Je, Iran inaweza kugeuza Aircraft Carrier za USA kuwa Shipwreck?

Upi naomba utaje mfano hatuelewani mkuu

..tangu miaka ya 1980 Iran iko kwenye vikwazo vya uchumi.

..kwa maoni yangu Iran inahitaji uongozi utakaowatoa kwenye vikwazo.

..Iran haihitaji uongozi unawalazimisha kuishi ktk vikwazo vya uchumi.
 
Duuh sawa mkuu tupo tofauti sana sasa iran kuwekewa vikwazo we unaona ni haki? Uongoz unawalazimisha waishi kwenye vikwazo sasa wewe ulitaka marekan abebe ile reserve ya oil&gas etc pale middle east ili iran asipewe vikwazo maana sielew hoja zako hapo
 
..nadhani mafuta ndio yanayowatia wendawazimu viongozi wa Iran.

..mimi naamini Iran wanaweza kufaidi mafuta yao, bila kukwaruzana na Wamarekani, na kusababisha vikwazo vya uchumi.

..sijui kama unaikumbuka vita ya Iran vs Iraq, pale ndio ungejua kwamba nchi zote mbili zilikuwa na viongozi vichwa maji wasiojali maisha ya wananchi wao.
 
Mkuu samahani lakini bado hujaielewa dunia vyema vita ni biashara na maslahi aliyekuambia hiyo vita walipigana hawa madogo kwa maslahi yao binafsi pole yako na iran njia pekee anayoweza kusurvive na kufaidi rasilimali zake ni kwa mwendo huu huu anaoutumia mkuu
 
Uzi mzuri sana kuna tech ya gharama na kuna tech ya kawaida ila makini sana.
Dunia ya sasa hakuna mwenye hatimiliki ya teknolojia kila nchi kubwa imewekeza kwenye teknolojia na kwa usiri mkubwa. USA alikua anajiaminisha anaweza fanya chochote duaniani na hakuna wa kumuuliza ila sasa anapiga hesabu mara 100 ,100 kabla ya kufanya jambo.

Great world lazima tuheshimiane
 
Kwahio unataka kutuaminisha kwamba HIZBULLA wana nguvu kuliko majeshi ya Kiarabu?

Hawa wanajificha nyuma ya migongo ya raia "human shields" ao inakuwa ngumu kushambuliwa maana wakishambuliwa ulimwengu unaishutumu Israel kuua raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Israel kila siku wanasumbuliwa na lical made missile toka Palestinian....... Israel wanatumia gharama kubwa kupambana na palestina ambayo haina hata msaada wa silaha achana na bajeti ya ulinzi ya kueleweka
 
Umejibu swali? Kwaio Khamas ameshawahi kuishinda Israel? Au nchi gani pale middle east?
 
Hapa kuna ngoswe kama tatu hivi
Meli mbovu ile ilizama au unakuta iliharibika unakuta ipo beach au chini kabisa ya maji huwa zinajulikana kama shipwreck.

SS-Thistlegorm-Egypt-SHIPS0816-2000.jpg

640px-Titanic_wreck_bow.jpg

Kuna jambo nililiona hapo tarehe 15 hii january ambalo si la kawaida, katika kipindi hiki ambapo Iran na USA wamekuwa na mvutano mkali hasa baada ya kuuawa kwa Fakhrizadeh mwanasayansi wa atomiki wa Iran na Iran kuwanyooshea Israel kidole kusema wanahusika na kusema wanalipiza kisasi ndipo USA akawa makini na hakuwa na masihara.

USA wanafahamu vyema waajemi watalipa kisasi ni baada ya Iran kulipua zile kambi za kule Iraq Al Asad na Erbil na kusababisha askari 110 kupata traumatic brain injury kama kisasi kwa general Soleiman baada ya USA kumshambulia kwa drone.
Kwanza USA walituma carrier yao kubwa kabisa na B-52s, hio ni kuwaonyesha Iran kwamba wasithubutu hata kujikuna.

800px-USS_Nimitz_%28CVN-68%29.jpg

Long story short USA alikuwa anawaonyesha waajemi watapata kipigo cha mbwa koko, sote tunaijua USA vyema linapokuja suala zima la mashine za kivita hawa jamaa hawana mpinzani, lakini kuwa na mashine za kivita zenye teknolojia advanced kabisa ndio kushinda vita? hapana, ukitaka kujua ukweli jiulize B-52s takribani 19 kwenye ile vita kati ya vietnam na USA ziliwezaje kupigwa?

Niseme kitu kimoja, linapokuja suala zima la vita ile ya kweli, acha mazoezi, hizo silaha zinaweza kuwa hazina umuhimu sio S-400 wala Patriot,B-52s au Nimitz, linapokuja suala zima la vita ile vita kabisa hizo mashine ubora wake utabaki maabara tu, kweli nakuambia.
Majaribio ya hizi silaha kimaabara ni tofauti na zinapokwenda kwenye vita, haya majaribio yanapelekea kuuzwa silaha ambazo uwezo wake ni wa kimaabara zaidi na katika hali fulani, hivyo ndivyo Russia na USA wanavyokula pesa kiulaini.

USA na mwenzake Russia wanaziwekea kitu kinaitwa kill switch, just in case silaha kama hio imeangukia kwenye mikono si salama wanaweza wakazima hio silaha we ukabaki na toy tu, au just in case kuna jambo lina maslahi kwao wanazima tu (chwiip), unabaki na toy lako hapo ukidhani una silaha.

Kuna kisa kimoja kilitokea, Israel walikwenda kushambulia kinu cha nuclear pale Syria pasipo hata S-300 kufanya chochote wala radar hazikuona chochote huku Israel wakisema walizilisha radar hizo false signal, je ni kweli? hapana. Kuna kipindi Iran ilidai Russia ameuza codes za air defenses aina ya s-300 zilizopo Syria kwa Israel, ilikuwa ni 2017 nadhani Iran walitoa madai hayo, ndege za Israel zilikuwa zinaruka tu kwenda kufanya mashambulizi Syria na kupiga sites za Iran pasipo system hizo kufanya lolote au kutoa onyo kama kuna ndege zinakuja.

Inasemekeana hio operation ya mwaka 2007 ya kulipua kinu cha nuclear, tayari warusi walikuwa wamewauza Syria na mwenzake Iran, F-16s sio stealth, but how comes walifanya mashambulizi pasipop hata radar kutoa warning?

Kutokana na ukaribu uliopo kati ya Syria na Israel, defenses za Iran au hizo za Syria zilipaswa kutambua kama ndege zimeruka toka Israel kwenda kufanya mashambulizi.

Iran walibaki wametahamaki, bila ya Moscow kujua ikabidi Iran watume engineers waende Syria kubadili codes za defense system hizo ambazo zilikuwa chini ya jeshi la Syria, jamaa walifanikiwa kubadili codes na system zikawa active, inasemekana baada ya zoezi hilo systems hizo ziliweza kutambua ndege zilizoruka toka Israel na zikaweza kurusha missiles ku intercept mashambulizi ya ndege hizo.
Iran wanasema systems hizo kabla ya marekebisho ziliweza kutambua ndege hizo za Israel kama friendly planes na sio ndege za maadui kitu ambacho kinaweka wazi Israel walikuwa wanajua secret codes hizo.

Hizi S-300 na S-400 ni threat kwa Israel, jirani ambae ni adui kama Syria anapomiliki systems kama hizo, ujue hizi system zinaweza kugundua ndege inapotokea(inapo take off), kwa ukaribu uliopo kati ya Israel na Syria hizi system zinaweza kutoa taarifa pale tu ndege ya Israel imeruka, hata ikiwa kwenye anga lao, hiko kinapelekea kumpa adui target wapi akupige.

Katika kisa kimoja baada ya ndege kuruka ya Israel kwenda kufanya mashambulizi Syria, S-300 zikatoa taarifa kuna ndege zinaruka na Hezbollah wakarusha roketi la thamani ya $2000 pale pale ndege hio ilipotokea na missile ya Israel yenye thamani ya $3m ikaweza ku intercept kombora hilo, mambo mengine yanachekesha kweli kweli.

Wakati mwingine kuwa na silaha advanced na za gharama inaweza kula kwako, na hapo ndipo Hezbollah huwa wanaijambisha Israel. Wao wanaweza kutuma missiles za gharama ya chini kabisa, Israel waka intercept kwa advanced weapons, beleive it or not, Israel unaweza kuisifu ina advanced weapons na za gharama lakini Hezbollah wakaimudu Israel, katika vita ambayo Israel walipigana kwa muda mrefu ni ile ya 2006 dhidi ya Hezbollah na ilikuwa mwezi mmoja tu, vipi ingefika mwaka? Kwani huo mwezi mmoja myahudi ulimi ulimi ulikuwa umemtoka nje kama amekimbia km 1000, choka mbaya.

Unarushiwa kombora la milioni 4, na wewe una li intercept kwa kombora la thamani zaidi ya bilioni 6, je unaweza kumudu vita kwa muda gani? kama kombora la milioni 4 unalizuia kwa bilioni 6.how much money you got?

Missile ya Iron dome ni $40,000(Milioni zaidi ya 90), sio mchezo, Thats why Israel haiwezi kumudu vita vya muda mrefu, wao wakija kukupiga ni wiki tu.

Unaambiwa Hezbollah wana missiles kama 150,000 , anti-tank missiles, anti-ship missiles na ni wataalamu kweli kweli kuzitumia, Hezbollah na wao hizo missiles kujua wanaziweka wapi ni sawa na mtu kukuambia kanitafutie chozi la simba.

Mossad ya Israel kwa jinsi walivyo na intelejensia ya hali ya juu, walitafuta hizo kombora zilipo kwa muda wa miaka 6, na siku walipokwenda kupiga kwenye ile vita ya 2006, kumbe hamna kitu, Hezbollah wamekwisha hamisha zamani, can you imagine?

Niendelee........(2007/2008)

Ni kweli Russia waliwapa Israel codes kwa maslahi yao, ilikuwa hivi...
Kuna kampuni binafsi Mexico linaitwa HYDRA, hii kampuni inaitwa HYDRA wanahusika na kutengeneza drones zenye teknolojia ya hali ya juu , serikali ya Mexico iliwekeza pesa za kutosha kwenye hii kampuni, inasemekana hizi drone za Mexico ni bora zaidi kuliko za Israel katika majaribio ambayo yalifanywa.

Georgia walikuwa wanatumia drones ambazo zinatengenezwa na Israel katika kipindi chote hiki.

Hawa HYDRA walipata order ya kuwauzia hizi drones Georgia, kilichofanya Georgia wahitaji hizi drone kutoka HYDRA ni kwa sababu Georgia waligundua drones zao zilikuwa hacked na Russians, na hizi drones za HYDRA unapojaribu kuzihack huwa zina back up system haraka na papo hapo zinarudi kwenda kwenye base.

Georgia waliwapatia picha HYDRA picha ya moja ya drone yao ambayo ilikuwa imeanguka, lakini kwa picha ile inaonekana ile drone iliteremshwa kwa lazima ardhini na haikushambuliwa, kwa sababu ingeshambuliwa basi wangeona vipisi tu.
Na haikutokea mara moja, baada ya Georgia kugundua mchezo ikabidi wajaribu kuziuza drones za Israel hizo kwa Azerbaijan(haijulikani kama deal ilifanikiwa),

HYDRA walikataa kufanya biashara na Georgia kwa sababu ingeleta mvutano mkubwa sana kati ya Mexico na Russia, inasemekana Venezuela walikuwa wa kwanza kutaka kununua drone hizo lakini pia HYDRA walisita kutokana na mambo ya kisiasa.
Hivyo Israel waliwapatia Russians data link ili wahack drones za Georgia na Russia wakawapatia Israel codes za namna ya kuhack defense system ikiwamo Tor M1 na S-300 za Syria.

Unakumbuka kile kisa cha Iran kuiteremsha ile ndege stealth ya USA(RQ-170 Sentinel)? ina maana Iran walikuwa na data link ya ile ndege, sasa walipataje? mi sijui, ndio haya ninayosema silaha nyingine zitabaki kuwa na ubora maabara tu.

Kuna systems S-300 Russia waliziuza Greece, sasa siwezi jua ilikuwaje Turkey walipata taarifa nyeti kuhusu hii mifumo na wakaweza kushirikiana na Israel namna ya ku crack hii mifumo, kwa sababu ilileta mvutano sana baada ya Turkey kuona Greece wana s-300 miaka ya 90 mwishoni, na sasa Turkey ana nunua S-400, wakifanikiwa kuzi crack S-400 lazima tu Turkey watashare taarifa na Israel just in case kuna maslahi yakitokea, na Israel na USA ni allies.

Ukitaka kuamini ninachosema tafakari kwa nini Iran anatengeneza air defense systems zake binafsi, kwa nini wanatengeneza drones zao binafsi? ask your self, wanaujua mchezo uliopo. Na hapo hapo Russia na wao huwezi kujua kwa nini wamemuuzia Turkey hizo S-400,Linapokuja suala zima la ulaji kila mtu anapita kivyake.

USA baada ya kuona Turkey wamepata S-400 na yeye amekataa kuwauzia F-35 Turkey, S-400 inaweza kupata intelligence kuhusiana na stealth ya F-35 kwa madai ya Uncle Sam, lakini tujiulize.

Mboma Greece ilikuwa na S-300 na hatukusikia haya madai? basi tuseme S-300 haiwezi kusoma stealth, lakini vipi S-400 zilizopo Syria? s-400 ina range ya km 400, S-400 ikiwa Syria inaweza kusoma radar signature za F-35 zilizoko Israel, ipo wazi, yaani Russia wakajua F-35 stealth inaonekana vipi kwenye radar ya S-400, kumbuka stealth aircraft inapunguza tu uwezo wa kuonekana kwenye radar lakini hata radar ya mwaka 1945 inaweza kugundua stealth aircraft.

Hata Turkey akiwa na F-35 bado zitaonekana Iran, Azerbaijan, Georgia n.k. Lakini bado USA ana wapa vikwazo Turkey vya uchumi, why?

USA hawataki kuona yeyote akinunua silaha za Russia, na yeye anataka ndio awe on top kwenye soko kuliko mwingine yeyote, biashara ya silaha ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa USA, USA asipo piga mikwara kuhusu nchi nyingine kununua silaha za Russia basi wengine wote watafuata na kuanza kununua silaha za Russia.

Unaweza pia kujiuliza kwa nini USA hataki nchi za Ulaya kutumia gas ya Russia? au gas ya Russia itasoma stealth technology ya F-35?
Na ukija kwenye suala zima la gas hapo umemshika Putin goroli, Russia ipo kumlinda Assad kwa sababu ya gas yake iuzwe ulaya, na kweli amefanikiwa kumkalisha uncle Sam. Putin yule sio mtu kabisa, achana na yule mtu, niliona video moja mwandishi wa habari russia anamuuliza Putin, "hivi wewe ni alien"?.

eh9UEPFVzC3Gy0khAtmjAShcMFG7nb1x1.jpg

Putin anaendesha formular one racing cars, Putin anendesha submarine, Putin anajua kutumia silaha, Putin anaendesha farasi yupo kifua wazi , Putin anaendesha ndege, ni former KGB spy,Putin anajua kuzichapa, Putin ni James Bond katika uhalisia, James Bond yeye ni character kwenye fiction movie, sasa huyu jamaa ni James Bond wa uhalisia.

Putin ndio mtu tajiri zaidi duniani utajiri wake ina sadikika ni $200bn. Putin ndio karejesha heshima ya Russia baada ya uongozi wa rushwa na hovyo chini ya Yeltsin.

Putin ndio aina ya mtu ambae kipindi yupo shuleni walimu ndio walikuwa wakinyoosha mikono kumuuliza maswali na kipindi Alexander Ghanan Bell amevumbua simu basi alikuta missed call 3 za Putin, Putin ndiye alidondosha wallet bahati mbaya pale Switzerland mpaka leo hii inaitwa Swiss Bank.

Ni utani tu jamani tusielewane vibaya. Lakini kiukweli Putin anatisha, kama wazungu wenzie wanamuuliza "are u alien"? unafikiri ni kawaida.

Vladimir Putin alienda akaimega Crimea hapo 2014 kibabe wakati NATO wakipiga kelele wakiongozwa na USA, Vladimir Putin ndio aliingia pale Syria akatawanya wale magaidi ambapo Uncle Sam na wenzake walikuwa waki support, Vladimir Putin ndie alimtuliza Uncle Sam pale Venezuela akatulia.

Uncle Sam huwa tunatumia jina hili kumaanisha United Sates sasa unajua inakuwaje United States ilikuja kuitwa Uncle Sam? Ilikuwa hivi, kuna jamaa alikuwa akijulikana kwa jina la Samuel Wilson, huyu alikuwa mfanya biashara maarufu sana karne ya 19, kwenye ile vita ya mwaka 1812 ambapo USA walikuwa kwenye vita na United Kingdom of Great Britain na Ireland, usichanganye Great Britain ni kisiwa kikubwa ambapo kuna Scotland,Wales na England, Great Britain sio nchi tuelewane ni jina la kisiwa, unaposema United Kingdom unamaanisha Northern Ireland, England, Wales na Scotland.

Southern Ireland wapo peke yao, ukisema British Isle unamaanisha sovereign states mbili ambazo ni United Kingdom ya Great Britain na Northern Ireland na nchi nyingine ni Southern Ireland.

Samuel Wilson ndiye alikuwa akipeleka chakula kwa majeshi ya USA, Ilikuwa ni nyama ya ng'ombe(beef), sasa huyu jamaa alikuwa akijulikana pia kwa jina la Uncle Sam(Uncle Samuel), sasa kwenye yale mapipa yaliyokuwa yanabeba chakula yalikuwa na stamp imeandikwa US, US ikisimama kama United State as government property na pia US ni kifupi cha Uncle Sam, ndipo hapo United States ikawa inajulikana kwa nick name ya Uncle Sam.

Lakini naomba kidogo nikuelezee kwa nini Russia amemsaidia Assad, naomba nielezee kidoogooo.
Ipo hivi.

Kuna sababu nyingi zilizopelekea Russia kumsaidia Assad aendelee kukaa madarakani na kwa kweli amefanikisha hilo. Russia wana mfungamano na Syria kwa karibu zaidi ya miaka 50 sasa, Hafez Assad baba wa huyu Bashar Al Assad alichukulia mafunzo ya kurusha ndege vita toka kwa wasovieti na baada ya kuwa raisi wa Syria, Russia ndio walikuwa wauzaji wakubwa wa silaha nchini Syria.

EU hawana ujanja kwa gas ya Russia, waende mbele warudi nyuma gas ya mrusi ni muhimu kwao, sasa linakuja suala zima la maslahi ya kiuchumi, Russia anataka EU waendelee kutegemea gas yake na pia Russia anataka silaha zake aendelee kuziuza na nchi kama Syria ni wateja wao wakuu kama nilivyosema, hapo awali Hafez(Baba yake Assad) alikuwa na urafiki sana na Russia mpaka kuwaruhusu Russia kujenga base yao ya kijeshi Tartus mwaka 1971 walikuwa maswahiba kweli kweli.

Qatar wana gas reserve kubwa sana ni ya tatu kuwa na reserve kubwa duniani, ya kwanza ikiwa Russia ikifuatiwa na Iran.
Russia yupo kifua mbele kwa umuhimu wa gas yake Ulaya na hapo Ulaya kwa pamoja wakimuona Russia wanasimama kwa ukakamavu na kusema shikamoo Russia, Russia anaitikia marhaba hamjambo? hatujambo, basi kaeni chini,woootee wanakaa chini kwa utulivu.

Kwa hilo USA hataki kuona Russia anakuwa na ushawishi na kujenga uchumi wake kupitia Ulaya, USA anataka yeye ndio awe supplier mkubwa wa gesi Ulaya.

Unaweza ukashangaa lakini ndio ukweli huo, Russia inaogopeka, USA anaona ni bora hata yeye akose kuuza gas Ulaya auze mwingine lakini sio Russia. akishirikiana na Qatar.

Lakini uchukuzi wa gas toka USA mpaka Ulaya ni ghali, Russia na Ulaya ni majirani, hata USA ikijenga bomba la mafuta toka USA mpaka ulaya ni gharama sana na watapata hasara tu.

Germany ndio mteja mkubwa wa gas ya Russia kwa ulaya na hapo 2019 USA walitangaza vikwazo vikali kwa kampuni za ulaya zinazohusika na ujenzi wa pipeline iitwayo Nord Stream 2 zinazoshirikiana na kampunbi ya Russia iitwayo Gazprom, katika ujenzi wa Nord stream 2 Germany ndiye alikuwa akishirikiana na Russia kwenye ujenzi huo wa pipeline ya gas yenye distance kubwa zaidi duniani kwa zaidi ya kilomita 1200, Nord stream 1 ilishajengwa na hii nord strem 2 ilianza ujenzi hapo 2011.

2019 ubalozi wa USA nchini Germany ulituma barua kwenda kwa makampuni yanayojihusisha na ujenzi wa bomba hilo la gesi kusimamisha ujenzi haraka kabla ya kukutana na vikwazo vikali.

43318158_7.png

Mabomba ya Nord Stream 1 na 2

20170410_CIA1_0.jpg

pendekezo la ramani ya Mabomba toka middle east Qatar na Iran kwenda ulaya

Tunaona jinsi USA ambavyo anapiga vita biashara ya gas kati ya Russia na nchi za Ulaya, USA na Qatar walitaka kutengeneza bomba la gas, kumbuka nimekueleza Qatar ni moja ya nchi yenye gas reserve kubwa duniani, USA alitaka Qatar awachallenge Russia kwa uuzaji wa gas pale Ulaya.

Lilitokea pendekezo la kujenga bomba la gas kutoka Qatar kwenda Ulaya kupitia Saudia then liingie Syria na kuikamata Turkey moja kwa moja mpaka Europe, USA walitoa baraka zao zote juu ya ujenzi huo wa bomba, lakini lazima bomba lipite Syria, kumbuka nilisema kwamba Syria ni mshirika mkubwa wa Russia kistratejia tangu enzi za baba yake Assad,na Assad hataki kuwaharibia swahiba zake warusi kwa sababu Russia anatengeneza uchumi wake kupitia gesi anayouza Ulaya, pindi gas ya Qatar ikiingia Ulaya ita challenge warusi na kuwaharibia uchumi wao.

Syria ikakataa katu kumuuza swahiba wake Russia kwa kupitisha bomba hilo kwenda Turkey kuingia ulaya, hapo Turkey kakosa ulaji kama simba aliyekosa swala mnono nakubaki kujilamba tu, sasa Turkey pia hawapendi uwepo wa Assad.

Qatar imefund vikundi vya kigaidi kupambana na uongozi wa Assad kwa kutoa dola bilion 3, Saudia Arabia pia amekuwa aki fund makundi ya kigaidi kushambulia Syria lengo likiwa kumtoa Assad, Turkey nae ali support anti-Assad groups.

Ukija kwa Turkey na yeye anategemea gesi ya Russia, kwa uongozi wa Assad kuanguka na ujenzi wa bomba la gas toka Qatar kupitia Turkey utamfanya awe huru dhidi ya utegemezi wa gas ya Russia. Pia kwa bomba la gas kupitia kwao lazima wangekuwa wanalipwa transfer fee.

Lakini hapo hapo tena kuna pendekezo la Iran pia kutengeneza bomba la gas, kumbuka nilisema kwamba ikitoka Russia kwa reserve kubwa ya gas inafuata Iran na kuingia kufuatiwa na Qatar, sasa Iran nao walitaka kufikisha gas yao kufika ulaya kupitia Iraq na Syria, Russia na Assad wakatoa baraka zao zote kwa Iran kupitisha bomba lao la gas Ulaya.

Iran ana matumaini kabisa siku moja anaweza kuwa mfanya biashara mkubwa wa gas pale Ulaya tokana na waliacha kuendeleza ICBMS, kwani kwa jinsi walivyo karibu na Ulaya, nchi za Ulaya zingeona ni threat kwao, lakini ICBM ya kufika USA wanayo. Shahab-6.

Kuna video moja niliiona wapiganaji wa Hezbollah walikutana na wapiganaji wa ISIS kule Syria, mpiganaji wa Hezbollah mmoja akaona haina haja ya kuanza vita ikabidi aanze maongezi nao wale wagaidi wa ISIS.
Mongezi yao kwa ufupi yalikuwa hivi...........video ipo hapo...

Hezbollah Soldier: Kuna mtu anakuja kuongea nanyi, kwa nini bado mmeshikilia silaha zenu? naona kama mnaogopa.

Hezbollah soldier: Hivi mmeona hali ya Al Zabadaan jana? Jinsi ilivyokuwa na jinsi ilivyo sasa, Al Zabadaan ilikuwaje miaka mitatu iliyopita na iko vipi sasa?

Hezbollah soldier: Nataka niwaambie kitu kimoja, msiwaamini viongozi wenu, Mnashuhudia nini kinatokea Zabadaani, sasa mpo hapa hamuogopi mnapigana lakini wako wapi
viongozi wenu au makamanda wenu?

Hezbollah soldier: Jina lako nani?

ISIS : Jina langu ni Abdullah.

Hezbollah soldier: Hata mimi jina langu ni Abdullah, sikiliza rafiki yangu nataka nikueleze ukweli, watu wanaolipa gharama ya vita ni wale walioko kwenye vita unafahamu hilo? Umesoma Quran? umesoma kitabu kitakatifu?

Wadhalimu ni Israel na America na sio ninyi wala waislamu wengine, tukubaliane kwa sasa sisi ni maadui lakini wapaswa kujua kwamba unanufaisha mpango wa hatari ambao hautakuwa na maslahi kwako, Mnawanufaisha Israel na wenzake, angalau naweza kuongea nanyi lakini makamanda wenu hawawezi kunisikiliza, hao ni wezi, mbwa,woote ni wafanya biashara wanaotumia wengine na watu wasiokuwa na makosa kulipa gharama ya vita.

Viongozi wenu hawapo kwenye hii vita,wapo busy sana wakitumia muda wao kula maisha huko America, Viongozi wenu wa Saudi, Qatar wapo busy wakicheza muziki huko America, tazameni wenyewe kwenye mitandao hakuna kinachojificha, Tazameni Gulf States wanachokifanya kwenye nchi zao.

Nafahamu viongozi wenu wamewalisha chuki dhidi ya Iran, wakiwaambieni Iran ni adui yenu, lakini Iran ana adui mmoja tu na huyo ni Israel.

ISIS : Vipi kuhusu Assad na uhalifu aliofanya?

Hezbollah Soldier: Upo sahihi na una haki ya kusimama lakini unapaswa kuelewa kwamba katika hiki kipindi haupiganii katika kile unachokiamini, Unapigania wale wanaosambaza chuki na kunufaika na hii vita, sipigani kwa ajili ya kumtetea au kumpinga Assad kwa sababu mimi sio Syrian, labda kama kuna mtu nyuma yake aliwaumizeni lakini binafsi hajaumiza yeyote.

Rushwa zipo kwenye kila serikali, hili linajulikana, hata serikali yetu na hata kwenye misikiti kuna watu ni wala rushwa, kuna mpango mkubwa wa kumuondoa Assad kwa sababu ya kuwa kinyume na Israel, USA na rafiki zake, watawatumieni ninyi, na maelfu kama ninyi kumuondoa Assad madarakani, nawaambieni kuna rushwa Syria, Lebanon na kwenye kila serikali. Tunamuomba tu mungu atusaidie, hivi mnafahamu walichokifanya Israel Lebanon? walitengeneza Hakat Amal wapigane na Hezbollah , shia wanaua shia wenzao.
Kulikuwa na nyumba moja ya ndugu watano, mmoja ni Amal,mwingine ni Hezbollah na nakadhalika.

ISIS: Sasa hivi wametengeneza Shia dhidi ya Sunni

Hezbollah Soldier: Hawawezi kuwaambieni ukweli wote, hii vita ni ya Israel, sasa hivi wapo wanakunywa whyskey wakitutazama tunavyouana sisi kwa sisi, wana furaha sana kwa sababu hata silaha mnazotumia zinatoka Saudi na Qatar, toka sasa hivi uende ukaangalie hao Saudi na Qatar walipo.

Hayo yalikuwa maongezi mafupi kati ya magaidi(ISIS) na mpiganaji wa Hezbolllah, hao askari wapo Syria, sio wapo Syria tu bali wapo vitani,wanajua mengi kuliko wewe na mimi tupo huku Africa tena tukitumia mitandao kufahamu yanayoendelea.

Niliposema kwamba vita dhidi ya Assad ni ya maslahi kuna ambao mtaona naongopa, lakini ndio ukweli huo, mmeshuhudia hio conversation.

Maneno ya huyu askari wa Hezbollah yanaonekana kumuingia kabisa huyo jamaa wa ISIS, Kaa ujue gaidi anaweza kutengenezwa, akatumiwa na kisha akauzwa kama bidhaa, gaidi ni silaha pia kama unavyoona vifaru vya kivita, hapo ndipo ulimwengu ulipofikia, na unatumiwa pasipo hata kufahamu kama unatumiwa.

Niendelee sasa......USA hataki kabisa kuona Russia ya Putin inarudi kwenye mchezo.

USA anataka yeye ndiye silaha zake ziwe sokoni, yeye ndie awe na control ya silaha zake, wazee wa kill switch ukizingua tu wanabonyeza button.

Turkey wanataka wawe na system inayojitegemea ya ulinzi, hapo middle East kila mmoja ana maslahi yake, USA wakati mwingine wanaweza kuwa na maslahi tofauti na Turkey mfano USA anavyo wapatia baadhi ya vikundi silaha nzito middle East kwenye hii vita ya kumtoa Assad, Turkey inaweza kuwa kwenye danger, na hapo inabidi wajitegemee kivyao kwenye masuala ya kiulinzi.

Mfano mzuri ni USA anawapatia Kurds silaha, Turkey anapambana na Kurds.

Kwa nini basi USA wasiwatoe Turkey kwenye umoja wa NATO?
Turkey kwenye umoja wa NATO wao ndio wanashikilia nafasi ya pili kuwa na nguvu ya kijeshi baada ya USA, Turkey kuna base za USA(NATO) zipatazo
24.
Operation zoote kwenda middle east zinatokea kwenye hizo base za Turkey, Turkey kujitoa NATO ni loss kubwa sana kwa USA, subiri kwanza USA apate base
zingine middle east then watakua tayari kumtoa Turkey.

Niendelee na mada sasa...

Niliposema niliona kitu kilichonishangaza tarehe 15, ilikuwa ni video niliona Iran waliirusha kwenye vyombo vya habari wakimjibu USA, huu mchezo ni kama wewe si una hiki? na mimi nina hiki, wanadorishiana mashine za kivita.

Na sio mashine tu za kivita, ni mashine za kisasa kabisa, hizo B-52s za USA usifikiri ni zile za Vietnam eti zinaruka usawa wa target na kuanza kuhara mabomu, hapana, hizi za sasa zinaruka mbali na wewe ile tunasema stand off missiles zinarushwa hata 500 km away, then hizi cruise missiles kama AGM-28,AGM-69 zinaanza kukufuata kuja kukuharibia siku yako nzima.

B-52 inaweza kutanguliza missiles kutambua tu ni wapi S-400 zipo, yaani hilo missile likiwa linakuja huku linauliza S-400 uko wapi?
S-400 bila kujua inazugwa inajitokeza nipo hapa tena kwa sauti, huku S-400 ikiwa inatoa missile yake huku ikitoa mwanga kama mti christmas, tayari infrared detectors zinaona tukio zima, linatumwa sasa cruise missile la pili lenye stealth capability, basi S-400 inapigwa na kusambaa, then B-52 linakuja sasa, linakunyea hapo mpaka basi.

b-52h_static_display_arms_06_3.jpg

Hio ni B-52 na kombora zake

Niendelee na mada..... Niliona hii video youtube Iran wakifanya mazoezi ya kijeshi, kwanza hawa jamaa wametengeneza drone zenye teknolojia ya kutisha, hizi ni stealth halafu zinaweza kwenda kupiga target km 1000 umbali, na pia ni kamikaze drones, yaani ikija yenyewe ndio silaha inapiga target na kulipuka.

Hapa waajemi nawapa shikamoo, tafadhali tazama video hapo chini ili twende sawa, kuna missiles na drone utaziona then nataka nifanye uchambuzi kidogo. Video ina dakika 1 tu.

View attachment 1682085
Tazama hio warhead yenye plasma cloud ikienda kupiga target. nimeizungushia mduara mwekundu.

f48c4dbdbb58470186b5725eda7ec379.png

AZ_3447_resize.jpg

Hivi katika mvutano kama huu ambapo USA anaonyesha midude kama carriers, Iran walinishangaza, niliona wanafanya testing ya missiles.

lakini mbona missiles mbona hata hamas wanazo? wanamuonesha nani missiles? Baada ya kujiuliza hivyo ndipo nikawa makini na kugundua ujumbe mzito uliokuwa kwenye hio video, tena hii video nimeiona hii january 15 tu hapo majuzi.

Sehemu ya kwanza wanaonyesha missiles zilizobebwa kwenye magari zinavyo kwenda kupiga target, sehemu ya pili ni drones zikifanya mashambulizi.

Kwenye missiles ndipo palipo nishtua na kuona ni kweli Iran wanaweza kupiga carrier, beleive it or not, wajuzi wa mambo wameona , walio na macho wameona.

Hizo missiles zilizopigwa kwenye hio video ni advanced, kwanza kabisa ni stealth kwa mujibu wa jeshi la Iran, tuachilie mbali stealth technology haya makombora yana kitu cha ziada.

Hio video ya youtube ipeleke kuanzia sekunde ya 59, tazama kwa makini, utaona kuna mlipuko tu na makombora hayaonekani, utasikia mlio yanakuja kupiga lakini huyaoni, ni kwamba yanaonekana ila kutokana na kasi yanapokwenda kupiga shabaha inakuwa vigumu kuyaona.

Ukichunguza utagundua re-entry vehicle yaani kile kichwa kinapokwenda kupiga hizo target kinakuwa na moto fulani, ila kinapita kwa kasi sana mpaka uwe makini.

Ipo hivi, haya makombora yanatumia plasma stealth technology na pia ni hypersonic missiles.

Hypersonic missiles ni missiles zenye kasi kubwa sana kuzidi sauti, hypersonic missiles speed yake ni zaidi ya mach 5 na kuendelea lakini kwa hizi missiles hapo kwenye video ni mach 8 au zaidi, Hypersonic missile inaweza kukwepa shambulizi licha ya kuwa kwenye speed kama mach 9.

Hizi kombora za Iran ni kama Zircon zile za Russia, Zircon ni latest na advanded kabisa hypersonic missiles, Iran sio kama tunavyoifikiria kwa kuambiwa na Western Medias, au kudanganywa na Western Media eti North Korea wana mapipa na sio silaha.

Jiulize nani alikuwa akiwasaidia Syria kule jangwani kufanya mradi wa Nuclear reactor? si North Korea.

Iran wakigeuza hii missile iwe ICBM , inaweza kupiga Washington na USA wasijue shambulizi limetoka wapi, utapigwa muda wowote na hutoweza kuzuia shambulizi, accuracy ya haya madude inaogopesha kwa kweli.
Hii missiles ikiiingia kwenye mikono ya Hezbollah sijui inakuwaje.

Nikisema mach 8 ina maana yana kasi mara 8 zaidi ya sauti yaani hapo linakwenda 9878km/hr au zaidi kwenda kupiga target, mpaka sasa hakuna defense system yenye uwezo wa ku intercept missiles zenye kasi ya namna hii, sio S-400 wala Patriot, kwa kasi ya hilo kombora sijui hio defense system ita lock target na kuanza ku track kwenda kulipiga, its impossible.

Nchi zenye technology kama hii zinahesabika amabapo kuna US, China na Russia na juzi hapa India nao waliingia kwenye chama, sasa kama hao wababe wana mashine kama hio na Iran naona wameonyesha kwamba huo utaalamu wanao.

Mbaya zaidi mfano Zircon ile ya Russia ilikuwa designed as anti-ship, yaani kupiga zile carriers na cruise.

Hypersonic missiles kama ile Zircon ya Russia zinaweza kukwepa mashambulizi pia hata katika speed kali kabisa,na hio hypersonic missile ya Russia walikuwa wanazijaribu 2020 hapo which means its latest technology, binafsi sishangai kuona kama Iran watakuwa na hypersonic missiles kwani wanawekeza sana kwenye teknolojia za missiles kuliko silaha yeyote.

Hizo kombora unaona zinawaka moto zinapokwenda kupiga target kwenye video, hio ni plasma, katika hio speed linatokea joto kali sana kati ya kombora na hewa hivyo kupelekea kichwa kuwaka kama moto (plasma cloud), inatokea cloud kuzunguka hizo kombora, sasa hii cloud inapelekea missile isionekane kwenye radar tokana na joto hilo kufyonza mawimbi ya radio/mawimbi ya radar.

Ina maana kwamba tayari hilo kombora hulioni kwenye radar na ukiliona je system zinaweza kuli intercept?

Juzi hapa hao hao Iran wamerusha missiles kwenda kutarget shabaha iliopo more than 1000km away na wakapiga shabaha. Ukweli ni kwamba carrier ya marekani kwa missiles za namna hii hachomoki mtu, nambie system gani inaweza ku intercept huo mwendo plus ina plasma cloud?

Hizi missiles zikielekezwa kama 12 tu kwenda kupiga carrier, hamtoona hata zilipotokea, na carrier itazamishwa tu, kuna hii mifumo kama Aegis system kwenye hizi cruiser za USA, Aegis system inasemekana inahitaji sekunde 8-10 kuingilia missile ya adui lakini kwa hizo sekunde 8-10 kombora linalokwenda kwa speed ya mach 8 linakuwa limetembea kilomita 20, are you there? na pia interceptor haitokuwa na kasi kuweza kuliwahi.

Hizo missiles zinaweza kuzamisha hata carrier advanced kabisa kama USS Gerald R.Ford, na hiki kinapelekea USA kuanza kujikuna kichwa katika matumizi ya carriers kwenye vita.

Kuna yale makombora yanaitwa bunker buster maalumu kabisa ya kupiga base zilizo chini ya ardhi, bado bunker buster hazioni ndani kwa kombora kama hizi Iran wameonyesha, unajua kwa sababu gani. Bunker buster ili iweze kupiga target iliyoko ndani ya ardhi inategemea mambo yafuatayo.

1-Imetengenezwa kwa material magumu na yenye weight sana (depleted uranium) kwa ajili ya kulipa bomu kinetic energy kubwa.

2-Wanayafanya yanakuwa na diameter ndogo na mbele yamechongoka ili kuyapa uwezo wa kupenetrate kwenye ardhi au target.

Haya bunker buster huwa yanaachiwa na ndege kama free falling body wakati hizi hypersonic missiles zinasukumwa na rocket engine.

Sasa linapokuja suala la missile inayotembea kwa speed ya mach 8 au 9,(more than 9800km/h) hio speed ikipiga carrier inatoboa kabisa na kutokea upande wa pili. Ina maana kinetic energy itakuwa kubwa zaidi, na kombora kama hili likiongezewa kinetic energy linaweza kuingia ndani kabisa ya ardhi more than 100m.

USA hizo carrier atakuja nazo bahari ya hindi kututishia huku sisi wanyonge, ila kwa wajanja, zile ni ngalawa tu za kufanyia uvuvi, I swear.

USA kuwa na carrier pia ni kutokana na base nyingi alizonazo ulimwenguni kote, kuwa na carrier kunakuwa na urahisi wa kufanya huduma mbali mbali, kama kupeleka silaha, ndege, askari n.k.

backpage-11601.jpg

Base za USA duniani.

Soma pia:

Ni jinsi gani Hezbollah iliweza kushinda vita dhidi ya Israel? (2006)

Je, Israel itaweza kushambulia vinu vya nuclear Iran?

By Mchichapori.
 
Nikuulize kwa nini ndege ya abiria aina ya Concorde ilisimamishwa kufanya kazi?
Hii ndege ilikuwa inakwenda speed ya mach 2.04, 2180km/hr, inabeba abiria zaidi ya 90.
Hio ilikuwa ni collaboration ya France na British, waliokuwa wanapanda ni wenye pesa.

Jifikirie nchi mbili zime join kufanya project kama hio, wanasayansi, engineers, bajeti waliyotumia,muda waliotumia n.k mwisho wa siku ndege zilirudi kupark baada ya miaka zaidi ya 20.
Hio ni kutokana na changamoto mbali mbali.

Sasa jifikirie kama France na Britain walikuwa hawana akili au ?
Kwa nini ushangae cariier kushambuliwa? walio design carrier wana akili na walio tengeneza concorde wana akili, hata waliotengeneza ile stealth RQ-170 sentinel iliyoshikwa na Iran wana akili.
Unapokuwa na akili fahamu kuna mtu upande wa pili ana akili kuliko wewe....
Ilisimamishwa na nani ? Zaidi ya hao waliokuwa wanaiendesha running cost zilikuwa kubwa mno

Cost per flight
Service per flight

Abiria enyewe unakuta inabidi sehemu pa laki tatu labda utoe 1Milion ndo uende ticket zaidi ya pesa mara tatu ya normal flight luxury kama sauli
 
Kumbe wangeweza idondoshea grenade ikasambaa bila kujulikana
Walisharusha hata drone juu ya carrier ya USA , na USA hawakujua chochote video hapo chini.

Pia Iran hao hao walikuwa wana spy drone ya USA kwa kutumia drone yao kwa juu bila hata ya waongozaji wa ile drone ya USA kufahamu, video hapo chini.
 
Fact zipi? Nyie ndo wapumbavu mnaoaminishwa ujinga hiv jiulize kati ya huyu mleta mada na mtengeneza hizo silaha nani anajua kuliko mwenzie? Unafikir hao waliotengeneza hizo silaha za mabilioni hawakujua kama kuna upande wa pili?....wa kujilinda? Umekaa zako madale huko ushavimbiwa ugali wako na siki unaungaunga mkono vitu vya kijinga rubbish
Wewe ni mzigo kwa taifa hili, rubbish
 
Mpishi anapika chakula halafu kuna mtu anatokea kwa ajili ya kuonja, aliye onja anasema chakula si kitamu na kimekosewa kupikwa, anatokea mtu mwingine na kumwambia muonjaji "kati yako na mpishi nani anajua kupika, ina maana wewe unajua kupika kuliko mpishi"?
Kumbe huyo mtu anayemwambia muonjaji hajui kitu kimoja kwamba, kuonja chakula na kufahamu kama ni kitamu au la haihitaji ujue kupika.

Tunapata feedback mitandaoni mkuu, moja wapo ni hiyo niliyoweka video kwenye huu uzi, jamaa aliyeshiriki designing ya ndege kama A-10 na F-16 akikosoa F-35, huyu mtu amefanya kazi Pentagon na amesomea hayo masuala, kwa nini nisimuamini?

Hata waliobuni ile stealth F-117(USA) iliyopigwa mwaka 1999 na S-125 kule Serbia waliibuni iwe stealth isionekane ili kujilinda, sasa kama S-300 haina capability ya kuona stealth, how comes S-125 ionadungua stealth?

kampuni za software zinabuni softwares kama adobe n.k kwa millions of dollars, kampuni za kutengeneza video games wanabuni gam,es kwa millions of dollars na miaka, lakini kuna hacker mmoja ambae yupo ndani na pc yake, ana hack kiulaini hilo game au software, watanzania wangapi tunatumia software za kununua? kama sio cracked.

Unafikiri kampuni za kutengeneza games na softwares hawajui kama kuna hackers wanaweza ku hack softwares zao? wanafahamu na wanajitahidi kuweka ulinzi lakini jinsi wanavyoweka ulinzi na hackers ndivyo jinsi wana umiza kichwa namna ya kudukua softwares hizo.

So the point is kutengeneza silaha za mabilioni haimaanishi kutodhibitiwa na silaha nyingine.......
Thanks
True
 
So whats your point?
Jaribu kufuatilia uzi vyema.
Nilichomaanisha kutolea mfano wa concorde ni jinsi walivyowekeza muda na pesa mwisho wa siku project ika buma.
Same na carriers, kutumia billions of dollars haimaanishi carrier haiwezi kuwa defeated, thats was my point.

Kipindi wana design concorde walijua wangeweza kukabiliana na kila changamoto, kumbe kuna changamoto walishindwa kuzitatua.

Same na carrier wameweka pesa nyingi lakini na zenyewe zinaweza kubuma pia, kuna silahakama hypersonic missiles kama Zircon, kama wataalamu wa mambo wanasema hypersonic haizuiliki na hakuna mfumo wowote duniani uliothibitishwa kuzuia hypersonic it means carrier its nothin kwa hypersonic.
Sasa tazama gharama ya hypersonic na gharama ya carrier twende sawa.

Concorde acha kusoma tu kwenye hizo blogs, nimetazama documentary, NAT GEO.
Ni blog ya mjinga mmoja ina matangazo mengi
 
Zinagongwa vizuri tu hizo
Iko hiv carrier unayoiona sio rahisi kuishambulia kizembe kama unavyodhani ina mitambo mingi ya kujilinda dhidi ya adui ina mitambo ya kuzuia makombora na ina mitambo ya kutoa tahadhar ya hatar inayoisogelea na isitoshe hiyo carrier huwa haitembei peke yake hata siku mmoja inatembea na zaidi ya destroyer 8 mpaka 10 kulingana na inapoenda(CARRIER STRIKE GROUP) zenye uwezo wa hali juu wa kushambulia target tofautitouti na kwa umbali mkumbwa kabla ya kulifikia hilo carrier tena katika msafara huo ipo mpaka submarine yenye uwezo wa kushambulia popote duniani(ballistic missile) .... Hiv mkuu hata wewe kwa akili ya kawaida hiv inawezakana carrier ya gharama likatembea bila ulinzi wowote tena karibu kabisa na maadui?

Picha chini nimeweka misafara zaidi ya 5 za carrier tofautitouti ikionyesha ikiwa na ulinzi mzito na namna carrier inavyolindwa

View attachment 1683646View attachment 1683650View attachment 1683652View attachment 1683651View attachment 1683653View attachment 1683656View attachment 1683654View attachment 1683655View attachment 1683657
 
Meli mbovu ile ilizama au unakuta iliharibika unakuta ipo beach au chini kabisa ya maji huwa zinajulikana kama shipwreck.

SS-Thistlegorm-Egypt-SHIPS0816-2000.jpg

640px-Titanic_wreck_bow.jpg

Kuna jambo nililiona hapo tarehe 15 hii january ambalo si la kawaida, katika kipindi hiki ambapo Iran na USA wamekuwa na mvutano mkali hasa baada ya kuuawa kwa Fakhrizadeh mwanasayansi wa atomiki wa Iran na Iran kuwanyooshea Israel kidole kusema wanahusika na kusema wanalipiza kisasi ndipo USA akawa makini na hakuwa na masihara.

USA wanafahamu vyema waajemi watalipa kisasi ni baada ya Iran kulipua zile kambi za kule Iraq Al Asad na Erbil na kusababisha askari 110 kupata traumatic brain injury kama kisasi kwa general Soleiman baada ya USA kumshambulia kwa drone.
Kwanza USA walituma carrier yao kubwa kabisa na B-52s, hio ni kuwaonyesha Iran kwamba wasithubutu hata kujikuna.

800px-USS_Nimitz_%28CVN-68%29.jpg

Long story short USA alikuwa anawaonyesha waajemi watapata kipigo cha mbwa koko, sote tunaijua USA vyema linapokuja suala zima la mashine za kivita hawa jamaa hawana mpinzani, lakini kuwa na mashine za kivita zenye teknolojia advanced kabisa ndio kushinda vita? hapana, ukitaka kujua ukweli jiulize B-52s takribani 19 kwenye ile vita kati ya vietnam na USA ziliwezaje kupigwa?

Niseme kitu kimoja, linapokuja suala zima la vita ile ya kweli, acha mazoezi, hizo silaha zinaweza kuwa hazina umuhimu sio S-400 wala Patriot,B-52s au Nimitz, linapokuja suala zima la vita ile vita kabisa hizo mashine ubora wake utabaki maabara tu, kweli nakuambia.
Majaribio ya hizi silaha kimaabara ni tofauti na zinapokwenda kwenye vita, haya majaribio yanapelekea kuuzwa silaha ambazo uwezo wake ni wa kimaabara zaidi na katika hali fulani, hivyo ndivyo Russia na USA wanavyokula pesa kiulaini.

USA na mwenzake Russia wanaziwekea kitu kinaitwa kill switch, just in case silaha kama hio imeangukia kwenye mikono si salama wanaweza wakazima hio silaha we ukabaki na toy tu, au just in case kuna jambo lina maslahi kwao wanazima tu (chwiip), unabaki na toy lako hapo ukidhani una silaha.

Kuna kisa kimoja kilitokea, Israel walikwenda kushambulia kinu cha nuclear pale Syria pasipo hata S-300 kufanya chochote wala radar hazikuona chochote huku Israel wakisema walizilisha radar hizo false signal, je ni kweli? hapana. Kuna kipindi Iran ilidai Russia ameuza codes za air defenses aina ya s-300 zilizopo Syria kwa Israel, ilikuwa ni 2017 nadhani Iran walitoa madai hayo, ndege za Israel zilikuwa zinaruka tu kwenda kufanya mashambulizi Syria na kupiga sites za Iran pasipo system hizo kufanya lolote au kutoa onyo kama kuna ndege zinakuja.

Inasemekeana hio operation ya mwaka 2007 ya kulipua kinu cha nuclear, tayari warusi walikuwa wamewauza Syria na mwenzake Iran, F-16s sio stealth, but how comes walifanya mashambulizi pasipop hata radar kutoa warning?

Kutokana na ukaribu uliopo kati ya Syria na Israel, defenses za Iran au hizo za Syria zilipaswa kutambua kama ndege zimeruka toka Israel kwenda kufanya mashambulizi.

Iran walibaki wametahamaki, bila ya Moscow kujua ikabidi Iran watume engineers waende Syria kubadili codes za defense system hizo ambazo zilikuwa chini ya jeshi la Syria, jamaa walifanikiwa kubadili codes na system zikawa active, inasemekana baada ya zoezi hilo systems hizo ziliweza kutambua ndege zilizoruka toka Israel na zikaweza kurusha missiles ku intercept mashambulizi ya ndege hizo.
Iran wanasema systems hizo kabla ya marekebisho ziliweza kutambua ndege hizo za Israel kama friendly planes na sio ndege za maadui kitu ambacho kinaweka wazi Israel walikuwa wanajua secret codes hizo.

Hizi S-300 na S-400 ni threat kwa Israel, jirani ambae ni adui kama Syria anapomiliki systems kama hizo, ujue hizi system zinaweza kugundua ndege inapotokea(inapo take off), kwa ukaribu uliopo kati ya Israel na Syria hizi system zinaweza kutoa taarifa pale tu ndege ya Israel imeruka, hata ikiwa kwenye anga lao, hiko kinapelekea kumpa adui target wapi akupige.

Katika kisa kimoja baada ya ndege kuruka ya Israel kwenda kufanya mashambulizi Syria, S-300 zikatoa taarifa kuna ndege zinaruka na Hezbollah wakarusha roketi la thamani ya $2000 pale pale ndege hio ilipotokea na missile ya Israel yenye thamani ya $3m ikaweza ku intercept kombora hilo, mambo mengine yanachekesha kweli kweli.

Wakati mwingine kuwa na silaha advanced na za gharama inaweza kula kwako, na hapo ndipo Hezbollah huwa wanaijambisha Israel. Wao wanaweza kutuma missiles za gharama ya chini kabisa, Israel waka intercept kwa advanced weapons, beleive it or not, Israel unaweza kuisifu ina advanced weapons na za gharama lakini Hezbollah wakaimudu Israel, katika vita ambayo Israel walipigana kwa muda mrefu ni ile ya 2006 dhidi ya Hezbollah na ilikuwa mwezi mmoja tu, vipi ingefika mwaka? Kwani huo mwezi mmoja myahudi ulimi ulimi ulikuwa umemtoka nje kama amekimbia km 1000, choka mbaya.

Unarushiwa kombora la milioni 4, na wewe una li intercept kwa kombora la thamani zaidi ya bilioni 6, je unaweza kumudu vita kwa muda gani? kama kombora la milioni 4 unalizuia kwa bilioni 6.how much money you got?

Missile ya Iron dome ni $40,000(Milioni zaidi ya 90), sio mchezo, Thats why Israel haiwezi kumudu vita vya muda mrefu, wao wakija kukupiga ni wiki tu.

Unaambiwa Hezbollah wana missiles kama 150,000 , anti-tank missiles, anti-ship missiles na ni wataalamu kweli kweli kuzitumia, Hezbollah na wao hizo missiles kujua wanaziweka wapi ni sawa na mtu kukuambia kanitafutie chozi la simba.

Mossad ya Israel kwa jinsi walivyo na intelejensia ya hali ya juu, walitafuta hizo kombora zilipo kwa muda wa miaka 6, na siku walipokwenda kupiga kwenye ile vita ya 2006, kumbe hamna kitu, Hezbollah wamekwisha hamisha zamani, can you imagine?

Niendelee........(2007/2008)

Ni kweli Russia waliwapa Israel codes kwa maslahi yao, ilikuwa hivi...
Kuna kampuni binafsi Mexico linaitwa HYDRA, hii kampuni inaitwa HYDRA wanahusika na kutengeneza drones zenye teknolojia ya hali ya juu , serikali ya Mexico iliwekeza pesa za kutosha kwenye hii kampuni, inasemekana hizi drone za Mexico ni bora zaidi kuliko za Israel katika majaribio ambayo yalifanywa.

Georgia walikuwa wanatumia drones ambazo zinatengenezwa na Israel katika kipindi chote hiki.

Hawa HYDRA walipata order ya kuwauzia hizi drones Georgia, kilichofanya Georgia wahitaji hizi drone kutoka HYDRA ni kwa sababu Georgia waligundua drones zao zilikuwa hacked na Russians, na hizi drones za HYDRA unapojaribu kuzihack huwa zina back up system haraka na papo hapo zinarudi kwenda kwenye base.

Georgia waliwapatia picha HYDRA picha ya moja ya drone yao ambayo ilikuwa imeanguka, lakini kwa picha ile inaonekana ile drone iliteremshwa kwa lazima ardhini na haikushambuliwa, kwa sababu ingeshambuliwa basi wangeona vipisi tu.
Na haikutokea mara moja, baada ya Georgia kugundua mchezo ikabidi wajaribu kuziuza drones za Israel hizo kwa Azerbaijan(haijulikani kama deal ilifanikiwa),

HYDRA walikataa kufanya biashara na Georgia kwa sababu ingeleta mvutano mkubwa sana kati ya Mexico na Russia, inasemekana Venezuela walikuwa wa kwanza kutaka kununua drone hizo lakini pia HYDRA walisita kutokana na mambo ya kisiasa.
Hivyo Israel waliwapatia Russians data link ili wahack drones za Georgia na Russia wakawapatia Israel codes za namna ya kuhack defense system ikiwamo Tor M1 na S-300 za Syria.

Unakumbuka kile kisa cha Iran kuiteremsha ile ndege stealth ya USA(RQ-170 Sentinel)? ina maana Iran walikuwa na data link ya ile ndege, sasa walipataje? mi sijui, ndio haya ninayosema silaha nyingine zitabaki kuwa na ubora maabara tu.

Kuna systems S-300 Russia waliziuza Greece, sasa siwezi jua ilikuwaje Turkey walipata taarifa nyeti kuhusu hii mifumo na wakaweza kushirikiana na Israel namna ya ku crack hii mifumo, kwa sababu ilileta mvutano sana baada ya Turkey kuona Greece wana s-300 miaka ya 90 mwishoni, na sasa Turkey ana nunua S-400, wakifanikiwa kuzi crack S-400 lazima tu Turkey watashare taarifa na Israel just in case kuna maslahi yakitokea, na Israel na USA ni allies.

Ukitaka kuamini ninachosema tafakari kwa nini Iran anatengeneza air defense systems zake binafsi, kwa nini wanatengeneza drones zao binafsi? ask your self, wanaujua mchezo uliopo. Na hapo hapo Russia na wao huwezi kujua kwa nini wamemuuzia Turkey hizo S-400,Linapokuja suala zima la ulaji kila mtu anapita kivyake.

USA baada ya kuona Turkey wamepata S-400 na yeye amekataa kuwauzia F-35 Turkey, S-400 inaweza kupata intelligence kuhusiana na stealth ya F-35 kwa madai ya Uncle Sam, lakini tujiulize.

Mboma Greece ilikuwa na S-300 na hatukusikia haya madai? basi tuseme S-300 haiwezi kusoma stealth, lakini vipi S-400 zilizopo Syria? s-400 ina range ya km 400, S-400 ikiwa Syria inaweza kusoma radar signature za F-35 zilizoko Israel, ipo wazi, yaani Russia wakajua F-35 stealth inaonekana vipi kwenye radar ya S-400, kumbuka stealth aircraft inapunguza tu uwezo wa kuonekana kwenye radar lakini hata radar ya mwaka 1945 inaweza kugundua stealth aircraft.

Hata Turkey akiwa na F-35 bado zitaonekana Iran, Azerbaijan, Georgia n.k. Lakini bado USA ana wapa vikwazo Turkey vya uchumi, why?

USA hawataki kuona yeyote akinunua silaha za Russia, na yeye anataka ndio awe on top kwenye soko kuliko mwingine yeyote, biashara ya silaha ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa USA, USA asipo piga mikwara kuhusu nchi nyingine kununua silaha za Russia basi wengine wote watafuata na kuanza kununua silaha za Russia.

Unaweza pia kujiuliza kwa nini USA hataki nchi za Ulaya kutumia gas ya Russia? au gas ya Russia itasoma stealth technology ya F-35?
Na ukija kwenye suala zima la gas hapo umemshika Putin goroli, Russia ipo kumlinda Assad kwa sababu ya gas yake iuzwe ulaya, na kweli amefanikiwa kumkalisha uncle Sam. Putin yule sio mtu kabisa, achana na yule mtu, niliona video moja mwandishi wa habari russia anamuuliza Putin, "hivi wewe ni alien"?.

eh9UEPFVzC3Gy0khAtmjAShcMFG7nb1x1.jpg

Putin anaendesha formular one racing cars, Putin anendesha submarine, Putin anajua kutumia silaha, Putin anaendesha farasi yupo kifua wazi , Putin anaendesha ndege, ni former KGB spy,Putin anajua kuzichapa, Putin ni James Bond katika uhalisia, James Bond yeye ni character kwenye fiction movie, sasa huyu jamaa ni James Bond wa uhalisia.

Putin ndio mtu tajiri zaidi duniani utajiri wake ina sadikika ni $200bn. Putin ndio karejesha heshima ya Russia baada ya uongozi wa rushwa na hovyo chini ya Yeltsin.

Putin ndio aina ya mtu ambae kipindi yupo shuleni walimu ndio walikuwa wakinyoosha mikono kumuuliza maswali na kipindi Alexander Ghanan Bell amevumbua simu basi alikuta missed call 3 za Putin, Putin ndiye alidondosha wallet bahati mbaya pale Switzerland mpaka leo hii inaitwa Swiss Bank.

Ni utani tu jamani tusielewane vibaya. Lakini kiukweli Putin anatisha, kama wazungu wenzie wanamuuliza "are u alien"? unafikiri ni kawaida.

Vladimir Putin alienda akaimega Crimea hapo 2014 kibabe wakati NATO wakipiga kelele wakiongozwa na USA, Vladimir Putin ndio aliingia pale Syria akatawanya wale magaidi ambapo Uncle Sam na wenzake walikuwa waki support, Vladimir Putin ndie alimtuliza Uncle Sam pale Venezuela akatulia.

Uncle Sam huwa tunatumia jina hili kumaanisha United Sates sasa unajua inakuwaje United States ilikuja kuitwa Uncle Sam? Ilikuwa hivi, kuna jamaa alikuwa akijulikana kwa jina la Samuel Wilson, huyu alikuwa mfanya biashara maarufu sana karne ya 19, kwenye ile vita ya mwaka 1812 ambapo USA walikuwa kwenye vita na United Kingdom of Great Britain na Ireland, usichanganye Great Britain ni kisiwa kikubwa ambapo kuna Scotland,Wales na England, Great Britain sio nchi tuelewane ni jina la kisiwa, unaposema United Kingdom unamaanisha Northern Ireland, England, Wales na Scotland.

Southern Ireland wapo peke yao, ukisema British Isle unamaanisha sovereign states mbili ambazo ni United Kingdom ya Great Britain na Northern Ireland na nchi nyingine ni Southern Ireland.

Samuel Wilson ndiye alikuwa akipeleka chakula kwa majeshi ya USA, Ilikuwa ni nyama ya ng'ombe(beef), sasa huyu jamaa alikuwa akijulikana pia kwa jina la Uncle Sam(Uncle Samuel), sasa kwenye yale mapipa yaliyokuwa yanabeba chakula yalikuwa na stamp imeandikwa US, US ikisimama kama United State as government property na pia US ni kifupi cha Uncle Sam, ndipo hapo United States ikawa inajulikana kwa nick name ya Uncle Sam.

Lakini naomba kidogo nikuelezee kwa nini Russia amemsaidia Assad, naomba nielezee kidoogooo.
Ipo hivi.

Kuna sababu nyingi zilizopelekea Russia kumsaidia Assad aendelee kukaa madarakani na kwa kweli amefanikisha hilo. Russia wana mfungamano na Syria kwa karibu zaidi ya miaka 50 sasa, Hafez Assad baba wa huyu Bashar Al Assad alichukulia mafunzo ya kurusha ndege vita toka kwa wasovieti na baada ya kuwa raisi wa Syria, Russia ndio walikuwa wauzaji wakubwa wa silaha nchini Syria.

EU hawana ujanja kwa gas ya Russia, waende mbele warudi nyuma gas ya mrusi ni muhimu kwao, sasa linakuja suala zima la maslahi ya kiuchumi, Russia anataka EU waendelee kutegemea gas yake na pia Russia anataka silaha zake aendelee kuziuza na nchi kama Syria ni wateja wao wakuu kama nilivyosema, hapo awali Hafez(Baba yake Assad) alikuwa na urafiki sana na Russia mpaka kuwaruhusu Russia kujenga base yao ya kijeshi Tartus mwaka 1971 walikuwa maswahiba kweli kweli.

Qatar wana gas reserve kubwa sana ni ya tatu kuwa na reserve kubwa duniani, ya kwanza ikiwa Russia ikifuatiwa na Iran.
Russia yupo kifua mbele kwa umuhimu wa gas yake Ulaya na hapo Ulaya kwa pamoja wakimuona Russia wanasimama kwa ukakamavu na kusema shikamoo Russia, Russia anaitikia marhaba hamjambo? hatujambo, basi kaeni chini,woootee wanakaa chini kwa utulivu.

Kwa hilo USA hataki kuona Russia anakuwa na ushawishi na kujenga uchumi wake kupitia Ulaya, USA anataka yeye ndio awe supplier mkubwa wa gesi Ulaya.

Unaweza ukashangaa lakini ndio ukweli huo, Russia inaogopeka, USA anaona ni bora hata yeye akose kuuza gas Ulaya auze mwingine lakini sio Russia. akishirikiana na Qatar.

Lakini uchukuzi wa gas toka USA mpaka Ulaya ni ghali, Russia na Ulaya ni majirani, hata USA ikijenga bomba la mafuta toka USA mpaka ulaya ni gharama sana na watapata hasara tu.

Germany ndio mteja mkubwa wa gas ya Russia kwa ulaya na hapo 2019 USA walitangaza vikwazo vikali kwa kampuni za ulaya zinazohusika na ujenzi wa pipeline iitwayo Nord Stream 2 zinazoshirikiana na kampunbi ya Russia iitwayo Gazprom, katika ujenzi wa Nord stream 2 Germany ndiye alikuwa akishirikiana na Russia kwenye ujenzi huo wa pipeline ya gas yenye distance kubwa zaidi duniani kwa zaidi ya kilomita 1200, Nord stream 1 ilishajengwa na hii nord strem 2 ilianza ujenzi hapo 2011.

2019 ubalozi wa USA nchini Germany ulituma barua kwenda kwa makampuni yanayojihusisha na ujenzi wa bomba hilo la gesi kusimamisha ujenzi haraka kabla ya kukutana na vikwazo vikali.

43318158_7.png

Mabomba ya Nord Stream 1 na 2

20170410_CIA1_0.jpg

pendekezo la ramani ya Mabomba toka middle east Qatar na Iran kwenda ulaya

Tunaona jinsi USA ambavyo anapiga vita biashara ya gas kati ya Russia na nchi za Ulaya, USA na Qatar walitaka kutengeneza bomba la gas, kumbuka nimekueleza Qatar ni moja ya nchi yenye gas reserve kubwa duniani, USA alitaka Qatar awachallenge Russia kwa uuzaji wa gas pale Ulaya.

Lilitokea pendekezo la kujenga bomba la gas kutoka Qatar kwenda Ulaya kupitia Saudia then liingie Syria na kuikamata Turkey moja kwa moja mpaka Europe, USA walitoa baraka zao zote juu ya ujenzi huo wa bomba, lakini lazima bomba lipite Syria, kumbuka nilisema kwamba Syria ni mshirika mkubwa wa Russia kistratejia tangu enzi za baba yake Assad,na Assad hataki kuwaharibia swahiba zake warusi kwa sababu Russia anatengeneza uchumi wake kupitia gesi anayouza Ulaya, pindi gas ya Qatar ikiingia Ulaya ita challenge warusi na kuwaharibia uchumi wao.

Syria ikakataa katu kumuuza swahiba wake Russia kwa kupitisha bomba hilo kwenda Turkey kuingia ulaya, hapo Turkey kakosa ulaji kama simba aliyekosa swala mnono nakubaki kujilamba tu, sasa Turkey pia hawapendi uwepo wa Assad.

Qatar imefund vikundi vya kigaidi kupambana na uongozi wa Assad kwa kutoa dola bilion 3, Saudia Arabia pia amekuwa aki fund makundi ya kigaidi kushambulia Syria lengo likiwa kumtoa Assad, Turkey nae ali support anti-Assad groups.

Ukija kwa Turkey na yeye anategemea gesi ya Russia, kwa uongozi wa Assad kuanguka na ujenzi wa bomba la gas toka Qatar kupitia Turkey utamfanya awe huru dhidi ya utegemezi wa gas ya Russia. Pia kwa bomba la gas kupitia kwao lazima wangekuwa wanalipwa transfer fee.

Lakini hapo hapo tena kuna pendekezo la Iran pia kutengeneza bomba la gas, kumbuka nilisema kwamba ikitoka Russia kwa reserve kubwa ya gas inafuata Iran na kuingia kufuatiwa na Qatar, sasa Iran nao walitaka kufikisha gas yao kufika ulaya kupitia Iraq na Syria, Russia na Assad wakatoa baraka zao zote kwa Iran kupitisha bomba lao la gas Ulaya.

Iran ana matumaini kabisa siku moja anaweza kuwa mfanya biashara mkubwa wa gas pale Ulaya tokana na waliacha kuendeleza ICBMS, kwani kwa jinsi walivyo karibu na Ulaya, nchi za Ulaya zingeona ni threat kwao, lakini ICBM ya kufika USA wanayo. Shahab-6.

Kuna video moja niliiona wapiganaji wa Hezbollah walikutana na wapiganaji wa ISIS kule Syria, mpiganaji wa Hezbollah mmoja akaona haina haja ya kuanza vita ikabidi aanze maongezi nao wale wagaidi wa ISIS.
Mongezi yao kwa ufupi yalikuwa hivi...........video ipo hapo...

Hezbollah Soldier: Kuna mtu anakuja kuongea nanyi, kwa nini bado mmeshikilia silaha zenu? naona kama mnaogopa.

Hezbollah soldier: Hivi mmeona hali ya Al Zabadaan jana? Jinsi ilivyokuwa na jinsi ilivyo sasa, Al Zabadaan ilikuwaje miaka mitatu iliyopita na iko vipi sasa?

Hezbollah soldier: Nataka niwaambie kitu kimoja, msiwaamini viongozi wenu, Mnashuhudia nini kinatokea Zabadaani, sasa mpo hapa hamuogopi mnapigana lakini wako wapi
viongozi wenu au makamanda wenu?

Hezbollah soldier: Jina lako nani?

ISIS : Jina langu ni Abdullah.

Hezbollah soldier: Hata mimi jina langu ni Abdullah, sikiliza rafiki yangu nataka nikueleze ukweli, watu wanaolipa gharama ya vita ni wale walioko kwenye vita unafahamu hilo? Umesoma Quran? umesoma kitabu kitakatifu?

Wadhalimu ni Israel na America na sio ninyi wala waislamu wengine, tukubaliane kwa sasa sisi ni maadui lakini wapaswa kujua kwamba unanufaisha mpango wa hatari ambao hautakuwa na maslahi kwako, Mnawanufaisha Israel na wenzake, angalau naweza kuongea nanyi lakini makamanda wenu hawawezi kunisikiliza, hao ni wezi, mbwa,woote ni wafanya biashara wanaotumia wengine na watu wasiokuwa na makosa kulipa gharama ya vita.

Viongozi wenu hawapo kwenye hii vita,wapo busy sana wakitumia muda wao kula maisha huko America, Viongozi wenu wa Saudi, Qatar wapo busy wakicheza muziki huko America, tazameni wenyewe kwenye mitandao hakuna kinachojificha, Tazameni Gulf States wanachokifanya kwenye nchi zao.

Nafahamu viongozi wenu wamewalisha chuki dhidi ya Iran, wakiwaambieni Iran ni adui yenu, lakini Iran ana adui mmoja tu na huyo ni Israel.

ISIS : Vipi kuhusu Assad na uhalifu aliofanya?

Hezbollah Soldier: Upo sahihi na una haki ya kusimama lakini unapaswa kuelewa kwamba katika hiki kipindi haupiganii katika kile unachokiamini, Unapigania wale wanaosambaza chuki na kunufaika na hii vita, sipigani kwa ajili ya kumtetea au kumpinga Assad kwa sababu mimi sio Syrian, labda kama kuna mtu nyuma yake aliwaumizeni lakini binafsi hajaumiza yeyote.

Rushwa zipo kwenye kila serikali, hili linajulikana, hata serikali yetu na hata kwenye misikiti kuna watu ni wala rushwa, kuna mpango mkubwa wa kumuondoa Assad kwa sababu ya kuwa kinyume na Israel, USA na rafiki zake, watawatumieni ninyi, na maelfu kama ninyi kumuondoa Assad madarakani, nawaambieni kuna rushwa Syria, Lebanon na kwenye kila serikali. Tunamuomba tu mungu atusaidie, hivi mnafahamu walichokifanya Israel Lebanon? walitengeneza Hakat Amal wapigane na Hezbollah , shia wanaua shia wenzao.
Kulikuwa na nyumba moja ya ndugu watano, mmoja ni Amal,mwingine ni Hezbollah na nakadhalika.

ISIS: Sasa hivi wametengeneza Shia dhidi ya Sunni

Hezbollah Soldier: Hawawezi kuwaambieni ukweli wote, hii vita ni ya Israel, sasa hivi wapo wanakunywa whyskey wakitutazama tunavyouana sisi kwa sisi, wana furaha sana kwa sababu hata silaha mnazotumia zinatoka Saudi na Qatar, toka sasa hivi uende ukaangalie hao Saudi na Qatar walipo.

Hayo yalikuwa maongezi mafupi kati ya magaidi(ISIS) na mpiganaji wa Hezbolllah, hao askari wapo Syria, sio wapo Syria tu bali wapo vitani,wanajua mengi kuliko wewe na mimi tupo huku Africa tena tukitumia mitandao kufahamu yanayoendelea.

Niliposema kwamba vita dhidi ya Assad ni ya maslahi kuna ambao mtaona naongopa, lakini ndio ukweli huo, mmeshuhudia hio conversation.

Maneno ya huyu askari wa Hezbollah yanaonekana kumuingia kabisa huyo jamaa wa ISIS, Kaa ujue gaidi anaweza kutengenezwa, akatumiwa na kisha akauzwa kama bidhaa, gaidi ni silaha pia kama unavyoona vifaru vya kivita, hapo ndipo ulimwengu ulipofikia, na unatumiwa pasipo hata kufahamu kama unatumiwa.

Niendelee sasa......USA hataki kabisa kuona Russia ya Putin inarudi kwenye mchezo.

USA anataka yeye ndiye silaha zake ziwe sokoni, yeye ndie awe na control ya silaha zake, wazee wa kill switch ukizingua tu wanabonyeza button.

Turkey wanataka wawe na system inayojitegemea ya ulinzi, hapo middle East kila mmoja ana maslahi yake, USA wakati mwingine wanaweza kuwa na maslahi tofauti na Turkey mfano USA anavyo wapatia baadhi ya vikundi silaha nzito middle East kwenye hii vita ya kumtoa Assad, Turkey inaweza kuwa kwenye danger, na hapo inabidi wajitegemee kivyao kwenye masuala ya kiulinzi.

Mfano mzuri ni USA anawapatia Kurds silaha, Turkey anapambana na Kurds.

Kwa nini basi USA wasiwatoe Turkey kwenye umoja wa NATO?
Turkey kwenye umoja wa NATO wao ndio wanashikilia nafasi ya pili kuwa na nguvu ya kijeshi baada ya USA, Turkey kuna base za USA(NATO) zipatazo
24.
Operation zoote kwenda middle east zinatokea kwenye hizo base za Turkey, Turkey kujitoa NATO ni loss kubwa sana kwa USA, subiri kwanza USA apate base
zingine middle east then watakua tayari kumtoa Turkey.

Niendelee na mada sasa...

Niliposema niliona kitu kilichonishangaza tarehe 15, ilikuwa ni video niliona Iran waliirusha kwenye vyombo vya habari wakimjibu USA, huu mchezo ni kama wewe si una hiki? na mimi nina hiki, wanadorishiana mashine za kivita.

Na sio mashine tu za kivita, ni mashine za kisasa kabisa, hizo B-52s za USA usifikiri ni zile za Vietnam eti zinaruka usawa wa target na kuanza kuhara mabomu, hapana, hizi za sasa zinaruka mbali na wewe ile tunasema stand off missiles zinarushwa hata 500 km away, then hizi cruise missiles kama AGM-28,AGM-69 zinaanza kukufuata kuja kukuharibia siku yako nzima.

B-52 inaweza kutanguliza missiles kutambua tu ni wapi S-400 zipo, yaani hilo missile likiwa linakuja huku linauliza S-400 uko wapi?
S-400 bila kujua inazugwa inajitokeza nipo hapa tena kwa sauti, huku S-400 ikiwa inatoa missile yake huku ikitoa mwanga kama mti christmas, tayari infrared detectors zinaona tukio zima, linatumwa sasa cruise missile la pili lenye stealth capability, basi S-400 inapigwa na kusambaa, then B-52 linakuja sasa, linakunyea hapo mpaka basi.

b-52h_static_display_arms_06_3.jpg

Hio ni B-52 na kombora zake

Niendelee na mada..... Niliona hii video youtube Iran wakifanya mazoezi ya kijeshi, kwanza hawa jamaa wametengeneza drone zenye teknolojia ya kutisha, hizi ni stealth halafu zinaweza kwenda kupiga target km 1000 umbali, na pia ni kamikaze drones, yaani ikija yenyewe ndio silaha inapiga target na kulipuka.

Hapa waajemi nawapa shikamoo, tafadhali tazama video hapo chini ili twende sawa, kuna missiles na drone utaziona then nataka nifanye uchambuzi kidogo. Video ina dakika 1 tu.

View attachment 1682085
Tazama hio warhead yenye plasma cloud ikienda kupiga target. nimeizungushia mduara mwekundu.

f48c4dbdbb58470186b5725eda7ec379.png

AZ_3447_resize.jpg

Hivi katika mvutano kama huu ambapo USA anaonyesha midude kama carriers, Iran walinishangaza, niliona wanafanya testing ya missiles.

lakini mbona missiles mbona hata hamas wanazo? wanamuonesha nani missiles? Baada ya kujiuliza hivyo ndipo nikawa makini na kugundua ujumbe mzito uliokuwa kwenye hio video, tena hii video nimeiona hii january 15 tu hapo majuzi.

Sehemu ya kwanza wanaonyesha missiles zilizobebwa kwenye magari zinavyo kwenda kupiga target, sehemu ya pili ni drones zikifanya mashambulizi.

Kwenye missiles ndipo palipo nishtua na kuona ni kweli Iran wanaweza kupiga carrier, beleive it or not, wajuzi wa mambo wameona , walio na macho wameona.

Hizo missiles zilizopigwa kwenye hio video ni advanced, kwanza kabisa ni stealth kwa mujibu wa jeshi la Iran, tuachilie mbali stealth technology haya makombora yana kitu cha ziada.

Hio video ya youtube ipeleke kuanzia sekunde ya 59, tazama kwa makini, utaona kuna mlipuko tu na makombora hayaonekani, utasikia mlio yanakuja kupiga lakini huyaoni, ni kwamba yanaonekana ila kutokana na kasi yanapokwenda kupiga shabaha inakuwa vigumu kuyaona.

Ukichunguza utagundua re-entry vehicle yaani kile kichwa kinapokwenda kupiga hizo target kinakuwa na moto fulani, ila kinapita kwa kasi sana mpaka uwe makini.

Ipo hivi, haya makombora yanatumia plasma stealth technology na pia ni hypersonic missiles.

Hypersonic missiles ni missiles zenye kasi kubwa sana kuzidi sauti, hypersonic missiles speed yake ni zaidi ya mach 5 na kuendelea lakini kwa hizi missiles hapo kwenye video ni mach 8 au zaidi, Hypersonic missile inaweza kukwepa shambulizi licha ya kuwa kwenye speed kama mach 9.

Hizi kombora za Iran ni kama Zircon zile za Russia, Zircon ni latest na advanded kabisa hypersonic missiles, Iran sio kama tunavyoifikiria kwa kuambiwa na Western Medias, au kudanganywa na Western Media eti North Korea wana mapipa na sio silaha.

Jiulize nani alikuwa akiwasaidia Syria kule jangwani kufanya mradi wa Nuclear reactor? si North Korea.

Iran wakigeuza hii missile iwe ICBM , inaweza kupiga Washington na USA wasijue shambulizi limetoka wapi, utapigwa muda wowote na hutoweza kuzuia shambulizi, accuracy ya haya madude inaogopesha kwa kweli.
Hii missiles ikiiingia kwenye mikono ya Hezbollah sijui inakuwaje.

Nikisema mach 8 ina maana yana kasi mara 8 zaidi ya sauti yaani hapo linakwenda 9878km/hr au zaidi kwenda kupiga target, mpaka sasa hakuna defense system yenye uwezo wa ku intercept missiles zenye kasi ya namna hii, sio S-400 wala Patriot, kwa kasi ya hilo kombora sijui hio defense system ita lock target na kuanza ku track kwenda kulipiga, its impossible.

Nchi zenye technology kama hii zinahesabika amabapo kuna US, China na Russia na juzi hapa India nao waliingia kwenye chama, sasa kama hao wababe wana mashine kama hio na Iran naona wameonyesha kwamba huo utaalamu wanao.

Mbaya zaidi mfano Zircon ile ya Russia ilikuwa designed as anti-ship, yaani kupiga zile carriers na cruise.

Hypersonic missiles kama ile Zircon ya Russia zinaweza kukwepa mashambulizi pia hata katika speed kali kabisa,na hio hypersonic missile ya Russia walikuwa wanazijaribu 2020 hapo which means its latest technology, binafsi sishangai kuona kama Iran watakuwa na hypersonic missiles kwani wanawekeza sana kwenye teknolojia za missiles kuliko silaha yeyote.

Hizo kombora unaona zinawaka moto zinapokwenda kupiga target kwenye video, hio ni plasma, katika hio speed linatokea joto kali sana kati ya kombora na hewa hivyo kupelekea kichwa kuwaka kama moto (plasma cloud), inatokea cloud kuzunguka hizo kombora, sasa hii cloud inapelekea missile isionekane kwenye radar tokana na joto hilo kufyonza mawimbi ya radio/mawimbi ya radar.

Ina maana kwamba tayari hilo kombora hulioni kwenye radar na ukiliona je system zinaweza kuli intercept?

Juzi hapa hao hao Iran wamerusha missiles kwenda kutarget shabaha iliopo more than 1000km away na wakapiga shabaha. Ukweli ni kwamba carrier ya marekani kwa missiles za namna hii hachomoki mtu, nambie system gani inaweza ku intercept huo mwendo plus ina plasma cloud?

Hizi missiles zikielekezwa kama 12 tu kwenda kupiga carrier, hamtoona hata zilipotokea, na carrier itazamishwa tu, kuna hii mifumo kama Aegis system kwenye hizi cruiser za USA, Aegis system inasemekana inahitaji sekunde 8-10 kuingilia missile ya adui lakini kwa hizo sekunde 8-10 kombora linalokwenda kwa speed ya mach 8 linakuwa limetembea kilomita 20, are you there? na pia interceptor haitokuwa na kasi kuweza kuliwahi.

Hizo missiles zinaweza kuzamisha hata carrier advanced kabisa kama USS Gerald R.Ford, na hiki kinapelekea USA kuanza kujikuna kichwa katika matumizi ya carriers kwenye vita.

Kuna yale makombora yanaitwa bunker buster maalumu kabisa ya kupiga base zilizo chini ya ardhi, bado bunker buster hazioni ndani kwa kombora kama hizi Iran wameonyesha, unajua kwa sababu gani. Bunker buster ili iweze kupiga target iliyoko ndani ya ardhi inategemea mambo yafuatayo.

1-Imetengenezwa kwa material magumu na yenye weight sana (depleted uranium) kwa ajili ya kulipa bomu kinetic energy kubwa.

2-Wanayafanya yanakuwa na diameter ndogo na mbele yamechongoka ili kuyapa uwezo wa kupenetrate kwenye ardhi au target.

Haya bunker buster huwa yanaachiwa na ndege kama free falling body wakati hizi hypersonic missiles zinasukumwa na rocket engine.

Sasa linapokuja suala la missile inayotembea kwa speed ya mach 8 au 9,(more than 9800km/h) hio speed ikipiga carrier inatoboa kabisa na kutokea upande wa pili. Ina maana kinetic energy itakuwa kubwa zaidi, na kombora kama hili likiongezewa kinetic energy linaweza kuingia ndani kabisa ya ardhi more than 100m.

USA hizo carrier atakuja nazo bahari ya hindi kututishia huku sisi wanyonge, ila kwa wajanja, zile ni ngalawa tu za kufanyia uvuvi, I swear.

USA kuwa na carrier pia ni kutokana na base nyingi alizonazo ulimwenguni kote, kuwa na carrier kunakuwa na urahisi wa kufanya huduma mbali mbali, kama kupeleka silaha, ndege, askari n.k.

backpage-11601.jpg

Base za USA duniani.

Soma pia:

Ni jinsi gani Hezbollah iliweza kushinda vita dhidi ya Israel? (2006)

Je, Israel itaweza kushambulia vinu vya nuclear Iran?

By Mchichapori.

Kaka waambie waajemi basi waipoteze Israeli kwenye ramani kama wanavyosema na waambie Hezbollah waache maneno matupu wawe wanatuonyesha na damage zao katika vita sio ngonjera tu na propagandas
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom