Je ingekuwa majambazi wameteka na kumtesa polisi wangekuwa bado hawajapatikana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ingekuwa majambazi wameteka na kumtesa polisi wangekuwa bado hawajapatikana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maingu z, Jul 22, 2012.

 1. m

  maingu z Senior Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana jf, nimekuwa nikifikiri na kufuatilia sana matukio ya ajabu na ya kutisha yanayotokea nchini mwetu, hasa ya ujambazi, wa kutumia silaha, ufisadi wa mali asili ya umma, na hili la sasa kutekwa na kuteswa ULIMBOKA, katika kufuatilia nikagundua kitu kimoja kwamba, matukio ya aina hii yanapowatokea raia wa kawaida, matokeo yanakuwa wahusika wala hawakamatwi na wala hakuna anatilia mkazo wa kufuatilia na kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa. La ajabu ni pale matukio ya wanasiasa wa upinzani kupinga ukandamizaji, wafanyakazi kudai haki yao kwa migomo, na maandamano ya raia kudai maisha bora, Hakika watashughulikiwa na kukamatwa na kushitakiwa haraka sana? Pia ikiwa chombo kama polisi wamepigwa na majambazi basi hao watu wanapatikana haraka sana. Sasa hoja yangu hivi vyombo vya dola kama Polisi vina haja ya kuendelea kuwepo, si bora ieleweke kuwa hakuna polisi wala usalama TIS(TANZANIA INSURGENCE SERVICES)( hii labda ndo italeta maana).
  Naombeni maoni yetu kuhusu hili.
   
Loading...