Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Mikhail Gorbachev anakumbukwa kama kiongozi wa Russia aliyefanya mapinduzi ya anguko la Soviet Union (USSR) mwishoni mwa miaka ya 80. Ni Gorbachev huyo alieingia madarakani na kukuta U-communist nchini Russia na ulaya mashariki umeshika mizizi kiasi cha kuwa ngome kuu ikishindana na Marekani. Kazi kubwa aliyohakikisha Rais Gorbachev ni kubadili mfumo na itikadi toka u-communist na kwenda Ubepari na kuwa ndio anguko na sambaratiko la kambi ya mashariki ya ki-communist.
Namfananisha JK na Gorbachev katika medani ya siasa kwa kuwa kiongozi huyu ameikuta CCM ikiwa bado inanguvu takriban mikoa yote ya Tanzania ukiondoa Pemba, Kilimanjaro, Kigoma na Mara. Wapo watu walidiriki kuamini CCM haitoanguka hivi karibuni at least miaka 20 mbele.
Lakini leo hii tayari chama hiki kimepoteza mvuto katika majiji yote makubwa yenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania ikiwemo DSM, Mwanza, Mbeya, Arusha pamoja na Manispaa ya Shinyanga mkoa ambao ni wa tatu kwa idadi kubwa ya watu nchini.
Kupoteza huku mvuto kwa CCM kunaashiria uongozi mbovu wa mwenyekiti wa chama kinachoongoza serikali na ambaye ndio Rais wa Jamhuri ya muungano.
Kama Gorbachev alivyosambaratisha USSR, inahitaji majibu ya kuridhisha sana kama kweli Jakaya Kikwete hajaja kusambaratisha CCM ili aweke historia ya kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania toka CCM. Watu mbalimbali wamekuwa wakijivunia kuvunja record mbalimbali zilizowekwa duniani kwa kufanya matukio ya kipekee. Bila shaka nadiriki kuamini kuwa bwana huyu ameamua kuwa Gorbachev wa pili kwa kuhakikisha anakuwa rais wa mwisho toka CCM.
Angalizo kwa wana-CCM wote kuweni makini kwa watu wanaotafuta kuvunja records kupitia migongo yenu. Anguko hilo limewafika jipu linawatumbukia mikononi.