Je Jerry Muro atatumia mbiinu na taratibu zipi za kisheria zitakazoweza kumnasua kwenye kesi yake?

kwa jinsi nilivyofuatilia kidogo kutokana na maelezo yaliyotolewa na walalamikaji inaonyesha wazi kuwa kuna mambo ya kubishaniwa kwenye shitaka hilo nafikiri hilo ndiyo limepelekea mahakama isitupilie mbali hilo shitaka. Kuna sababu nyingi ila nafikiri unyeti wa kesi yenyewe pamoja na kuweka imani kwa vyombo vilivyohusika kufungua shitaka nahisi ni baadhi ya mambo yaliyosababisha kesi isikilizwe aidha ieleweke wazi kuwa kuna mashitaka kadhaa ambayo yamefunguliwa kwenye kesi hiyo kwa mfano ishu ya Jerry Murro kumiliki pingu, bastola ni baadhi ya mambo ambayo nahisi ni lazima ayatolee maelezo ya kutosha mbele ya mahakama, shitaka la kuomba rushwa sidhani kama lina ushahidi wa kutosha kwani kuna maswali mengi ambayo upande wa mashitaka utalazimika kujenga hoja za kueleweka ili kuifanya mahakama iridhike na ushahidi huo.
 
Back
Top Bottom