Je, JK Gorbachev part II?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Mikhail Gorbachev anakumbukwa kama kiongozi wa Russia aliyefanya mapinduzi ya anguko la Soviet Union (USSR) mwishoni mwa miaka ya 80. Ni Gorbachev huyo alieingia madarakani na kukuta U-communist nchini Russia na ulaya mashariki umeshika mizizi kiasi cha kuwa ngome kuu ikishindana na Marekani. Kazi kubwa aliyohakikisha Rais Gorbachev ni kubadili mfumo na itikadi toka u-communist na kwenda Ubepari na kuwa ndio anguko na sambaratiko la kambi ya mashariki ya ki-communist.

Namfananisha JK na Gorbachev katika medani ya siasa kwa kuwa kiongozi huyu ameikuta CCM ikiwa bado inanguvu takriban mikoa yote ya Tanzania ukiondoa Pemba, Kilimanjaro, Kigoma na Mara. Wapo watu walidiriki kuamini CCM haitoanguka hivi karibuni at least miaka 20 mbele.

Lakini leo hii tayari chama hiki kimepoteza mvuto katika majiji yote makubwa yenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania ikiwemo DSM, Mwanza, Mbeya, Arusha pamoja na Manispaa ya Shinyanga mkoa ambao ni wa tatu kwa idadi kubwa ya watu nchini.

Kupoteza huku mvuto kwa CCM kunaashiria uongozi mbovu wa mwenyekiti wa chama kinachoongoza serikali na ambaye ndio Rais wa Jamhuri ya muungano.

Kama Gorbachev alivyosambaratisha USSR, inahitaji majibu ya kuridhisha sana kama kweli Jakaya Kikwete hajaja kusambaratisha CCM ili aweke historia ya kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania toka CCM. Watu mbalimbali wamekuwa wakijivunia kuvunja record mbalimbali zilizowekwa duniani kwa kufanya matukio ya kipekee. Bila shaka nadiriki kuamini kuwa bwana huyu ameamua kuwa Gorbachev wa pili kwa kuhakikisha anakuwa rais wa mwisho toka CCM.

Angalizo kwa wana-CCM wote kuweni makini kwa watu wanaotafuta kuvunja records kupitia migongo yenu. Anguko hilo limewafika jipu linawatumbukia mikononi.
 
Lakini Gorbachev aliisambaratisha USSSR kwa sera zake za Glasnost na Perestroika. na kikwete wanafananaje? Tafuta Historia ya Ponzi Scheme Hungary ndiyo utajua Kikwete hafanani na Gorbachev!!
 
Kifupi ni kwamba kazi imemshinda sasa hili la kumfananisha na Gorbachev naona Kama unajaribu kumtetea vile?!
 
Hiyo yote ni kuashiria mwisho wa magamba umefika,hivyo anatimiza unabii!! hata hivyo mimi napita tu jamani.
 
Mkuu, kuwafananisha hawa marais wawili si sahihi. Kwanza Gorbachev hajawahi kuwa rais wa Russia, alikuwa ni kiongozi wa USSR. Russia ilikuwa ni moja ya jamhuri zilizokuwa zinaiunda USSR.

Pili Gorbachev alileta Perestroika (Reconstruction) na Glasnost (freedom of speech), ili Warusi wabadilike kiuchumi na wawe na uhuru wa kuongea, hakuleta ubepari kama unavyodai.

Tatu, kipindi chake ndicho kilichoimaliza vita baridi kati ya blocks mbili kuu zilizokuwepo enzi hizo (Warsaw Pact na NATO), na ndiye aliyewaunganisha Wajerumani wa mashariki na magharibi hadi kupewa heshima ya funguo za mji wa Berlin na uraia wa Ujerumani pia. Ni mtu aliyefanya mambo makubwa.

Tamaa za uongozi za watu wasiokuwa na uwezo wa kuongoza za watu kama Boris Yeltsen ndizo zilizoiangusha USSR, ambapo kwa kuwa hakutaka kuiingiza nchi vitani Gorbachev aliamua kwa hiari yake mwenyewe na kutangaza katika vyombo vya habari kwamba kuanzai leo (siku hiyo), najivua uongozi na u-amiri jeshi mkuu wa USSR. Ndiyo maana mpaka leo bado anaheshimika, si kwao tu bali duniani kote.

Ndiyo maana pia, vijana aliokuwa nao enzi hizo akina Putin, kwa kugundua makosa yale ya akina Yeltsen, wanabadilishana madaraka ili kutoruhusu watu wa aina ya Yeltsen kuingia madarakani kuiharibu nchi ambayo kwa sasa inapaa kiuchumi duniani.

Nisingependa kuelezea na kufananisha na Tz, kwa sababu yenyewe siyo historia bali ni kitu kilichopo na kinachoendelea na kila mwenye macho anaona na mwenye masikio anasikia.
 
kwani Jk hajaruhusu uhuru wa kuongea?washikaji pale mjengoni wanashusha swaga za kufa mtu. JK ataua kila kitu. Mle Ikulu hatujampeleka tu CAG akakague, tutakuta hadi mashuka hayapo. Katumwa huyo kuifilisi nchi ili Wamarekani waje kututawala. Yani huyu jamaa ni Gobachev liye!
 
kwani Jk hajaruhusu uhuru wa kuongea?washikaji pale mjengoni wanashusha swaga za kufa mtu. JK ataua kila kitu. Mle Ikulu hatujampeleka tu CAG akakague, tutakuta hadi mashuka hayapo. Katumwa huyo kuifilisi nchi ili Wamarekani waje kututawala. Yani huyu jamaa ni Gobachev liye!
 
Lakini Gorbachev aliisambaratisha USSSR kwa sera zake za Glasnost na Perestroika. na kikwete wanafananaje? Tafuta Historia ya Ponzi Scheme Hungary ndiyo utajua Kikwete hafanani na Gorbachev!!

Kumlinganisha Gorbachev na Kikwete kunanipa swali kama huyu mleta mada yuko serious au kaleta habari kwa kebehi na kejeli tu.
 
Pia Gorbachev alikuwa amepandikizwa na Wamarekani ili asaidie kusambaratisha USSR.

Back
Top Bottom