Je Jk anapumzika wapi kwa kodi yetu huku tukitaabika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Jk anapumzika wapi kwa kodi yetu huku tukitaabika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gembe, Dec 24, 2007.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwaka jana mkuu wa nchi alikuwa na mapumziko kwa muda wa siku 5 moja pale sasakwa lodge amabyo iko serengeti,Gharama zake per nite ni $1800,na alikuwa na ujumbe wa watu 25 ambao unajumuisha wapishi wake na walinzi wake pamoja na wasaidizi wa rais na familia yake pia.ukiangalia gharama za malazi tu kwa siku hizo ni sh. $45,000 kwa muda wa siku 5 ni kama $ 225000,Je hizo gharama za mapumziko na Rais ni kwa mfuko upi?

  Je mwaka huu kaenda wapi?
   
 2. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2007
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umaskini unatuweka mahala ambapo hata Mkuu akienda haja tutauliza leo kaingia choo kipi? Na alipoingia alijisaidia haja kubwa au haja ndogo?Mbona huko UK hawaulizi Brown kapumzika wapi na katumia hela ngapi? Au ndiyo yale yale ya bongo zetu zinavyowaza mambo.Unataka kutwambia Mkuu anaiba?
   
 3. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huku kwa brown mambo yote adharani,wanatumia pesa zao na sio za serikali,tena huwa awana wapambe kama huko bongo,utawaona wakiogelea beach na kula maisha bila kificho.
   
 4. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,276
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  huna uchungu na nchi yako ama hujui ulinenalo ama nawe ni mmoja wao
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2007
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama hizi figures ziko sawa dollar 225,000 ni hela nyingi sana kwa nchi masikini.Chukua hesabu ndogo tu mtu wa kawaida, mfanyakazi wa serikali analipwa kiasi gani kima cha wastani halafu uniambie kuna mishahara mingapi ya wafanyakazi wa serikali kwa mwaka mzima.

  Au hata yeye mwenyewe JK, ina maana anatumia more kwenye likizo kuliko anavyo earn? Au kwa sababu ni pesa za umma? ingekuwa kampuni ya babae na madeni yote tuliyonayo angediriki?

  Alivyokuwa foreign kuna wazee walikuwa wansema sana alivyokuwa anatumia pesa vibaya kutanua.Tukawakanya watu chonde chonde wasimchague urais (urahisi?) hawakusikia wakatuona wazushi, sasa tunaona wenyewe.
   
 6. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ndugu una uhakika na hizi gharama? Hiyo ni Serengeti ya Bongo ama ya mahali pengine? Sijawahi kuona hoteli bongo yenye gharama hizo, kama kuna watu huku wanajua watusaidie. Hebu tuwekee hata invoice moja hapa (si lazima iwe hiyo aliyotumia mwungwana JK), kututhibitishia kuwa kweli hiyo ndio bei yake.
   
 7. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2007
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nasema hivyo kwa sababu hakuna uthibitisho wa madai ya matumizi hayo.Ni hulka ya masikini kubuni vitu ili mradi alalame tu.Kama ni kweli angetupa data za uhakika.uzushi kwa sababu una chuki na Mkuu hauna maana.Lete ushahidi hapa nitakuunga mkono lakini lawama zisizokuwa na kichwwa wala miguu...no bwana...
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  SASAKWA LODGE


  Set on a hill above the rolling hills of the Serengeti

  7 luxury cottages all en suite with bath, shower and dressing room

  Each cottage has private living room, verandah and infinity pool
  Host of exciting activities, including a spa, equestrian centre, archery range & game drives

  Sasakwa, the flagship lodge of Grumeti Reserves, is set high on a hill above the rolling plains of the Serengeti with spectacular views. With its elegant architecture and exquisite furnishings, the lodge is reminiscent of the early 1920’s. The long sweeping verandahs, beautifully appointed drawing rooms, fine antiques and works of art at Sasakwa truly reflect the exceptional style of a former era. Enjoy the fine cuisine in the beautiful dining room where shimmering silver candelabras, Stuart crystal and Wedgwood china compliment the mighty backdrop of the African bush.

  Accommodation consists of seven luxurious cottages offering between one and four bedrooms, all en suite with bath, shower and dressing room. Each cottage also has a guest toilet, private living room, veranda with Swarovski spotting scope, garden and heated infinity plunge pool. The lodge areas offer a dining room, bar lounge, games room with satellite television, DVD player and library, Playstation and board games, and garden room opening onto wide wrap round verandas, as well as a library, billiards room, wine cellar, and Colonial Trading Post. A unique facility of the lodge is the spa, featuring a steam room, relaxation area, hydrotherapy tub, gymnasium, yoga room and two therapy rooms for treatments. Many treatments can also be conducted in guest cottages. A heated infinity swimming pool and Jacuzzi are located alongside the Spa.

  There are sixteen horses at the Equestrian Centre, a combination of polo ponies, part thoroughbreds and warm blood sport horses. All equestrian activities are led by professional, fully qualified horse guides. Tennis can be enjoyed at the Sports Pavilion, with a choice of court surfaces – artificial clay and rebound ace. Other professionally guided activities include game drives in open vehicles, walks, night drives, mountain biking and archery. At Sasakwa lodge there really is something for everyone.

  Sasakwa Lodge may be booked on an exclusive basis and will accommodate up to 28 individuals. Total cost per night is $42000 which accommodates up to 28 individuals.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kithuku,Kama jana uliangalia thread mojawapo niliweza kujibu hili baada ya Admin kung'oa hii maada.Asante Invisible kwa kuirudisha.
  ndio matumizi ya Viongozi wetu,Kupenda Maisha Ya kifahari.mkwa usiku Mmoja kwa Gharama za Kawaida ni $1500.Maji moto katoa na Link hapo.

  Pili Mkuu kaenda kupumzika na katuachia balaa la kupandishwa kwa Umeme
   
 11. i

  ishengoma Member

  #11
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa wewe ulitaka aende wapi,na uwezi kuhoji preveleges za rais bwana ni haki yake uspende kujilinganisha nae ndg hoji mambo mengine reasonable kwa hili skuungi mkono,wacha apumzike amebeba majukumu makubwa ya nchi!His word can destroy the whole precess or can make it better
   
 12. i

  ishengoma Member

  #12
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umejibu vema mkuu nimependa arguement yako
   
 13. i

  ishengoma Member

  #13
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo kubwa naisi sio matumizi makubwa ndio maisha halisi ila tatizo ni uwajibikaji wao ktk mamlaka waliopewa,laiti wangekuwa strict ktk kazi zao,means no rushwa hata wakistarehe no problem,lakini inauma kama unaenda kustarehe wakati umefanya kazi madudu.
   
 14. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ishengoma,
  Tatizo si kwenda wapi,Je kuna Haja gani kwa Rasi kutumia gharama kubwa kiasi hicho wakati asilimia 80 waliompa kura wakitaabika?
  huujui uchungu wa nchi hii ndio maana unatoa maneno hayo yasiyo na chembe ya hoja,
  Akapumzike ?amebebea majukumu mazito?yapi?amebeba mafisadi kama kina Rostam,amewakumbatia kina karamagi na kina Mnyang'ayanyi,ametudhalilisha kwa kuishi maisha yasiyofaa..maisha yasiyo Bora,
  aliyekutuma uje na hoja dhaifu hapa ameshikwa pabaya.na Nakuonya Mwana wa Kitanzania,Dhambi ya kutetea Ufisadi itakupeleka Motoni sababu Ufisadi ni dhambi!
  Tunaendelea kumkoma Nyani giladi mchana kweupe mpaka kieleweke.

  Mkombozi
  Kada Wa Chama Cha Mapinduzi
  CCM SIO MAMA YANGU
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hilo tu mkuu,

  Japo wewe ni kada mkereketwa lakini maslahi ya taifa mbele..., tafadahali wafikishie makada wenzio ujumbe!
   
Loading...