Je, Intelijensia ya Jeshi (JKT) haina uwezo wa kung'amua mambo ndani ya Jeshi?

DARUSO siku hizi ni tawi la UVCCM bila kadi ya chama hugombei. Hasa DUCE. Madogo wote wajinga wajinga tu.
Dah! Miaka hiyo likiitishwa kunji, basi ni kunji kweli! Ole wako uonekane eti uko darasani unapiga msuli! Unatolewa na viboko kudadeki! Waoga wote wa mgomo mara zote walibaki hostel au kwenye mageto yao, siku zote tulipo goma! Na ilikuwa ni lazima kieleweke.

Maprof. na Madokta vichwa maji walitolewa kwenye ule ukumbi wa Nkrumah wakiwa wamebebwa mzobe mzobe!! Sasa leo naambiwa DARUSO ni Uvccm! aka Mlenda mlenda!! Kweli siku zinaenda kasi sana.
 
Sasa sijui tusemee wapi?

Vijana 30 - 1 sasahiv wanahangaikaa. (huyo mmoja alipigwa Risasi alipoenda kutafuta ridhiki usiku

Alafu sasa mpaka mwanasheria mkuu..,alikubali kua,

HUWEZI KUFUKUZWA KWA MDOMO( jamaa walifukuzwa kwa mdomo, nakupewa hela ya nauli kila mmoja)

WALIFUNGWA GEREZA LA UKONGA.

MPAKA LEO HAWAJAPEWA BARUA ZA KUFUKUZWA.

HATA KM WANGEPEWA, VIPI STAHIKI ZAO????
Askari hawezi kushtakiwa kwa kosa la jinai kabla ya kufukuzwa kazi, atafukuzwa kwanza kaz kwenye mahakama ya kijeshi alaf atapelekwa mahakama ya kiraia ndo huko ataenda gerezan, ila kama hakutendewa haki anaweza kukata rufaa na kama alionewa atalipwa fidia pamoja na kurudishwa kazini
 
Kama wameasi kweli basi wamepata stahiki yao.

Tena bora wafungwe hata miaka 100 tuu kabisa, waasi sio watu wa kucheka nao kabisa
 
Nimemsikiliza Jana CDF Jenerali Mabeyo akisema Kwamba takriban Vijana 854 wamefukuzwa Jeshi kwa Kufanya maandamano na Kugoma ambapo alisema ni uasi.

Je, Hao Vijana Kama Walikuwa na Uwezo Wa Kupanga na Kufanya Uasi ndani ya Jeshi ina maana intelijensia ya Jeshi Haina Uwezo Wa Kugundua Hivi Vitu na Kuzima Hizi Harakati za Hawa Vijana Mapema?

Haya wanaondolewa Jeshini na Wana kila Aina ya Mafunzo Je Wakiwa uraiani Watafuatiliwaje Ili wasifanye Madhara Yoyote Kwa Wananchi au Wanaweza Kujiunga Hata na Magenge Ya Uhalifu.

Je, wataachwa kiholela bila Kufuatiliwa Serikali ikajua wanafanya nn?

Cc MtamaMchungu JokaKuu
Mkuu hawa hawana hiyo 'Kila aina ya mafunzo' ya Jeshi Uliyoandika, isitoshe hawa ni wale walikuwa wa kujitolea, siyo wote wanapata ajira, wengine hurudi nyumbani kuendelea na maisha,
 
Jkt hawana hicho unachoita kila aina ya mafunzo

Wanalima na kufuga tu
 
Askari hawezi kushtakiwa kwa kosa la jinai kabla ya kufukuzwa kazi, atafukuzwa kwanza kaz kwenye mahakama ya kijeshi alaf atapelekwa mahakama ya kiraia ndo huko ataenda gerezan, ila kama hakutendewa haki anaweza kukata rufaa na kama alionewa atalipwa fidia pamoja na kurudishwa kazini
Kwa Sheria ipi? Walevi wa wanzuki huwa mnabuni-buni tu.
 
Nimemsikiliza Jana CDF Jenerali Mabeyo akisema Kwamba takriban Vijana 854 wamefukuzwa Jeshi kwa Kufanya maandamano na Kugoma ambapo alisema ni uasi.

Je, Hao Vijana Kama Walikuwa na Uwezo Wa Kupanga na Kufanya Uasi ndani ya Jeshi ina maana intelijensia ya Jeshi Haina Uwezo Wa Kugundua Hivi Vitu na Kuzima Hizi Harakati za Hawa Vijana Mapema?

Haya wanaondolewa Jeshini na Wana kila Aina ya Mafunzo Je Wakiwa uraiani Watafuatiliwaje Ili wasifanye Madhara Yoyote Kwa Wananchi au Wanaweza Kujiunga Hata na Magenge Ya Uhalifu.

Je, wataachwa kiholela bila Kufuatiliwa Serikali ikajua wanafanya nn?

Cc MtamaMchungu JokaKuu
Ndugu yanguunaposema wana kila aina ya mafunzo unakosea Sana'a hebu jaribu kufatilia
 
Kusema hao njuka wamepata kila aina ya mafunzo ni kulinajishi jeshi!

Kama wameshindwa kuwa wavumilivu wakagoma, waache wale jeuri yao! Na huko mtaani wakithubutu kufanya uhalifu eti kwa sababu wamefuzwa kwata kidogo na kushika gobole watanyofolewa shingo!

Mambo mengine yanatokea kwa sababu, maalum! Elewa jeshini si sehemu ya ajira! Wanajeshi si waajiriwa!

Naungana na Mabeyo!

popoma lingine hili hapa
 
Unavyosema wana kila aina ya mafunzo una maanisha nini...!?

Hawa wamepitia tu huko jkt miaka mitatu, tena zaidi walikuwa wanajishughulisha na shughuli za ujenzi na mafunzo waliyoyapata jeshini huko ni haifiki hata 5% ya mafunzo ya jeshi!

Sasa wewe unakurupuka eti wana kila aina ya mafunzo!

Hao hata raia wa kawaida ambaye hajapitia hata mgambi anaweza kuwakunja!
Wanajua matumizi ya bunduki ? Au mpaka wawe wanajeshi ndio wanafundishwa kutumia bunduki ? Na vitani kinacho tumika kumuua adui ni bunduki au ni mafunzo asilimia 1000%?
 
popoma lingine hili hapa

Najua bado hujapata kazi ya body guard uchwara, kama vipi nitumie vielelezo vyako pm, nikupe mchongo uondokane na stress za kukosa ajira!

MkNadhani baada ya kuwatumisha bila malipo kwenye miradi ya ujenzi ni wakati sahihi kuwatema.Si kweli kwamba hawana intelligent ya kugundua viasilia vyovyote kabla ya tukio.
Hapana ukweli usemwe malipo walikua wanapata na wanajua wanapewa sh ngapi na haya wakati wanajaza mkataba walikua wanajua posho sh ngapi.
 
Nimemsikiliza Jana CDF Jenerali Mabeyo akisema Kwamba takriban Vijana 854 wamefukuzwa Jeshi kwa Kufanya maandamano na Kugoma ambapo alisema ni uasi.

Je, Hao Vijana Kama Walikuwa na Uwezo Wa Kupanga na Kufanya Uasi ndani ya Jeshi ina maana intelijensia ya Jeshi Haina Uwezo Wa Kugundua Hivi Vitu na Kuzima Hizi Harakati za Hawa Vijana Mapema?

Haya wanaondolewa Jeshini na Wana kila Aina ya Mafunzo Je Wakiwa uraiani Watafuatiliwaje Ili wasifanye Madhara Yoyote Kwa Wananchi au Wanaweza Kujiunga Hata na Magenge Ya Uhalifu.

Je, wataachwa kiholela bila Kufuatiliwa Serikali ikajua wanafanya nn?

Cc MtamaMchungu JokaKuu
Intelijensi ipo imara haswaa pale Jeshini..

Sema yawezekana hilo jambo walilopanga hao vijana lilifika mezani mapema( Understand the Current condition of Operation(U.C.O))

watu Makini wakachambua na kudadafua madhara yake wakaona(Visualize Desired condition of Operation(V.D.O)) hakutokuwa na Challenge Wakawaacha vijana watekeleze lengo na dhumuni lao ili Cognitive Hierarchy Model (C.H.M) ya jeshi itoe FUNDISHO KWA WATAKAO TAMANI,THUBUTU AU JARIBU SIKU NYINGINE...

"Ubinadamu lazima umalize vita kabla ya vita kumaliza wanadamu"
 
Unavyosema wana kila aina ya mafunzo una maanisha nini...!?

Hawa wamepitia tu huko jkt miaka mitatu, tena zaidi walikuwa wanajishughulisha na shughuli za ujenzi na mafunzo waliyoyapata jeshini huko ni haifiki hata 5% ya mafunzo ya jeshi!

Sasa wewe unakurupuka eti wana kila aina ya mafunzo!

Hao hata raia wa kawaida ambaye hajapitia hata mgambi anaweza kuwakunja!
Mwenyewe nawashangaa sana watu wanaosema kauli za aina hiyo, jamani jeshi halina mwenye mafunzo kiasi cha kutishia kwamba hawezi kuchukuliwa hatua pale anapokosea since hicho kinachoitwa mafunzo aliyonayo kuna watu walimfundisha.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom