Je, Israel itaweza kushambulia vinu vya nuclear Iran?

Kinaendelea kunuka Iraq mda huu

Four attacks on #US military convoys in #Iraq in one day

In four separate attacks, Iraqi resistance groups targeted US military convoys near Samawah in Muthanna province, Nasiriyah in Dhi Qar province, al-Diwaniyah in Qadisiyah province and Babil province
US WILL NOT ATTACK IRAN.
NEITHER US NOR IRAN WANT WAR FOR THIS TIME. MAY BE LATER BUT NOT NOW!!
SO STAY COOL NOTHING WILL HAPPEN.

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
Nyie watu bwana mwanzo mlisema IRAQ iwezekani mwisho wasiku mkashuhudia jamaa anapigwa kamba ya shingo kweupeeee mara mkasema SYRIA matokeo yake mmeona leo mmeanza Iran ikipigwa nayo mtasema ooh SOMALIA Duu yaani hamchoki
Scott Ritter:

If we get into a war with Iran, we will not win, (we - being the United States)

Iran has a significant ballistic missile force, with an extraordinary capability.

It’s Capable of targeting American naval vessels, sinking American aircraft carriers,..... https://t.co/yrOnRQDVWj
 
Hujui mbinu za medani
Usije ukashangaa hizi nuke za Iran zikalipuka Iran huko huko!
Muda utasema!
Scott Ritter, former United Nations weapons inspector in #Iraq:

We cannot destroy Iran. We lack the military capacity to defeat Iran.

We can damage #Iran, we can harm Iran, but we cannot compel their surrender, and we cannot overthrow the regime. https://t.co/nWMZLajAVj
 
Jamii ya kiyahudi ndio imeshikilia congress ya ya US pia kama unafahamu "deep state" ya US imetawaliwa na wahayudi hadi wenyewe wanalalamika
Mkuu hizi sio conspiracy! Congress ina member wangapi, na kati ya hao Israelites ni wangapi na je congress kuwa run na waisrael inathibitisha nchi kuongozwa na waisrael? US bana inaongozwa na sera ya kuwapa nafasi intellectuals wa mataifa mbalimbali kwenda kujenga nchi yao, wanaweza kuwa waisrael, wajerumani, warusi, wajapan au watanzania. Hizi habari za deep state hazina ushahidi wowote zaidi ya hisia tu za watu so huwa sitaki kuziongelea katika jukwaa kama hili labda tungekuwa kijiweni
 


Rudi kwenye search engine badala ya Jews weka watu wa mataifa mengine kama Germany, Arabs, Chinese, Russians, English nk uone kama hautopata majibu yale yale.. Hizi habari za wayahudi kuiongoza USA zinaanzishwa na anti jews ili kujenga hisia za chuki kwa wamarekani dhidi ya wayahudi kwa kuwa lengo ni kuamsha hisia miongoni mwa wamarekani kwamba nchi yao imetekwa na wayahudi. Hata Hitler alianza hivi kupata sababu ya kuwaangamiza wayahudi. So pro Israel kuweni makini na hizi sifa mnazowapa wayahudi, mnacheza ngoma ya wasiowatakia mema wayahudi. Shauri yenu
 
Mkuu hizi sio conspiracy! Congress ina member wangapi, na kati ya hao Israelites ni wangapi na je congress kuwa run na waisrael inathibitisha nchi kuongozwa na waisrael? US bana inaongozwa na sera ya kuwapa nafasi intellectuals wa mataifa mbalimbali kwenda kujenga nchi yao, wanaweza kuwa waisrael, wajerumani, warusi, wajapan au watanzania. Hizi habari za deep state hazina ushahidi wowote zaidi ya hisia tu za watu so huwa sitaki kuziongelea katika jukwaa kama hili labda tungekuwa kijiweni
Mkuu umenena vyema, wayahudi wenyewe wanakataa hili kwamba wao wanaongoza USA, kuna mtu nimemjibu kwenye huu uzi, hizi theory zinatokana na makundi ya kibaguzi (white supremacist) wenye chuki juu ya jews, ni sawa na hapa kwetu usikie serikali imekaliwa na rwandese, hili lazima lijenge chuki dhidi ya rwandese.

Sasa wenzetu wanaona kusema jews wana control USA wanafikiri ni sifa kwamba jews are superior.
 
Tarehe 7 June 1981 Israel ilifanya mashambulizi katika vinu vya nuclear huko Iraq,hii ilikuwa ni shambulizi la ghafla katika mradi huo chini ya Sadam Hussein, hii ilijulikana kama operation opera au Operation Babylon, Kinu kilichojulikana kama Osirak Nuclear Reactor kilichokuwa kusini mashariki mwa Baghdad kiligeuzwa majivu, hakika lilikuwa shambulizi la ghafla na hakuna aliyetarajia.
Katika shambulizi hilo watu 11 walifariki ikiwamo raia mmoja wa kifaransa na askari wa Iraq 10.

Hata hivyo hapo 2005 professor wa utafiti katika fizikia kutoka chuo cha Havard alisema kuwa kinu cha nuclear cha Osirak kilitengenezwa na engineer wa France Yves Girard maalumu kisiwe na uwezo wa kutengeneza silaha za nuclear, lakini Israel bado iliona ni hatari kwao na walitaka kufanya mashambulizi juu ya kinu hicho.

SHAMBULIZI IRAQ.

Hapo 7 june 1981 Israel Air Force walitekeleza shambulizi hilo, zilikuwa ndege zipatazo 8 aina ya F-16A zikiwa zinapewa ulinzi na F-15A zipatazo sita, F-16 zilikuwa na mabomu heavy yajulikanayo kama mark-84 haya ni delay-reaction bombs, kila F-16 ilibeba mawili, jamaa waliruka toka Israel wakapita anga la Jordan na Saudi zaidi kilomita 1000 bila kujulikana mpaka walipofika Iraq, ndege zilifika zikaachia mabomu 16 heavy kwenye kinu hicho halafu wazee wakatembea kama sio wao, haya ni aina ya mabomu yanayolipuka baada ya muda fulani(delay-reaction bomb).

Moja ya vitu vilivyorahisisha Israel kufanya shambulizi lao ni katika wakati huu Iran na Iraq walikuwa wamekamatana(Iran-Iraq war), huu ukawa ni mtelezo kwa Israel kutekeleza shambulizi hilo, mradi huu France ndiye aliyetoa wataalamu na pia kuwapa training wanasayansi wa Iraq, hata katika shambulzi mfaransa mmoja aliuawa, Iraq walitoa pesa ndefu sana ($300 million) kwa France, gharama ikijumuisha kupelekwa kwa wataalamu na uranium kilo 72, mwaka 1975 jamaa walisaini waanze mradi na hapo 1976 mradi ulianza rasmi.

Israel ilitaka kufanya shambulizi toka 1979 lakini kuna vitu vilipaswa kukamilika ili wafanye operation hio, unaweza ukacheka sana jinsi watu walivyo kimaslahi nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.

France walikula pesa za Sadam wakalala mbele $300 (sawa na $1.4 Bilion-(2020)) kwa mwaka 1975 ilikuwa ni pesa ndefu mno, tena France iliwakingia kifua Iraq kuwa ulikuwa ni mradi salama na dunia haikupaswa kuwa na wasi wasi wowote juu ya hilo, mradi huo ulikuwa chini ya uangalizi wa IAEA lakini USA na Israel walikuwa na wasiwasi juu ya hilo.

1978-1979 yanafanyika mapinduzi Iran(Islamic revolution) kwa kumtoa Shah Mohammed Reza Pahlavi na serikali yake na kuweka Islamic Republic chini ya Ayatollah Khomeini tunaweza kusema kwamba Shah na serikali yake walikuwa ni pro-Western wakati Ayatollah ni anti-Western, USA ilichukizwa sana juu ya jambo hili kwani 1979 Iran tayari ilikuwa ni Islamic republic, kwa kweli yalikuwa ni maandamano makubwa hasa ya kupinga serikali iliyopo ni stori ndefu long short kulitokea uharibifu mkubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe(Iran) ni katika wakati huu Iran ilikuwa weakened.

1980 Sadam anaiona Iran ipo weak kutokana na mapinduzi ya 1979, vikwazo walivyowekewa na umoja wa mataifa ikiongozwa na US na pia kutengwa kimataifa, Sadam hakika alikuwa amewekeza vya kutosha katika silaha katika jeshi la Iraq baada ya kuwa defeated na Iran hapo 1975.

Nilikuwa naelezea jinsi maslahi yanavyoweza kufanya hata rafiki yako au ndugu akusaliti lakini naomba nielezee kidogo kuhusu Iran ili twende sawa.

Kabla ya vita hii ya 1980 iliyochukua takribani miaka 8 kati ya Iraq na Iran, Iraq ilidhibitiwa ipasavyo na Iran hapo 1975 hiki ndicho kilichopelekea Sadam kununua silaha za kutosha, Iraq ilinunua vifaru 1600, armoured Personel Carriers na ndege vita za kirusi 200, hadi kufikia 1980 Iraq ilikuwa na askari 242,000 vifaru zaidi ya 2300 na ndege vita 340.

Katika wakati huo ilikuwa ikitoka Egypt kuwa na askari wengi ilikuwa inafuatia Iraq katika ulimmwengu wa waarabu, 1980 intelejensia iliyofanywa na Iraq walibaini kuwa Iran hana lolote wala chochote, pia walibaini kuwa hata uwezo wa Iran kuzuia mashambulizi ni mdogo, wataweza kumshambulia na kummaliza mara moja kwa kuchukulia advantage ya Iran kuwa weak baada ya mapinduzi ya mwaka 1979, Najua tupo katika mada inayozungumzia kama Israel itaweza kumshambulia Iran au la, lakini nimepiga kona nyingi lengo ni tufahamu kwanza mambo muhimu yatakayotupa mwanga hapo mbeleni.

Ahsante....... tuendelee...

Nilisema Iraq ilidhibitiwa 1975 na Iran kabla ya ile vita ya 1980-1988, sasa chanzo kilikuwa ni nini? ilikuwa hivi:

Kuna mto unaitwa Shatt al-Arab, mto huu unaweka mipaka kati ya Iran na Iraq kabla ya kumwaga maji yake kwenda Persian Gulf, kutokana na umuhimu wake nchi zote Iraq na Iran kwa miaka zimekuwa zikitetea haki zao juu ya uhuru wa kutumia mto huo ikizingatiwa ilikuwa ni mahala muhimu pa kufanya oil exportation kwa Iran na Iraq, kulikuwa na mzozo wa muda mrefu mpaka pale 1937 waliposaini mkataba kumaliza mzozo wao juu ya eneo hilo, ushirikiano uliendelea vizuri mpaka pale 1968 Iraq ilipotaka kuchukua mto uwe chini yake kimabavu hivyo kuwa na mamlaka juu ya mto huo.

1969 Iran ilijitoa kwenye yale makubaliano ya 1937 waliyofanya na Iraq ni baada ya Iraq kukiuka makubaliano hayo, Wakati huo huo serikali ya Iraq ilikuwa na mvutano na wakurdi wakati Iran iki support waKurdi, Iran ilikataa kutoa ushuru kwa Iraq wakati meli zake zilipotumia njia hio ya maji, Hapo kukawa na mvutano mkali, Mwaka 1971 Iraq sasa ikiwa chini ya Sadam, Iran iliwakaribisha wakurdi nyumbani kwao kwa kuwapa base za kijeshi na silaha.

Mwaka 1974-75 ndipo Iran na Iraq wakakamatana ilikuwa ni march 1974 mpaka march 1975, Iran ikiwa inawapa support waKurdi, Iraq ilituma vifaru ndani ya Iran lakini Iran walijibu mashambulizi na kuwazidi Iraq, wakitumia jeshi la anga la Iran, Iran waliishinda Iraq ki wepesi.

Iraq wakaona hali imekuwa ngumu wakaamua kurudi kwenye makubaliano juu ya mto Shatt al-Arab na hapa walisaini mkataba uliojulikana kama Algiers Agreement.

Kumbe mzee Sadam alikuwa bado ana duku duku juu ya Iran iliyokuwa chini ya Shah baada ya kupewa kichapo, labda niseme tu Iran walikuwa ni nchi ya tano duniani katika nguvu za kijeshi wakati huo, Sasa ndio naanza kurudi tuelewane niliposema kwamba watu na maslahi.

Sadam alikuwa anataka mapinduzi yakiongozwa na Ayatollah ili kuitoa serikali ya Shah yafanikiwe, Shah alikuwa adui wa Sadam na Ayatollah, baada ya mapinduzi kufanikiwa mwaka 1979 kuna mengi sana kwa kweli yalitokea Iran, machafuko makubwa ya wao kwa wao, mauaji ya hapa na pale, marekani ilikuwa karibu na Iran kipindi cha Shah hivyo baada ya mapinduzi Iran iliingia kwenye msoto mkali baada ya kutengwa na kuwekewa vikwazo vikali, mataifa mbali mbali hayakushirikiana tena na Irani kibiashara, Sadam pembeni kumbe bado alikuwa ana lile wazo lake la kuchukua eneo la mto ule, ndio maana jamaa alinunua silaha za kutosha ili kuimalizia kabisa Iran lengo ni iraq iwe super power Middle East.

WATU NA MASLAHI ASIKUAMBIE MTU

Sadam ana msupport Ayatollah ili mapinduzi yakifanyika Iran iwe weak yeye amgeuke tena Ayatollah amshushie kichapo atengue makubaliano ya ule mkataba wa Algiers, ajimilikishe mto wa Shatt al-Arab na aiache weak Iran ili awe super power pale middle East.
Sadam alikuwa amefanya maandalizi tayari na ilipofikia mwaka 1980 ulikuwa ni wakati muafaka kwa Iraq kuanza kusudio lao, Sadam akiwa na wafuasi wake waliompa support ikiwemo Saudia Arabia, Kuwait na nchi nyinginezo za uarabuni.

Sasa naomba tuelewane wazee, naomba mkae kimya, ipo hivi...

1-Iraq ilikuwa imejiandaa kijeshi kwa kuongeza silaha kama vifaru, ndege na jeshi kuikabili Iran.

2-Marekani waliwapa Iraq satelite ya kufanya intelligence na silaha za kibaiolojia(bio-weapon).

3-Iraq walipewa washauri wa kivita 90 toka Britain na US kusaidia majeshi ya Iraq ili kuwasaidia mahala wanapaswa kupiga toka angani na ardhini.

4-Saudia,Kuwait na waarabu wengine walitoa msaada wa pesa n.k. kwa Iraq.

5-Umoja wa kisovieti walikuwa na chuki na Iran katika wakati huu, hii ni kutokana na Iran kukiua chama cha kikomunisti(Tudeh Party) kilichokua Iran, hivyo USSR ilipeleka msaada wa silaha za kutosha kwenda Iraq zikiwemo ndege vita, helicopters za uchukuzi n.k.

Iran walikuwa hawana pesa ya kununulia silaha kama Iraq tokana na vikwazo.
Libya,Syria na North Korea ndio waliompa msaada Iran, ndege vita zao zilikuwa za kimarekani na wataalamu wa kufanya maintanace ya vyombo hivyo walikuwa ni US wenyewe , but how wali survive kwa miaka 8 wakipambana na Iraq iliyokuwa inapewa back-up na USSR, US,Britain na nchi toka Persian Gulf na bado Iraq hakuibuka mshindi?
(naomba niandae kuhusu andiko hili kwa urefu next time. Ahsante).

Nirudi tena kwenye mada, nilikuwa nasema kuwa Israel ilitaka kufanya shambulizi kwenye kinu cha nuclear cha Iraq mapema 1979, lakini walikuja kufanya shambulizi hilo 1981, unajua ni kwa nini? kuna kitu kilikuwa hakijakamalika, je ni kitu gani hicho?
Mapema kabisa Israel walijua mradi unaoendelea huko Iraq, lakini Israel walihitaji picha za kiintelejensia ya eneo husika na kinu hicho, hapa ndipo Iran wakatekeleza, ndege ya Iran aina ya F-4 Phantom ilichukua picha katika kinu hicho cha Osirak, picha zilihifadhiwa kwa usiri mkubwa na kutumwa kwenda Israel, na hapo Israel wakaanza ku plan sasa kuhusu operation Opera, wazee wakaanza mazoezi wakitumia ndege aina ya A-4 skyhawk kabla ya kupokea F-16 kwa ajili ya mashambulizi ya kinu hicho.

Katika wakati huu Iran na Iraq vita imechachamaa na Israel anaona ndio mwanya kwao kufanya maangamizi kwa sababu Iraq Air Force walikuwa busy wakichapana na Iran. Kuna kisa kimoja ndege ya Israel aina ya F-4 iliyokuwa ikifanya intelligence huko Iraq,ilikimbizwa na mig-21 ya Iraq, ndege ya Iraq mafuta yakaisha ikawa rubani aka eject na kuiacha F-4 kupepea, kupitia mission hizo Israel iligundua upenyo Iraq wa kupitia upande wa Saudia ambapo radar za Iraq zilikuwa hazimuliki, hii ni kwa sababu Saudia alikuwa anampa Iraq msaada kumtwanga Iran, hivyo Iraq iliona hakuna haja yeyote kuweka sana ulinzi huko kwani wana mahusiano mazuri na Saudia na hawatarajii kuingia vitani.

Sasa tuendelee...

Israel walikuwa na wasiwasi na Iraq kutokana uwezo wa mig-21, lakini Iraq ilikuwa vitani which is ni upenyo kwao kutekeleza mission yao, sasa sikia hii.

Mwaka 1981 april 4 jeshi la anga la Iran lilifanya shambulizi katika base iliyojulikana kama H-3 airbase ya Iraq iliyoko karibu na Jordan na Israel ndege 8 za jeshi la anga la Iran zilizokuwa zimebeba makombora ya masafa walipiga kambi hio, ambapo ndege takribani 48 za Iraq ziligeuzwa vyuma chakavu hata hivyo US walikuja na taarifa kwa kusema ndege 27 tu ndio ziliteketezwa huku 11 zikiharibiwa, moja ya ndege zilizoharibiwa ni pamoja na Tu-22 Blinder mbili na Tu-16 Badger tatu.

Labda niweke mambo sawa hizo ndege tatu aina ya Tu-16 Badger hizo ni strategic bombers za kirusi, ni ndege hatari ambazo zilikuwa threat kwa Israel, ninaposema strategic bomber ni ndege zile zinaweza kusafiri umbali mrefu sana pia zinaruka juu sana kiasi kwamba huzioni halafu zinaanza kunya mabomu, we unachoona ni mvua tu ya mabomu toka angani, ndege haionekani.

niendelee.....

Baada ya shambulizi hilo Israel waliona ni nafasi ya pekee kwao, Kwani ulikuwa ni muda muafaka wa kutekeleza mashambulizi, kama vile mig-21 ya Iraq ilivyoonyesha uwezo wa kuitoa nduki F-4 ya Israel ina maana Iraq Air Force ilikuwa threat kwa Israel na sasa kutokana na shambulizi hilo lilipunguza uwezo wa jeshi la anga la Iraq kujibu mashambulizi, hii ilipelekea Iran kuwa superiority kwenye anga la Iraq, Israel iliona sasa Iraq imepigwa rungu kwenye viwiko na magoti na nguvu imewaishia.

SHAMBULIZI
Ndege za Israeli ziliondoka Etzion Airbase, zikiruka bila kuzuiwa katika anga ya Jordan na Saudi. Ili kuepusha kugundulika, marubani wa Israeli walizungumza kwa Kiarabu chenye lafudhi ya Saudia wakiwa katika anga ya Jordan na kuwaambia Jordan kuwa walikuwa doria ya Saudia ambayo ilikuwa imepotea njia.

Walipokuwa wakiruka juu ya Saudi Arabia, walijifanya kuwa Wajordani, wakitumia ishara na mifumo ya redio za Jordan.
Long story short Israel walipiga kinu cha nuclear na wakapotea, kilikuwa ni kitendo cha dakika mbili tu.

Niseme tu kwamba Iraq ilikuwa vizuri kweli kweli, mfano hizo strategic bomber walizokuwa nazo ilikuwa ni tishio sana, israel hawakuwa na bombers zenye uwezo wa kwenda mbali kama hizo za Iraq, hata hivyo Israel haihitaji bombers kama hizo tokana na targets zao zipo eneo ambalo hata F-16 Fighting Falcon zinafika. Lakini niseme tu bomber kama hizo ilikuwa ni tishio kwa Israel.

View attachment 1656870

Watu na maslahi, US ana support Iraq impige Iran na Iran anampatia Israel picha za vinu vya nuclear Israel ili vilipuliwe , kama tujuavyo Israel ni mshirika wa US lakini akaamua kumtwanga Iraq, huku wafaransa wamekula pesa za uranium za Iraq wamelala mbele, niseme tu sitaki kuamini kama France hawakujua kwamba one day Israel atavigeuza vinu hivyo vya Osiraq kuwa jivu which means walijua walichofanya, hizi kazi za intelligence kuna mambo mazito, France walijua fika Israel haiwezi kukubaliana na nchi kama Iraq kuwa na reactor,mimi nahisi Iraq ilifanyiwa movie.

niendelee...

SHAMBULIZI (SYRIA)

Ilikuwa ni 2007 september shambulizi lingine la Israel kushambulia kinu cha nyuklia ni pale Syria(Operation Outside the Box) waliposhambulia kinu cha nyuklia cha Al Kibar, ndege aina ya F-15 zikiwa escorted na F-16 ziliondoka toka Ramat David Airbase, Israel wanasema walizifanya radar za Syria kuona kengeza na tatu tatu kwa kuzilisha false signals.

Nielezee kwa ufupi sana kwa maana hadi operation ya kuteketeza kinu hiko pale Syria ni story ndefu sana hapo hatujaongelea intelejensia ilivyohusika mpaka Israel kufahamu kulikuwa na kinu hicho pale Syria.

Usiku wa saa 4 na nusu ndege vita zinaruka toka Israel zikiwa zimebeba mabomu mawili mawili kwa ajili ya kukiteketeza kinu hicho, ndege 8 zinaingia anga la Syria zikiruka altitude ndogo sana kama 100 meters, baada ya kufika kwenye kinu cha nuclear ndege zinaachia makombora ya kutosha, baada ya shambulizi lililochukua dakika chache sana jamaa wanageuza wakitembea altitude ndogo kuelekea Turkey kisha wanakunja kona kuelekea Israel, saa 7 unusu ndege zinatua Israel.

Kinu hiki cha Syria ilikuwa ni kwa msaada wa North Korea na pia Iran ili fund pesa ndefu katika kinu hicho.

View attachment 1656874
/Kinu cha Al Kibar kabla na baada ya shambulizi/

Nirudi kwenye mada kuu.......

JE, ISRAEL ITAWEZA KUSHAMBULIA KINU CHA NUCLEAR IRAN KAMA ILIYOFANYA KWA IRAQ NA SYRIA?

1-Kwanza kabisa Iran ina semekana wana sites tofauti zenye vinu vya nuclear vilivyo underground kitu ambacho ni kigumu sana kutekeleza mashambulizi kwa kutumia ndege kama F-16 na F-15 kama Israel ilivyofanya Iraq na Syria.

Inasemekana vinu hivyo vimeongezewa zege au niseme layer fulani yenye kuzuia mashambulizi ya mabomu ukiachilia mbali ni deep underground.

Vinu vya nuclear vya Iraq na Syria vilikuwa vimejengwa kama Cube fulani, ilikuwa rahisi kwa satellite za US ku monitor kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwa maana yalikuwa ni majengo ya kawaida.

Kuna kinu kimoja Iran kipo chini ya mlima, kitu ambacho inakuwa ni vigumu sana kwa Israel au US kushambulia kwa sababu hata bomu zito zaidi la marekani lenye uzito wa tons 16 bado halitaweza kuharibu vinu hivyo vya nuclear wakati jumla ya uzito wa mabomu yaliyotumika kupiga kinu cha Al-kibar pale Syria ni 17 tons.

2-Iran ipo mbali zaidi ya Syria au Iraq toka Israel, sasa tujiulize kama F-16 na F-15 zinaweza kubeba makombora yenye uwezo wa kupiga vinu vya nuclear vilivyopo chini ya ardhi kwa kuyabeba umbali toka Israel mpaka Iran? hii inamaanisha mabomu ya maangamizi yawe na filling weight kubwa kuliko yale waliyotumia Syria na Iraq, katika mashambulizi ya Iraq na Syria ndege za Israel zilikuwa zikibeba external tanks, katika operation ya kwanza ndege ziliachia tanks kwenye jangwa la Saudi hata mission ya pili ndege ziliachia tanks Turkey wakati wanarudi hii ni kupunguza uzito,sasa F-16 na F-15 zitabeba tanks kubwa kiasi gani zenye fuel ya kutosha kuzifikisha Iran na kurudi?

Katika operation zote mbili Israel walizofanya kuangamiza vinu vya nuclear ndege vita zilikuwa zikipita chini kabisa ku avoid radar detection, ndege kama F-16 au F-15 inaporuka mfano altitude ndogo niseme 100 meters itakula fuel zaidi ili kuipa thrust kubwa ikimbie mbele, mfano katika ile operation Opera kule Iraq baada ya shambulizi ndege ziliruka juu zaidi kuzuia ulaji wa mafuta ili warudi nyumbani.

3-Ulinzi wa anga wa jeshi la Iran ni tishio, pia Saudia hatokubali kuruhusu kupitisha ndege za Israel kwenda kushambulia Iran kama operation Opera kwani lazima atalipa kwa alichokifanya pindi akibainika, je? Saudia yupo tayari kuruhusu hilo?, Pia kabla ya ndege za Israel kufika Iran lazima Iran watakuwa notified hii itawapa muda wa kujiandaa kukabiliana na mashambulizi.

Hii ni kutokana na maendeleo ya teknolojia kwenye ulinzi wa anga, S-400 zipo Middle East kwa sasa kitu ambacho ni tishio, msione marekani anakataa S-400 kuwapo Turkey wanajua walifanyalo.

4-Iran italipiza kisasi, Iran lazima italipa kisasi kwa Israel na yeyote atakayeshiriki kumshambulia, sio Saudi au nchi yeyote middle East itakayoshriki katika hilo, pindi ikibainika lazima wataingia kwenye matatizo makubwa kwani Iran ilishasema shambulio moja kwake litapelekea Middle East yote iwake moto kingine ni vikundi vitiifu vya Iran vilivyopo Yemen,Palestine, Lebanon(Hezbollah),Syria n.k lazima Israel italipa kwa walichokifanya, kitu ambacho Israel atakuwa matatani.

5-Sema watumie cruise missile zitakazo ruka chini kukwepa radar right? bado haitowezekana kutokana na vinu hivi kuwa chini ya ardhi.
Kuna makombora yanaitwa Bunker Buster yana uwezo wa ku penetrate kwenda ardhini then yanalipuka chini kwa chini, lakini lazima ndege iruke kwenda usawa wa target na kuachia mokombora, vinu vya nuclear vya Iran licha ya kuwa deep underground vimezungukwa na mifumo ya ulinzi wa anga ikiwemo mamia ya AAA(Anti-Aircraft Artillery) lazima ukutane na mvua za makombora kabla hata hujaachia makombora, na pia idadi ya vinu vya nuclear kumbuka sio kinu kimoja idadi kamili haijulikani.

Pia lazima kutatokea mvutano mkubwa kimahusiano kwenye umoja wa mataifa mfano mzuri ni operation Opera, kulitokea mvutano mkubwa na Israel kuwa matatani.

HITIMISHO
Ukweli ni mchungu, lakini sina budi kuusema, Kwa sababu tukiongea ukweli utasikia wanasema umelalia upande mmoja, Sasa sikia usichopenda kusikia.

Niseme tu kwamba tusitegemee aina yeyote la shambulizi la Israel katika kinu chochote cha nuclear cha Iran, Israel imekuwa ikisema haiko tayari kuona Iran ikirutubisha nuclear lakini tusitegemee kuona operation yeyote ya Israel kwenda Iran.

Kwa hilo Israel imekuwa ikifanya namna nyingine kwa kuwawinda wanasayansi wa Iran na kuwamaliza pia kutumia computer virus huku Israel ikiendelea kusema. Haipo tayari kuona Iran inamiliki silaha za nuclear huku Iran ikijua kumiliki silaha za maangamizi ni muhimu kwao kwa ajili ya kujilinda.

Sote tunajua Iran ina makombora advanced mashariki ya kati yenye uwezo wa kufika USA, sasa Israel haitokuwa tayari kuona missiles nzito zikitalii kwenye anga la Tel Aviv, tuseme watumiane makombora ya masafa marefu bado Israel itaumia, Iran ina 1.7 million km square wakati Israel wana 21000 km square, hapo unazungumzia Iran yenye population ya watu mara 10 ya israel na Iran ina mikoa 10 dhidi ya Israel yenye miji miwili(2).

Ili Israel amfanye Iran ku-surrender lazima akaange base zake zote katika miji yote iliyo umbali wa maelfu ya kilomita huku Israel ikiwa miji yake ina umbali usiozidi kilomita 200.

Uwezo wa Iran kuhimili vita vya muda mrefu ni mkubwa kuliko wa Israel, Iran ilishapigana vita kati yake na Iraq kwa miaka 8 kama nilivyosema hapo awali huku Iraq ikipata misaada ya kila aina ikiwemo silaha za sumu ambazo tayari zilishapigwa marufuku kutoka nchi za magharibi na USSR, vita pekee iliochukua muda mrefu kwa Israel ni ile kati yake na Hezbollah ambayo ilichukua mwezi mmoja tu ambapo hata mwisho wake israel hakushinda.

Iran ni moja kati ya nchi zenye mafuta ya kutosha na gesi duniani, pindi vita itakapotokea hawatotegemea nchi nyingine yeyote kama itakavyokuwa kwa Israel.

Niseme Israel haiwezi kusimama dhidi ya Iran kama US haitoingilia kati hivyo ni sababu pia ya Israel kutofanya mashambulizi ya moja kwa moja kwa Iran.

Kwa hio ndugu zangu msitegemee Israel kuichokoza Iran kwa kushambulia moja kwa moja vinu vyake kama ilivyo fanya kwa Syria na Iraq, ndio maana mnaona Israel inafanya kuwanyatia wana sayansi wa Iran na kuwamaliza kitu ambacho Iran kwao wanasema wamekufa kama Shaheed, hii kitu ni moja ya vitu vinawapa Iran morali ya kivita.

Israel kufanya mashambulizi kwa wanasayansi haitosimamisha juhudi za Iran kumiliki silaha za nyuklia bali kwao mwanasayansi kama akiuawa anaonekana shujaa aliyeuawa akipigania nchi yake na dini yake (Shaheed) hivyo bado kuna mamia ya scientists wapo tayari kukalia nafasi hizo.
Sasa sioni kengeza
 
Kisasi cha wairani sijui lini kitaisha
Hii leo
#Iraq
Breaking: IED attack on two #US convoys south of Iraq

A U.S. military convoy was attacked by a roadside bomb on the Al-Diwaniyah International Road and another convoy in the al-Samawah area by the Iraqi resistance groups in south of Iraq.

 
Kisasi cha wairani sijui lini kitaisha
Hii leo
#Iraq
Breaking: IED attack on two #US convoys south of Iraq

A U.S. military convoy was attacked by a roadside bomb on the Al-Diwaniyah International Road and another convoy in the al-Samawah area by the Iraqi resistance groups in south of Iraq.

Biden atakapoingia kwenye uongozi itafahamika, Lakini kitendo cha Iran kusema kwamba wanaongeza urutubishaji wa uranium baada ya kifo cha Fakhrizadeh ni pigo tosha tayari kwa Israel na USA.
 
Back
Top Bottom