Je India ni salama kwa wanafunzi wa Kitanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je India ni salama kwa wanafunzi wa Kitanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RayB, Mar 14, 2010.

 1. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hivi karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio ya kunyanyaswa kibaguzi kwa wanafunzi wa kitanzania huko India. Ni mlolongo wa matukio ya kudhalilisha na ya kinyama kutoka kwa wahindi hawa. Mi najiuliza Is India safe for Tanzanian Students anymore? And what is the reaction of these two countries? Mbona huku kwetu wanatanua tu, na uongozi wanapewa na ufisadi wanafanya? What is a solution?

  Hii ni ya recently:

  TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
  (TASABA
  )

  WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA
  KUUWAWA KWA MOTO BANGALORE -INDIA

  Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 11:30 wanafunzi wawili ,Hamis Mbelwa Fintan mwenye na Olais Alexendra Siarra waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Walinusurika kuuwawa kwa moto baada ya fujo iliyofanywa na wahindi wakidai kuwachukia waAfrika.

  Wahindi hao waliamua kuchukua mafuta ya petrol na kumwaga dirishani na mlangoni, walifanikiwa kuwasha moto kupitia malangoni na moto kuanza kuingia ndani wakati vijana hao wakiwa ndani. Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuuzima moto uliokuwa unaingia ndani na ule wa nje wasamalia wema waliuzima, bahati nzuri petrol ilikuwa chache hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea.

  Nilipopata taarifa hii nilitoka na kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilipouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru.
  Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to cop with them like it or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine.

  Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka kifo cha mwenzetu Imran Mtui ni mwezi tu na siku 7 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio lingine la kuua kwa kutumia petrol.

  Hali hii inatisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha.


  Baada ya kuona hakuna masaada kutoka police niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tunaomba sana msaada toka nyumabani na ofisi zetu za ubalozi zilizopo New-Delhi India kutafuta jinsi ya kufanya waTanzania waishio Bangalore –India na kwingine kote kuishi kwa amani, imezoeleka kuwa mara zote wanafunzi ni wakorofi lakini kwa tukio hili nakataa kabisa kama chanzo ni wahanga hawa bali ni chuki binafsi iliyoko dhidi ya wa Afrika ambayo inatufanya tuishi kwa uoga na wasiwasi mkubwa sana. Leo hii petrol ilikuwa chache siku nyingine itakuaje? Je wangefanikiwa kutoa roho za vijana hawa majibu kutoka vyombo vya dola vya India ingekuwa ni nini? Au wangesema wamejiua tena vijana hawa kwa moto? Haya ni maswali machache ya kujiuliza.


  “Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki wanafunzi wa kiTanzania tuishio Bangalore India”


  Fidelis Msomekela


  Mwenyekiti – TASABA

  +919742176980
   
 2. K

  Kijiweni Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK kashikwa pabaya na wahindi
  Tutamkumbuka Mwalimu Nyerere
   
 3. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wakulaumiwa ni polisi. Lakini haya mambo yanatokea popote ulimwenguni. Baadhi ya wanafunzi wa kihindi nchini Australia waliuawa pia, kama sikosei. Poleni kwa wote wasio na hatia.
   
 4. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Lakini hawa watu wanaendelea kuishi vizuri tu wakiwa huku na kama hawataki wageni kutoka africa kwanini wasiseme tu jamani kuwa watu wasiapply? Hivi wana elimu nzuri sana mpaka watu wanakwenda huko?
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Tukio la kuchoma moto nyumba mijini BANGALORE -INDIA, lina uhusiano gani na Wahindi wanao ishi Tanzania?
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Kwani hamjui wahindi ni wabaguzi tokea enzi hizo nenda kwenye shule zao na hospitali zao utaona unatakiwa ujaze RACE yako,urafiki wa wahindi nasisi wamatumbi upo katika kutuuzia huduma na bidhaa zao,kutunyonya na kutufisadi kwa kutumia wamatumbi wasomi au viongozi,wahindi duniani kote ni watu wa kujitenga,hata ndoa zao ni wao kwa wao,ole wako utoke nje ,wanakutenga na kukususa
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  India sio salama kama ukiwa ni mtu wa kujiexpress! Watu wamesoma huko na wamemaliza masomo yao na kurudi home salama tu. wabongo wengine wakiwa huko wanakuwa ni marimbukeni! Chapombe, matanuzi meeeengi na ujinga mwingi mwiiiiingi! Wengine mpaka wanatia kinyaa! Halafu tabia nyingine mbaya ni wabongo wengi kuishi kama mke na mume!! Wanatoka bongo safiii lakini wakifika huko (India) wanawekana vimada. I feel pitty!
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Huku kwenu wao ndio wameshika nchi yenu. Kama ikiwezekana na sisi tujaribu kushika hiyo ya kwao. Huku kwetu wahindi wako above the law. Kwa hiyo huwezi kulalama.

  Ushauri wangu ni kuwa kaza buti tu. Do not expect sympathy or any assistance from serikali. Unaweza ukawa unajificha na unasoma, ukimaliza rudi zako nyumbani> Uzoefu ni kuwa serikali inaweza kujaribu kuandika barua au kutuma fax au e mail. Lakini usutegemee msaada wowote.
   
 9. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tunajaribu tu kucompare hii race wanavyoishi Bongo na wabongo wanavyoishi huko kwao India
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nilikuwa najiuliza staili ya watu wabongo jinsi wanavyoishi huko manake ujue hatusikii upande wa pili inawezekana nao wanalikoroga sana huko na kuleta utanzania wao.

  Lakini mkuu Pape kuwekana vimada kuna athari gani? Unaweza kukuta wengine wakiishia kuwa pamoja maishani mwao bana
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  India sio salama kama ukiwa ni mtu wa kujiexpress! Watu wamesoma huko na wamemaliza masomo yao na kurudi home salama tu. wabongo wengine wakiwa huko wanakuwa ni marimbukeni! Chapombe, matanuzi meeeengi na ujinga mwingi mwiiiiingi! Wengine mpaka wanatia kinyaa! Halafu tabia nyingine mbaya ni wabongo wengi kuishi kama mke na mume!!
   
 12. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mkuu,
  kila nchi inautaratibu wake. Huko india kama hujaoa/hujaolewa ni mwiko kuwekana kinyumba! Hii tabia wabongo na wakenya wanayo! Inatia kinyaa sana. Vijana wanatoa sana mimba. Usiku wa manane wanafungulia miziki kwa sauti eti wenyewe wanaita 'bashi', hii kitu wahindi hawapendi ndio maana wanafanya revenge mara wakipata loop hole! Kitu kingine ni hawa jamaa zetu kwa kushirikiana na wakenya wanawatapeli sana wahindi wakipata tu kanafasi!
   
 13. p

  pori Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari hii inasikitisha. hawa wahindi wasifanye mambo kama vile wao hawako kwenye nchi za wenzao. kama ni hivyo basi iwe jino kwa jino, yaani na sisi tuwafanyie hivyo hivyo nchini kwetu. kwa nini wao wajifanye wako so superior kuliko binadamu wenzao?
   
 14. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu wewe,
  bongo kuna wahindi vile vile na wanasoma kama watanzania walivyo huko India. Hawa wahindi wa bongo hawana tabia ya ulimbukeni! Wabongo (wengi wao wanaosoma India) ni rimbukeni sana! Wakiacha tabia ya kujiexpress basi haya yote yatakwisha weweeee. Najua wahindi ni wabaguzi lakini wahindi pia ni watu safi sana kama ukijua kujishusha na kuishi kama wao!!
   
 15. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  India wabongo wamejaa kila 'state', sasa wewe jiulize ni kwanini shida/vuguru/matatizo kila siku zitokee Bangalore na Mysore? Hiyo miji miwili inaidadi kubwa ya wanafunzi wa kitanzania! Mambo yanayofanyika huko 'naona aibu kuyaweka hapa jamvini'. Wengine hata wazazi wenu hawajui kama ni nyienyie ndiyo mnayoyafanya huko! Ni aibu! Acheni kuwalaumu wahindi! Wahindi wamechoka kha!
   
 16. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  As thinks stand now mi naona kuna hitilafu na matatizo ndani ya hii jamii ya kitanzania. Ni kweli mimi nilikuwa najiuliza hivi kweli kwanini ni wao tu? Halafu kwanini ni miaka ya hivi karibuni inawezekana kabisa hawa wana matatizo sana. Ok tunajuwa wahindi kwa ubaguzi na unayanyasaji lakini tukichunguza upande wa pili unaweza kuta hawa ndugu zetu nao wana makosa kibao tu
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  At last umehelewa!
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu sema labda hujatembelea India na huijui sisi tunaoijua na mpaka dakika hii tupo tunapambana nao tunajua machungu tuliyo nayo.
   
 19. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tuambie what is the real source? Sio kuwa ninyi ndo mnaharibu huko?
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  wahindi hawana hadhi wanayotaka kujipa. magabachori tu. itafika siku wataiona bongo chungu
   
Loading...