Urais ni taasis kubwa yenye mkono mrefu inayoweza kufika kona yoyote ya nchi kupata habari sahihi kwa wakati sahihi.
Lakini kwa hali inavyoendea nchini naanza kupata shaka na intelligence na watu wanaompa taarifa rais.
Kwanza rais kila siku anahubiri kuwa wanaoisoma namba ni wavivu na mafisadi, hivi kweli taarifa sahihi zinamfikia kuwa wakulima na wanyonge ambao wanajituma katika shughuli zao ndo wananyanyasika huku hakuna fisadi hata mmoja kwenye hao tunaowasikia anaisoma namba? Mahakama imeanzishwa lakini hakuna kesi hata moja ya maana tumeisikia sasa ilikuwa na haja gani kuanzishwa.
Pili ajira, je serikali ilipokuwa inaahidi ajira kwa vijana wakati wa kampeni haikujua vijana wanatakiwa kujiajiri hivi hatuwezi kuajiri huku tunaendelea na uhakiki wa watumishi hewa?, intelligensia inajua ni kiasi gani serikali inapoteza kwa kutoajiri wafanyakazi kwenye taasisi mbalimbali? Maana hawaajiriwi kusaidia serikali bali kuleta faida serikalini.
Tatu, serikali inatambua kuwa raia wengi wanaombea rais afeli ili abadilishe muolekeo wake qa kutokushaurika? Au bado wanakaa kukariri kwamba huku mtaani bado wapendwa na kusifiwa kama watetezi wa wanyonge.Inajua kuwa wazee wazalendo walisiolipwa mafao yao hawana imani tena na serikali, inajua kuwa vijana wanaofanya kazi kwa mkataba na hawajapata mafao yao hawasikilizi tena habari za "serikali ya wanyonge" inafahamu kwamba wanafunzi waliokosa mkopo na watu wa kagera hawawatazami kama walivyowatazama awali.
Ni wakati serikali iache michezo ya kuigiza na matamko yasiyo na tija ni wakati wa serikali kukubali walipotea waanze upya kwa kushughulikia matatizo ya wananchi. Sio kuhangaika na ndege, mahakama ya mafisadi na sheria kandamizi za habari. Tunataka tuambiwe tulime mazao gani maana no viwanda gani vinajengwa na sio ubabaishaji.