100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 3,326
- 11,087
- Thread starter
- #161
Upo sawa mkuu, viongozi hawapendi vita , USA na Israel ndio tatizo hilo lipo wazi, mkuu hata leo hii huku Africa ukiwa na mali tu ni shida, taifa lolote duniani likiwa na mali na uende against na USA wewe ni threat kwao...naamini Iran angewekeza kwenye teknolojia za kiraia na sio kijeshi wangekuwa mbali sana leo hii.
..hawa jamaa wamebarikiwa vipaji na uwezo ktk sayansi lakini wanaangushwa na viongozi na watawala wao wanaopenda vita.
..Iran wangeweza kuwekeza ktk kuunda magari na mitambo kama South Korea na mitambo hiyo ingekuwa inatumika dunia nzima.
..Wangeweza pia kuwekeza ktk kutengeneza madawa kama walivyofanya India ambao leo hii inasemekana wanatengeneza 60% ya chanjo za covid-19.
..Nafasi ambayo India na South Korea wapo naamini ktk sayansi na teknolojia Iran wangeweza kuifikia kama wangekuwa na viongozi wenye maono.
..Samahani kwa kuwatoa nje ya mada yenu.
Kifaru anaponzwa na pembe zake, tazama China wamekuja na 5G, waliitest Japan tatadocomo ilikuwa inakwenda 1Gb/sec latency yake ilikuwa nzuri mno, lakini tazama USA alichokifanya.Kapiga vita.
TikTok ilianza kuleta ushawishi na kupendwa sana tazama USA alichofanya mpaka wameinunua, wanataka instagram,facebook, whatsapp,youtube n.k vya kwao ndio viwe juu siku zote.
Wanaipiga Russia vita kuuza gas ulaya.
Tatizo la wenzetu ni wabinafsi sana asee.
Libya kuwa na mafuta tu ilikuwa threat kwao,wakaja wakampiga mzee Gaddafi wakamzalilisha sana na kumuua.
Nchi imenuka na wao wamekimbia.
Iran inachofanya ni sawa, bora kuwa mbishi tu.