Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 45,931
- 102,002
Wanabodi,
Paskali
Kwa wale wapenda haki ambao mtapenda kujielimisha zaidi,
ukipitia mitaa hii, itakusaidia zaidi kunielewa ili twenda pamoja.
Anza na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
Kisha njoo Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ikiwa ni kwa njia ya swali fikirishi "Jee Jicho la Rais Mama Samia Suluhu Hassan, litaweza kuangazia ubatili huu ndani ya Katiba tetu, unaopora haki ya msingi ya kushiriki uchaguzi kwa kugombea, uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha tuu?.
- Hii ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya pili ya mada hii nilioianza wiki iliyopita kuhusu wema wa Rais Samia ambaye ni mpenda haki, na mtenda haki, na jinsi anavyoliponya taifa kupitia wema wake na kutenda haki kwake, Makala ya wiki iliyopita ni hii HAPA! nikaahidi, kuanzia wiki hii, nitaangazia baadhi ya vifungu vya katiba yetu, vinavyonyima haki, zilizotolewa na ibara moja, zikaja kupokonywa na ibara nyingine, kwa kuchomekewa vipengele vinavyoipora haki hiyo, na kuchomekwa kiubatili ndani ya katiba yetu systematically ili kuvihalalisha kikatiba, wakati kiukweli kabisa vifungu hivyo ni batili na vimechomekewa kiubatil na viko kinyume cha nia njema ya mtunga katiba hivyo hapa nina viangazia kwa kuvimulikia ili jicho la haki la Rais Mama Samia livione viondolewe, ili kuwatendee haki Watanzania.
- Nimepata bahati kusomea sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM na kufunza na waalimu manguli kabisa na wabobezi wa sheria, na hawa ni baadhi ya waalimu wetu, kina Prof. Issa Shivji, Prof. Palamagamba Kabudi, Prof. Sifuni Mchome, Dr. Ibrahim Juma (sasa Prof. na ndiye Jaji Mkuu) Prof. Safari, Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo, Prof. Chris Peter Maina, Dr. Hamud Majamba, Tulia Akson, (sasa ni Spika, wakati huo hata u Dr. bado) kwa kuwataja wachache, walitufunza, moja ya maeneo magumu sana kwenye fani ya sheria, ni eneo la kutafsiri katiba na sheria, kiingereza wanaita, “Legal Interpretations” na kutokana na umuhimu wa eneo hili, kwa mujibu wa katiba yetu, taasisi pekee yenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni mhimili wa Mahakama, upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
- Tulifundishwa, katika kutafsiri sheria, mahakama inaangalia nia na dhamira ya mtunga katiba na mtunga sheria, au alidhamiria nini kutunga kipengele hicho kinachohitaji kutafasiriwa, hivyo ili kutafsiri kifungu chochote cha katiba, lazima kwanza wewe mfasiri uvae viatu vya mtunga katiba.
- Hivyo hapa mimi sio Mahakama, kutafsiri Katiba, bali naileta hii mada kama mwananchi wa kawaida tuu anayavijaribisha kuvivaa viatu vya mtunga katiba, alidhamiria nini wakati anatunga kifungu hicho, cha Katiba ninachotaka jicho la Mama Samia likiangazie, kwanza ni Ibara ya 5 ya msingi wa haki na dhamira ya mtunga katiba
- Ibara ya 5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura (na kupigiwa kura) katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi.
- Ibara ya 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
- Kifungu hicho ndio nia na dhamira ya mtunga katiba kwamba “kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao”
- Kumbe haki hiyo ya kikatiba, iliyotolewa na ibara 5 na Ibara ya 21 hiyo, imekuja kufanyiwa marekebisho kinyume cha katiba kwa kuipora haki hiyo ya msingi kwa kuichomekea ibara ndogo mbili ya 39 na 67 zinazoipora kabisa haki iliyotolewa na Ibara ya 5 na Ibara ya 21 ya katiba.
- Ibara hizo zinasema
- Ibara ya 39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama- (c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
- Ibara ya 67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
- Kwa mtu wa kawaida tuu ambaye sio mtaalamu wa kuisoma katiba, utakiona vipengele hivyo vya katiba viko sawa kabisa vinatoa haki kwa kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kumbe haki hizo zimeporwa kwa kuchomekewa sherti la kudhaminiwa na chama cha siasa, ambalo sio dhamira ya mtunga katiba.
- Ni Bunge ndio lilichomekea sherti hilo, la kudhaminiwa na cha siasa ni kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni kinyume cha Universal Declaration of Human Rights, ni kinyume cha The United Nations Human Rights Committee, ni kinyume cha African Chatter of People and Political Rights hivyo tunamuomba Rais Samia, lile jicho lake la haki, pia likiangazie kipengele hiki cha dhulma, ili kuwatendea haki Watanzania.
- Katiba ni mali ya wananchi, katiba hiyo inatungwa kwa misingi ya haki, Katiba imeweka haki ya wananchi kuchagua na kuchaguliwa na ikazifungia haki hizo kwa kuweka “ring fencing” Bunge la JMT lilipata wapi mamlaka ya kuipindua katiba ya JMT?.
Paskali
Kwa wale wapenda haki ambao mtapenda kujielimisha zaidi,
ukipitia mitaa hii, itakusaidia zaidi kunielewa ili twenda pamoja.
Anza na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
Kisha njoo Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.