Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,448
Wanabodi,
  1. Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ikiwa ni kwa njia ya swali fikirishi "Jee Jicho la Rais Mama Samia Suluhu Hassan, litaweza kuangazia ubatili huu ndani ya Katiba tetu, unaopora haki ya msingi ya kushiriki uchaguzi kwa kugombea, uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha tuu?.
  2. Hii ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya pili ya mada hii nilioianza wiki iliyopita kuhusu wema wa Rais Samia ambaye ni mpenda haki, na mtenda haki, na jinsi anavyoliponya taifa kupitia wema wake na kutenda haki kwake, Makala ya wiki iliyopita ni hii HAPA! nikaahidi, kuanzia wiki hii, nitaangazia baadhi ya vifungu vya katiba yetu, vinavyonyima haki, zilizotolewa na ibara moja, zikaja kupokonywa na ibara nyingine, kwa kuchomekewa vipengele vinavyoipora haki hiyo, na kuchomekwa kiubatili ndani ya katiba yetu systematically ili kuvihalalisha kikatiba, wakati kiukweli kabisa vifungu hivyo ni batili na vimechomekewa kiubatil na viko kinyume cha nia njema ya mtunga katiba hivyo hapa nina viangazia kwa kuvimulikia ili jicho la haki la Rais Mama Samia livione viondolewe, ili kuwatendee haki Watanzania.
  3. Nimepata bahati kusomea sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM na kufunza na waalimu manguli kabisa na wabobezi wa sheria, na hawa ni baadhi ya waalimu wetu, kina Prof. Issa Shivji, Prof. Palamagamba Kabudi, Prof. Sifuni Mchome, Dr. Ibrahim Juma (sasa Prof. na ndiye Jaji Mkuu) Prof. Safari, Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo, Prof. Chris Peter Maina, Dr. Hamud Majamba, Tulia Akson, (sasa ni Spika, wakati huo hata u Dr. bado) kwa kuwataja wachache, walitufunza, moja ya maeneo magumu sana kwenye fani ya sheria, ni eneo la kutafsiri katiba na sheria, kiingereza wanaita, “Legal Interpretations” na kutokana na umuhimu wa eneo hili, kwa mujibu wa katiba yetu, taasisi pekee yenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni mhimili wa Mahakama, upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
  4. Tulifundishwa, katika kutafsiri sheria, mahakama inaangalia nia na dhamira ya mtunga katiba na mtunga sheria, au alidhamiria nini kutunga kipengele hicho kinachohitaji kutafasiriwa, hivyo ili kutafsiri kifungu chochote cha katiba, lazima kwanza wewe mfasiri uvae viatu vya mtunga katiba.
  5. Hivyo hapa mimi sio Mahakama, kutafsiri Katiba, bali naileta hii mada kama mwananchi wa kawaida tuu anayavijaribisha kuvivaa viatu vya mtunga katiba, alidhamiria nini wakati anatunga kifungu hicho, cha Katiba ninachotaka jicho la Mama Samia likiangazie, kwanza ni Ibara ya 5 ya msingi wa haki na dhamira ya mtunga katiba
  6. Ibara ya 5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura (na kupigiwa kura) katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi.
  7. Ibara ya 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
  8. Kifungu hicho ndio nia na dhamira ya mtunga katiba kwamba “kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao”
  9. Kumbe haki hiyo ya kikatiba, iliyotolewa na ibara 5 na Ibara ya 21 hiyo, imekuja kufanyiwa marekebisho kinyume cha katiba kwa kuipora haki hiyo ya msingi kwa kuichomekea ibara ndogo mbili ya 39 na 67 zinazoipora kabisa haki iliyotolewa na Ibara ya 5 na Ibara ya 21 ya katiba.
  10. Ibara hizo zinasema
  11. Ibara ya 39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama- (c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
  12. Ibara ya 67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
  13. Kwa mtu wa kawaida tuu ambaye sio mtaalamu wa kuisoma katiba, utakiona vipengele hivyo vya katiba viko sawa kabisa vinatoa haki kwa kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kumbe haki hizo zimeporwa kwa kuchomekewa sherti la kudhaminiwa na chama cha siasa, ambalo sio dhamira ya mtunga katiba.
  14. Ni Bunge ndio lilichomekea sherti hilo, la kudhaminiwa na cha siasa ni kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni kinyume cha Universal Declaration of Human Rights, ni kinyume cha The United Nations Human Rights Committee, ni kinyume cha African Chatter of People and Political Rights hivyo tunamuomba Rais Samia, lile jicho lake la haki, pia likiangazie kipengele hiki cha dhulma, ili kuwatendea haki Watanzania.
  15. Katiba ni mali ya wananchi, katiba hiyo inatungwa kwa misingi ya haki, Katiba imeweka haki ya wananchi kuchagua na kuchaguliwa na ikazifungia haki hizo kwa kuweka “ring fencing” Bunge la JMT lilipata wapi mamlaka ya kuipindua katiba ya JMT?.
Tukutane wiki ijayo, na kwa vile hii ni issue nyeti, ya kikatiba na kisheria, tutakwenda mdogo mdogo ambapo nita wapitisha taratibu, hatua kwa hatua, uhuni huu kuchomekewa ndani ya katiba yetu ilitokeaje tokeaje, kipengele hicho batili, kikachomekewa ndani na katiba yetu huku tuna wanasheria ma nguli na wabobezi wa katiba, ndani ya Bunge letu, tena akiwemo yule graduate wa Havard (Havard kilichopo Marekani, ndio chuo No. 1 cha sheria duniani, kikifuatiwa na Yale cha Uingereza) wapo wapo tuu na wamenyamaza huku wanaangalia katiba yetu inavyochezewa?.

Paskali
Kwa wale wapenda haki ambao mtapenda kujielimisha zaidi,
ukipitia mitaa hii, itakusaidia zaidi kunielewa ili twenda pamoja.
Anza na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!

Kisha njoo Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
 
Sasa naelewa kwanini nikisoma historia ya Rais Jomo Kenyatta kuongozana /kufuatana kwa karibu na mwanasheria wake mkuu katika ziara za wilayani, mkoani na nje ya nchi kwamba kubwa ni Mzee Jomo Kenyatta alitaka kujua kila jambo analo ambiwa au kutaka kutoa maelekezo je katiba inasemaje, kuna mkinzano kisheria n.k

1654850204274.png

Photo : Mzee Jomo Kenyatta akiwa amemshika mkono mtoto uhuru Kenyatta na mwanasheria mkuu Charles Njonjo QC mwenye suruali nyeupe akiwa karibu kutoa dondoo yoyote ya papo kwa hapo kumsaidia rais Jomo Kenyatta masuala ya kustukiza ya kisheria inapobidi
Kupitia historia inaonekana umuhimu wa mwanasheria mkuu wa serikali kujumuishwa katika ziara zote za mheshimiwa rais wa Tanzania ili aweze kumshauri papo kwa hapo kuhusu masuala ya katiba na sheria.

ZIARA YA MH. RAIS MKOANI KAGERA, YAZUA GUMZO LA KISHERIA

9 Juni 2022
Kagera, Tanzania

RAIS SAMIA HASSAN AWAVAA TRA ''KUANZIA SASA MSIDAI KODI ZA NYUMA'' WAPENI RAHA WAFANYABIASHARA

Mh. Rais ahoji mamlaka ya mapato Tanzania TRA na halmashauri za wilaya / miji kukimbizana na wananchi kukusanya madeni ya kodi za miaka ya nyuma, na kuwataka waachane na mtindo huo wa kufuatilia madeni ya miaka mitatu, minne, mitano nyuma bali labda tu deni la mwaka mmoja nyuma ndiyo linafaa kufuatiliwa ili kulipwa, asema mheshimiwa rais ambaye yupo ziarani mkoa wa Kagera.

Mh. Rais ametoa kauli hiyo kufuatia mbunge kuzungumzia suala la wananchi kusumbuliwa kodi.

MWANASHERIA MKUU CHARLES NJONJO QC WA KENYA HAKUCHEZA MBALI ALIKUWA KILA MARA YUPO JIRANI NA RAIS KUTOA USHAURI WA KISHERIA

https://www.milleradvocates.com › l...
Charles Njonjo, Jomo Kenyatta's powerful Attorney-General

Mwanasheria mkuu Charles Njonjo QC hakutaka marais washauriwe vibaya, siku zote alikuwa katika misafara ya marais tayari kutoa ushauri wa kisheria

1654851010338.png

6 Jan 2022 — “When Mzee (Jomo Kenyatta) became Prime Minister, I was appointed Attorney-General and when Kenya became a Republic in 1964, ...
 
Adui no 1 wa taifa hili ni CCM wala hakuna cha katiba, CCM imeleta mifumo mibovu ya hovyo sn ndiyo nchi pekee duniani Spika na Naibu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote hata ukikutana naye bar akachukua bastola akakupiga kisa umemnyang'anya demu au bia wala hawezi kufanywa chochote, ni mfumo wa kijinga sn.
 
Sasa naelewa kwanini nikisoma historia ya Rais Jomo Kenyatta kufuatana na mwanasheria wake mkuu katika ziara za wilayani, mkoani na nje ya nchi kubwa ni Mzee Jomo Kenyatta alitaka kujua kila standalone au kusema je katiba inasemaje, kuna mkinzano kisheria n.k

View attachment 2256109
Photo : Mzee Jomo Kenyatta akiwa na mwanasheria mkuu Charles Njonjo QC

ZIARA YA MH. RAIS MKOANI KAGERA, YAZUA GUMZO LA KISHERIA

9 Juni 2022
Kagera, Tanzania

RAIS SAMIA HASSAN AWAVAA TRA ''KUANZIA SASA MSIDAI KODI ZA NYUMA'' WAPENI RAHA WAFANYABIASHARA

Mh. Rais ahoji mamlaka ya mapato Tanzania TRA na halmashauri za wilaya / miji kukimbizana na wananchi kukusanya madeni ya kodi za miaka ya nyuma, na kuwataka waachane na mtindo huo wa kufuatilia madeni ya miaka mitatu, minne, mitano nyuma bali labda tu deni la mwaka mmoja nyuma ndiyo linafaa kufuatiliwa ili kulipwa, asema mheshimiwa rais ambaye yupo ziarani mkoa wa Kagera.

Mh. Rais ametoa kauli hiyo kufuatia mbunge kuzungumzia suala la wananchi kusumbuliwa kodi.

Jama wapo mbali sn
 
1654851637538.png

Picha : Wapili kushoto mwenye sweta la mistari Charles Njonjo QC mwanasheria mkuu akiwemo ktk ziara za Jomo Kenyatta. Wenye makofia ni wakuu wa mikoa provincial commissioners wa mikoa wateule wa kisiasa ambao hawajui masuala ya sheria na katiba.

.Mwanasheria mkuu wa Kenya, Charles Njonjo QC alikuwa muda wote karibu na rais kutoa ushirikiano kuhusu sheria

Picha mstaafu Charles Njonjo QC katikakati akiwa na rais Moi kushoto na profesa Anyang' Nyongo kulia .

1654850857494.png
 
Pascal Mayalla naona umetoa hitimisho la kesi ile jinsi itakavyokuwa na kama ni hivi basi tutaendelea kuchezewa rafu siku zote ikiwa wataalam wa sheria wataendelea kukaa kimya na kuelimisha jamii.

Ila hili linafanyika makusudi kwa manufaa ys vikundi fulani pamoja na wanufaika wachache.
 
Tukutane wiki ijayo, na kwa vile hii ni issue nyeti, ya kikatiba na kisheria, tutakwenda mdogo mdogo ambapo nita wapitisha taratibu, hatua kwa hatua, uhuni huu kuchomekewa ndani ya katiba yetu ilitokeaje tokeaje, kipengele hicho batili, kikachomekewa ndani na katiba yetu huku tuna wanasheria ma nguli na wabobezi wa katiba, ndani ya Bunge letu, tena akiwemo yule graduate wa Havard (Havard kilichopo Marekani, ndio chuo No. 1 cha sheria duniani, kikifuatiwa na Yale cha Uingereza) wapo wapo tuu na wamenyamaza huku wanaangalia katiba yetu
Yale university ipo Connecticut, Marekani pia!

Kuhusu 'ubatili' wa Katiba, naunga mkono hoja..
 
Asante kwa andiko hili. Nadhani utakuja na lile la Ngorongoro pia sheria inasemaje?. Lakini pia tuliambiwa ni swala la Uhifadhi Mazingira, na sasa hizi rumors za Uwekezaji zinakujaje? Katiba inasemaje

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Pascal Mayalla hongera kwa bandiko zuri,sehemu pekee ulipoharibu ni kuwataja waalimu wako Kabudi,Tulia na Prof Ibrahimu kama waalimu wako na kujenga msingi wa hoja yako juu Mgombea huru.

Kwa hakika hao waalimu labda ni wazuri katika kufundisha tu,matendo yao yanapinganana na kile walichokufundisha.Khasa Prof Kabudi hajaitendea vyema taaluma yake zaidi ya kujipendekeza na kutoa mimacho.

Ngongo kwasasa Kagera.
 
Umri wa kuchagua na kuchaguliwa ni miaka 18..

Katiba hiyohiyo inazuia kuchaguliwa umri kati ya 18- 39 kuwa rais.

Tubadilisheni iwe hivi
1. Achaguliwe ngazi yoyote mwenye sifa ya kuchagua
Au
2. Umri wa kuchagua uwe miaka 40+.

Tusiwadhulumu vijana.

Nyerere alikuwa na 39 wakati anachukua nchi
 
Hili la umri wa Rais nadhani hiyo miaka 40 ni sahihi kabisa.Ebu fikiria bahati mbaya Sabaya kachaguliwa Rais wetu.
 
Wanasheria wote lazima msome vitabu vya ziada kuongeza upana wa maono mfano kitabu cha Donnie Brasco: Unfinished Business (is the final chapter in the story of a real American hero) na ku-demand nafasi yenu muhimu ya kutoa ushauri wa kisheria kwa clients wenye nguvu kubwa katika jamii.

Hao viongozi ni pamoja na wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, viongozi wa kiimani wakubwa n.k ili muweze kuwaongoza vizuri katika maamuzi yao na pia kuwaasa ni watu gani wakae nao mbali maana wanaweza kuwarubuni kufanya mambo au maamuzi yatakayozua mtafaruku kisheria leo au siku za usoni .
Picture

Why Book Joe Pistone?​

Millions around the globe know Joe Pistone as "Donnie Brasco," arguably the most influential law enforcement agent in American history. His unrivaled undercover work lead to the imprisonment of hundreds of Mafiosi and rocked the American Mob to its core.

In the years since leaving the FBI, Joe has become a highly sought-out keynote speaker. He has spoken around the world, from universities and educational institutions, to military gatherings and corporate events. Perhaps his greatest strength as a communicator is his unique form of storytelling. His down-to-earth approach is powerful, and his firsthand insights captivate an audience and holds their attention like few other speakers can.

It has often been said that a pin drop can be heard when Joe Pistone speaks.
Read more : Joe Pistone
 
Wanabodi,
  1. Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ikiwa ni kwa njia ya swali fikirishi "Jee Jicho la Rais Mama Samia Suluhu Hassan, litaweza kuangazia ubatili huu ndani ya Katiba tetu, unaopora haki ya msingi ya kushiriki uchaguzi kwa kugombea, uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha tuu?.
  2. Hii ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya pili ya mada hii nilioianza wiki iliyopita kuhusu wema wa Rais Samia ambaye ni mpenda haki, na mtenda haki, na jinsi anavyoliponya taifa kupitia wema wake na kutenda haki kwake, Makala ya wiki iliyopita ni hii HAPA! nikaahidi, kuanzia wiki hii, nitaangazia baadhi ya vifungu vya katiba yetu, vinavyonyima haki, zilizotolewa na ibara moja, zikaja kupokonywa na ibara nyingine, kwa kuchomekewa vipengele vinavyoipora haki hiyo, na kuchomekwa kiubatili ndani ya katiba yetu systematically ili kuvihalalisha kikatiba, wakati kiukweli kabisa vifungu hivyo ni batili na vimechomekewa kiubatil na viko kinyume cha nia njema ya mtunga katiba hivyo hapa nina viangazia kwa kuvimulikia ili jicho la haki la Rais Mama Samia livione viondolewe, ili kuwatendee haki Watanzania.
  3. Nimepata bahati kusomea sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM na kufunza na waalimu manguli kabisa na wabobezi wa sheria, na hawa ni baadhi ya waalimu wetu, kina Prof. Issa Shivji, Prof. Palamagamba Kabudi, Prof. Sifuni Mchome, Dr. Ibrahim Juma (sasa Prof. na ndiye Jaji Mkuu) Prof. Safari, Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo, Prof. Chris Peter Maina, Dr. Hamud Majamba, Tulia Akson, (sasa ni Spika, wakati huo hata u Dr. bado) kwa kuwataja wachache, walitufunza, moja ya maeneo magumu sana kwenye fani ya sheria, ni eneo la kutafsiri katiba na sheria, kiingereza wanaita, “Legal Interpretations” na kutokana na umuhimu wa eneo hili, kwa mujibu wa katiba yetu, taasisi pekee yenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni mhimili wa Mahakama, upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
  4. Tulifundishwa, katika kutafsiri sheria, mahakama inaangalia nia na dhamira ya mtunga katiba na mtunga sheria, au alidhamiria nini kutunga kipengele hicho kinachohitaji kutafasiriwa, hivyo ili kutafsiri kifungu chochote cha katiba, lazima kwanza wewe mfasiri uvae viatu vya mtunga katiba.
  5. Hivyo hapa mimi sio Mahakama, kutafsiri Katiba, bali naileta hii mada kama mwananchi wa kawaida tuu anayavijaribisha kuvivaa viatu vya mtunga katiba, alidhamiria nini wakati anatunga kifungu hicho, cha Katiba ninachotaka jicho la Mama Samia likiangazie, kwanza ni Ibara ya 5 ya msingi wa haki na dhamira ya mtunga katiba
  6. Ibara ya 5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura (na kupigiwa kura) katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi.
  7. Ibara ya 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
  8. Kifungu hicho ndio nia na dhamira ya mtunga katiba kwamba “kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao”
  9. Kumbe haki hiyo ya kikatiba, iliyotolewa na ibara 5 na Ibara ya 21 hiyo, imekuja kufanyiwa marekebisho kinyume cha katiba kwa kuipora haki hiyo ya msingi kwa kuichomekea ibara ndogo mbili ya 39 na 67 zinazoipora kabisa haki iliyotolewa na Ibara ya 5 na Ibara ya 21 ya katiba.
  10. Ibara hizo zinasema
  11. Ibara ya 39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama- (c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
  12. Ibara ya 67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
  13. Kwa mtu wa kawaida tuu ambaye sio mtaalamu wa kuisoma katiba, utakiona vipengele hivyo vya katiba viko sawa kabisa vinatoa haki kwa kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kumbe haki hizo zimeporwa kwa kuchomekewa sherti la kudhaminiwa na chama cha siasa, ambalo sio dhamira ya mtunga katiba.
  14. Ni Bunge ndio lilichomekea sherti hilo, la kudhaminiwa na cha siasa ni kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni kinyume cha Universal Declaration of Human Rights, ni kinyume cha The United Nations Human Rights Committee, ni kinyume cha African Chatter of People and Political Rights hivyo tunamuomba Rais Samia, lile jicho lake la haki, pia likiangazie kipengele hiki cha dhulma, ili kuwatendea haki Watanzania.
  15. Katiba ni mali ya wananchi, katiba hiyo inatungwa kwa misingi ya haki, Katiba imeweka haki ya wananchi kuchagua na kuchaguliwa na ikazifungia haki hizo kwa kuweka “ring fencing” Bunge la JMT lilipata wapi mamlaka ya kuipindua katiba ya JMT?.
Tukutane wiki ijayo, na kwa vile hii ni issue nyeti, ya kikatiba na kisheria, tutakwenda mdogo mdogo ambapo nita wapitisha taratibu, hatua kwa hatua, uhuni huu kuchomekewa ndani ya katiba yetu ilitokeaje tokeaje, kipengele hicho batili, kikachomekewa ndani na katiba yetu huku tuna wanasheria ma nguli na wabobezi wa katiba, ndani ya Bunge letu, tena akiwemo yule graduate wa Havard (Havard kilichopo Marekani, ndio chuo No. 1 cha sheria duniani, kikifuatiwa na Yale cha Uingereza) wapo wapo tuu na wamenyamaza huku wanaangalia katiba yetu inavyochezewa?.

Paskali
Kwa wale wapenda haki ambao mtapenda kujielimisha zaidi,
ukipitia mitaa hii, itakusaidia zaidi kunielewa ili twenda pamoja.
Anza na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!

Kisha njoo Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Paskali haya unayotaka tuyajadili ni madogo sana kuliko ya nchi kuendeshwa bila ya kufuata katiba, nadhani ingekuwa jambo jema ungeleta mjadala wa nchi iendeshwe kwa matakwa ya katiba, hilo bunge halikidhi matakwa ya katiba kwani lipolipo tu kwa matakwa ya wenye nchi.
 
Huyu rais wetu yeyote ambaye atakuwa madarakani kipindi chochote lazima 'awezeshwe' kwa 'lazima' kuongozana na Mwanasheria Mkuu ili kwamba mheshimiwa rais jambo lolote analolitaka kupitia tamko analotaka kutoa, kushawishi, kugawa fedha za walipa kodi, teuzi za wasaidizi wake n.k n.k kwa ujumla mambo yote ya kiuamuzi kama rais lazima apate ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali.

Je huyu mwanasheria mkuu wa serikali atakayekuwa na ubavu wa kumshauri ipasavyo apatikane kwa njia ya mchakatako gani ili awe huru kumshauri rais bila woga au hila huyu rais mwenye madaraka makubwa ?

25 September 2014

President Obama Delivers a Statement on Attorney General Eric Holder

On September 25, 2014 at the White House, President Obama offered thanked Attorney General Eric Holder for his six years of service.

In remarks from the White House State Dining Room this afternoon, President Obama announced that Eric Holder will be stepping down from his current position as U.S. Attorney General.

Assuming office in February 2009, Holder's nearly six-year tenure makes him one of the longest-serving Attorney Generals in U.S. history. He will continue to serve as Attorney General until the President nominates his successor, and the successor is confirmed by the Senate.

As the President noted, Holder's career in public service "began nearly 40 years ago as a young prosecutor in the Department that he now runs." Over his career, Holder has served at the Department of Justice under six U.S. presidents -- including serving as acting Attorney General at the beginning of President George W. Bush's first term.

Attorney General Eric H. Holder Jr.,  delivers remarks following President Barack Obama's statement announcing Holder's departure

Attorney General Eric H. Holder Jr., delivers remarks following President Barack Obama's statement announcing Holder's departure, in the State Dining Room of the White House, Sept. 25, 2014. Attorney General Holder will remain at the Department of Justice until his post is filled. (Official White House Photo by Chuck Kennedy)
"As younger men, Eric and I both studied law," President Obama said. "And I chose him to serve as Attorney General because he believes, as I do, that justice is not just an abstract theory. It’s a living and breathing principle."

It’s about how our laws interact with our daily lives. It’s about whether we can make an honest living, whether we can provide for our families; whether we feel safe in our own communities and welcomed in our own country; whether the words that the Founders set to paper 238 years ago apply to every single one of us and not just some.
That’s why I made him America’s lawyer, the people’s lawyer.

"I chose him to serve as Attorney General because he believes, as I do, that justice is not just an abstract theory. It’s a living and breathing principle."

-- President Barack Obama

Attorney General Eric Holder speaks at the National Action to Realize the Dream March

Attorney General Eric Holder speaks at the National Action to Realize the Dream March, August 24, 2013. (Justice Department photo by Lonnie Tague)
President Obama went on to detail the portfolio that Holder assumed as Attorney General --
from counterterrorism to civil rights, and from public corruption to white-collar crime -- emphasizing the "superb job" that Holder has done:

He’s worked side by side with our intelligence community and the Department of Homeland Security to keep us safe from terrorist attacks and to counter violent extremism. On his watch, federal courts have successfully prosecuted hundreds of terror cases, proving that the world’s finest justice system is fully capable of delivering justice for the world’s most-wanted terrorists.
He’s rooted out corruption and fought violent crime. Under his watch, a few years ago, the FBI successfully carried out the largest mafia takedown in American history. He’s worked closely with state and local law enforcement officers to make sure that they’ve got the resources to get the job done. And he’s managed funds under the Recovery Act to make sure that when budgets took a hit, thousands of cops were able to stay on the beat nationwide.
He’s helped safeguard our markets from manipulation, and consumers from financial fraud. Since 2009, the Justice Department has brought more than 60 cases against financial institutions, and won some of the largest settlements in history for practices related to the financial crisis, recovering $85 billion -- much of it returned to ordinary Americans who were badly hurt.
He’s worked passionately to make sure our criminal justice system remains the best in the world. He knows that too many outdated policies, no matter how well-intentioned, perpetuate a destructive cycle in too many communities. So Eric addressed unfair sentencing disparities, reworked mandatory minimums, and promoted alternatives to incarceration. And thanks to his efforts, since I took office, the overall crime rate and the overall incarceration rate have gone down by about 10 percent. That’s the first time that they’ve declined together, at the same tim, in more than 40 years.
The President noted that Holder's "proudest achievement," however, may be his efforts to reinvigorate and restore the Civil Rights Division of the Justice Department --

He has been relentless against attacks on the Voting Rights Act -- because no citizen, including our servicemembers, should have to jump through hoops to exercise their most fundamental right. He’s challenged discriminatory state immigration laws that not only risked harassment of citizens and legal immigrants, but actually made it harder for law enforcement to do its job.
Under his watch, the Department has brought a record number of prosecutions for human trafficking, and for hate crimes -- because no one in America should be afraid to walk down the street because of the color of their skin, the love in their heart, the faith they practice, or the disabilities that they live with.
He’s dramatically advanced the cause of justice for Native Americans, working closely with their communities. And several years ago, he recommended that our.....

READ MORE : Source : U.S. Attorney General Eric Holder Is Stepping Down After Six-Year Tenure
 
Huyu rais wetu yeyote ambaye atakuwa madarakani kipindi chochote kazima 'awezeshwe' kwa 'lazima' kuongozana na Mwanasheria Mkuu ili kwamba mheshimiwa rais jambo lolote analolitaka kupitia tamko analotaka kutoa, kushawishi, kugawa fedha za walipa kodi, teuzi za wasaidizi wake n.k n.k kwa ujumla mambo yote ya kiuamuzi kama rais lazima apate ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali.

Je huyu mwanasheria mkuu wa serikali atakayekuwa na ubavu wa kumshauri ipasavyo apatikane kwa njia ya mchakatako gani ili awe huru kumshauri rais bila woga au hila huyu rais mwenye madaraka makubwa ?

25 September 2014

President Obama Delivers a Statement on Attorney General Eric Holder

On September 25, 2014 at the White House, President Obama offered thanked Attorney General Eric Holder for his six years of service.

Hapa Tanzania asemacho rais ni sheria kwa miaka hii, niwakumbushe tu miaka iliyopita mzee Mwinyi akiwa rais, akiwa Mtwara kwenye sherehe za Mei Mosi masikini raisi alipandisha kima cha chini cha mshahara ila bahati mbaya kwa wakati ule angalau katiba ya nchi ilikuwa ikiheshimiwa, serikali haikutekeleza agizo hilo la jukwaani na mpaka kesho halijatekelezwa.
 
Ndiyo tatizo kubwa, hivyo rais awezeshwe kwa kulazimishwa kuwa, rais na taasisi ya urais mara zote mbele ya jamii lazima tuone akiongozana na mwanasheria mkuu vijijini, wilayani, mikoani, kuzindua soko la Kariakoo DSm n.k ili tuamini kuwa masuala yote ya kikazi ikiwemo sera, matamko yake yote, ugawaji wa fedha za miradi, ugawaji wa mipaka ya maeneo, teuzi za wasaidizi * (wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya ), sherehe za kitaifa, n.k anazifanya kwa mujibu wa katiba inavyosema. Hii ni ili kuondoa kisingizio cha kushauriwa vibaya, kutopewa taarifa sahihi n.k

Maana rais ni binadamu hana uwezo wa kufahamu kila kitu au tukio hivyo awezeshwe ili awajibike ipasavyo bila ya baadaye wasaidizi wake kuja na visingizio vya kuwa rais muda ule alikosa ushauri sahihi kumbe hatukumuwezesha kwa kumpa washauri wa karibu kabisa muda wote na mahali pote.
 
Back
Top Bottom