mafisadi wote na akaanza kuwasaka mmoja mmoja na kuwashitaki kwa ufisadi na ukwepaji mkubwa wa kodi.

Hapo ndipo maisha ya mabilionare mafisadi au "the oligachy" yakawa magumu, wengi walifungwa na kunyang'anywa biashara zao, wakati wengine iliwalazimu kukimbia nchi, watu kama Roman Abromivich, Boris Berezovsky na Vladimir Gusinksky ni baadhi tu ya waliokimbia nchi na kuishi uhamishoni mpaka leo hii kwa kukwepa mkono wa sheria.

Turudi kwa bwana Magufuli, ni wazi kwamba amefanikiwa kuwa mgombea wa CCM baada ya Vita baina ya makundi makubwa ndani ya CCM yanayosapotiwa na wafanyabiashara wakubwa nchini, yaliyoondolewa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi kwa kuhakikishiwa kulindwa na the neutral Magufuli.

Makundi hayo hayajaoendelewa kirahisi tu, bali ni lazima yameahidiwa kulindwa na CCM endapo yataunganisha nguvu na kumuunga mkono Bwana Magufuri.

Hali ya sasa ya Tanzania haina tofauti sana na ile ya kipindi cha Bwana Boris, kwani serikali imekithiri vitendo vya ufisadi, imekua ikilinda wafanya biashara wakubwa walio maarufu wa kutolipa kodi stahiki na shutuma nyingine nyingi.

Watu wachache wanamiliki uchumi wa tanzania wakati jumuia kubwa ya watanzania bado wakiwa hoi taabani kwa umaskini uliokithiri.

Bwana Magufuli anawania kiti cha uraisi akijua fika ana kazi ya kulinda mfumo mzima wa CCM uliojaa Mafisadi endapo atashinda uchaguzi huu ili kutimiza kiapo alichokula mara alipochaguliwa kwa kishindo kuwa mgombea wa CCM.

Je, Magufuli ataweza kuwa Putin mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania? Nikiwa namaanisha, Je
Magufuli ataweza kuyasaliti makundi hayo na mfumo mzima wa CCM uliojaa mafisadi na kuanza kuushitaki na kukamata mafisadi na wakwepaji wakubwa wa kodi ili kuijenga Tanzania mpya?

Vladimir Putin alithubutu na aliweza kuwashitaki mafisadi.

Je, Magufuli ataweza kuwa Putin wa Tanzania?
 

Forum statistics

Threads 1,203,563
Members 456,824
Posts 28,118,884