Je, JF tumefungwa bao au tunajifunga wenyewe ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, JF tumefungwa bao au tunajifunga wenyewe ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Nov 10, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mtu akisoma kwa makini mijadala inavyoendelea humu ndani atagundua mara moja kuwa tumeanza kujenga katabaka humu ndani ya sisi na wao. Kwa Tanzania yetu kama tunavyoijua hili halishangazi hata kidogo kwa sababu karibu wote tumetumbukia kwenye haka ka ugonjwa wa kuita koleo kijiko kwa vile tu nafsi zetu hazikubali ukweli kuwa zinatawaliwa na vitu vitatu - rushwa, tamaa na unafiki. Hivi sasa ni vigumu kumpata Mtanzania ambaye haangukii kwenye moja wapo ya hizo sifa na matokeao yake kuzaa mwenzetu na si mwenzetu.

  Nitaanza kwa kukichambua CCM kwani ndicho si tu kimeshika usukani bila kimechangia kwa kiwango kikubwa kutufikisha hapa. Nje ye CCM, anayeshabikia chama chochote kingine sio tu si mwenzao bali huonekana adui anayehatarisha hali ya usalama na amani. Ndani ya CCM, anayekuwa na mawazo tofauti sio tu anaonekana si mwenzao bali huwa kama msaliti anayetaka kukigawa chama. Hivyo usalama ndani ya CCM ni kuwa mwenzao na ikiwezekana kufumbia macho maovu - huu unaitwa unafiki.

  Wadhifa ndani ya CCM integemea utakavyowawezesha wanachama kujua uzito wa ujumbe wako kwa kutumia hali na mali. Kijijini kwenye umasikini chumvi na sukari inaweza kabisa ikatosha kukuzolea kura kibao na mjini kiwango cha ushindi utaendana na ukubwa wa mshiko. Kwa wafanya biashara na matajiri wakubwa ahadi tu za upendeleo zinakuhakikishia tsunami ya mafanikio. Mambo yote haya hufanyika kwenye karibu ngazi zote za uchaguzi na hoja si hoja tena - kwa maneno mepesi hii huitwa rushwa.

  Katika maisha ya binadamu , hakuna asiyependa utajiri, hakuna asiyependa kuwa na nyumba nzuri na hakuna anyeona raha watoto wake kulala njaa. Lakini baba anayepata habari kwamba hela zote anazoletewa na mwanae zinatokana na wizi, akiamua kukaa kimya na kuzitafuna, je atashangaa siku mwanawe anafungwa ama kuuwawa kwa wizi ama ujambazi. Je watoto wake wengine si ndio anawafundishwa kuwa wizi ni ruksa mradi hukamatwi ? Ndani ya CCM, tamaa inakomazwa kuanzia vijana.

  Humu JF tumeanza kushuhudia haya ya CCM ya sisi na wao yakianza kushika kasi kwa nguvu ya ajabu. Rushwa haiitwi rushwa labda iwahusishe watu fulani tu, unafiki sio unafiki labda kwa kikundi fulani tu, tamaa ni zao ni zetu. Wizi unatetewa kwa kuangalia itikadi, rushwa inatetewa kwa kuangalia jina la mtu, uzembe utatetewa kwa kuangalia dini ya mtu ili mradi tunatafuta namna ya kutokumbebesha mzigo anayehusika kwa kuwa yuko kundi fulani - sisi na wao.

  Na sasa kibaya zaidi ni kujaribu kuwatenga tunaotofautiana nao kwa kuwaona ama si wenzetu au ni wasaliti. Siyo tu tunajenga CCM humu ndani lakini tuna NEC wanaofikiria wana majukumu mazito zaidi kwa nchi yetu kuliko wengine. Watu wanatumiana PM kwa mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu na hivyo kupotosha nia halisi ya JF - kama una ya kumwaga yamwage humu na kama hutaki kwa nini kwa mfano msianzishe jukwaa lenu la kuwasiliana na si kutumia mgongo wa JF.

  Inanikumbusha bunge letu linapotumiwa kama kitengo cha CCM na mambo mazito ya nchi yakajadiliwa humo wakati wa kikao cha Bunge. Kwenye vikao hivi hata Spika anaweza kuwekwa kiti moto kuhusiana na maamuzi ya Bunge wakati idadi ya wabunge wa CCM ndani ya Bunge ni asilimia zaidi ya 80%. Kwa nini hoja itolewe bungeni kuliko na wawakilishi wa wananchi wote na kujadiliwa kwenye vikao vya CCM - inakuwaje washindwe kutetea hoja hiyo ndani ya bunge - huu nauita ufisadi wa hoja.

  Lazima tukubali wana JF tumepigwa bao na sasa wapinzani wetu wanaangalia tu na kuchekelea tunavyoendelea kujifunga wenyewe kila kukicha.
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  MAG ยง

  Nimependa tafsiri yako ya unafiki. Je maana ya unafiki inaishia hapo tu? Kwa kuanza tu, unaioanisha vipi huu unafiki na JF kufungwa bao au kujifunga wenyewe.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mag3,

  Heshima yako bro, hii nilikuwa sijaiona, hili hapo juu linanihusu sana mimi na sina tatizo kulijibu, ni kwamba kwanza sijawahi kumtumia mtu ujumbe wa aina yoyote wa dataz za siasa kwa kutumia PM ya JF, unless ulikuwa unazumgumzia member mwingine,

  Yes, kwa kawaida kuna members ambao wengi tunajuana in the real life, ambao sio tu tunatumiana PM, bali huwa tunawasiliana kwa njia mbali mbali, na kwa mambo mbali mbali mpaka ya harusi zetu, na hata siku moja hatujawahi ku-compromise misimamo yetu kwenye JF kwa sababu ya kuwasiliana nje ya forum, huwa tunapigana mawe kama kawaida,

  Mtu akiwa na habari za siasa ambazo ni nyeti sio lazima aziweke wazi, na kuna sababu mbali mbali na muhimu kuliko zote ni kuogopa kuwa-compromise wanaotoa hizo habari, zingine zinakuwa hazina uhakika, zingine zinakuwa sio njema kwa jamii, lakini the bottom line ni kwamba habari zangu siwezi kulazimishwa na anybody kuziweka mahali popote, not only JF, na ni haki yangu kumpa yoyote ninayetaka, na sijawahi kutumia PM ya JF kwa shughuli kama hiyo, never!

  Sasa unless ulikuwa unamuongelea mwingine lakini kama ni mimi ninasema hivi I have nothing to do na uliyoyasema, na nirudie tena ni haki yangu kuja hapa JF kuweka mawazo yangu, na ni haki yangu kisheria ya jamhuri kushabikia chama ninachokipenda cha siasa, na kiongozi yoyote yule ninayemuona kwangu anafaa, ninaamini kuwa tupo hapa JF kulisaidia taifa letu, naona recently tunaanza kujaribu kugeuziana kibao as if humu kuna Rais wa jamhuri, as if hapa tuna Waziri Mkuu Pinda,

  Hapana hapa tupo wananchi, ninaamini wenye uchungu na taifa letu, sasa hatuwezi kuwa sawa kwa mtizamo of how kuleta changes kwa taifa, kutofautiana kimawazo ni lazima na ni kawaida, lakini tusianze kubebeshana mizigo isiyo sahihi kwa sababu tu hatukubaliani mawazo yetu kisiasa, ninarudia tena kwamba hizi taarabu haziwezi hata siku moja ku-accomplish anything positive, zaidi tu kuzidisha chuki ambazo in the end haziwezi kumbadili anybody hapa, tatizo la taifa haliko JF wala kwenye watu wa JF, tunajua lilipo ndio maana tupo hapa.

  Kwa kumaliza ni kwamba habari zangu za aina yoyote sio lazima niziweke JF, na pia sijawahi kutumia PM kwa habari hizo, lakini ninaitumia PM yangu kwa sababu niliyopewa tena inachukua mesaage 1000 kwa hiyo nina uhuru wa kuitumia nitakavyo, bila kuingiliwa na member mwingne, sheria za JF kuhusu PM na sekta zote nyingine ninazijua toka mwaka 2006 nilipoojiunga na JF, sihitaji kuja kufundishwa leo na member mwingine that is pathetic! Na nitaendelea na hiyo tabia ya kuwasiliana na member wengine nje ya hapa kwa kupashana habari za taifa letu, na hatuna haja ya kuanzisha foum nyingine, kama ni dhambi kwa yoyote hapa so be it lakini haijavunjwa sheria ya JF kwa kuwasiliana nje ya JF.

  Ahsante Mkuu!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  PM ni moja ya features za JF kuna mambo members wangependa wawasiliane privately hakuna ubaya kwenye hilo
   
 5. C

  CRITICAL MIND JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2016
  Joined: Sep 1, 2013
  Messages: 402
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  just bumping this relevant thread....
   
Loading...