Je, inawezekana ubongo kutolewa kichwani na kufungwa tumboni, kisha ukafanya kazi yake kwa ufanisi kama upo kichwani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,627
154,992
Nasukumwa kuuliza swali hili baada ya kuona hii video ya huyu jamaa anayesema ubongo wake uko tumboni na unafanya kazi kama kawaida.

Tumsikilize Kisha wataalam watupe elimu.

Nasukumwa kuuliza swali hili baada ya kuona hii video ya huyu jamaa anayesema ubongo wake uko tumboni na unafanya kazi maka kawaida.
Tumsikilize Kisha wataalam watupe elimu.

View attachment 1635179
Usahihi ni kwamba kuna kipande cha mfupa wa fuvu (skull-NA SIO UBONGO) kimetolewa kutoka kichwani, na kuhifadhiwa kwenye sehemu ya mbele ya tumbo (anterior abdominal wall-na sio tumboni ndani), ili kisipoteze "uhai" wake kwa mfano blood supply.
Hii hufanyika pale mtu anapopata brain injury na kupelekea ubongo "kuvimba" hivyo kuongeza presha kwenye fuvu; Walichofanya madaktari ni kuondoa kipande cha fuvu ili kuupa nafasi ubongo uweze kutanuka kwa nafasi bila kusababisha madhara, then baada ya muda, ubongo ukishakua vizuri, wanaunganisha tena hicho kipande cha fuvu kilipokua.
Pia, hakuna "communication" yoyote kati ya kipande cha hilo fuvu kilichohifadhiwa kwenye sehemu ya mbele ya tumbo na ubongo, na wala hakuna ubongo wowote kwenye kipande hicho, ni kipande tu cha mfupa.
 
Nimeelewa vizuri sana Sasa, Asante kwa Maelezo na maelekezo mazuri
 
Mheshimiwa ,kwa kuwa video imegoma kufunguka kwa upande wangu,na kwa kuwa nimesoma Hapo juu hoja yako,
Naomba nikujibu Kama ilivyo swali lako
Ndio Mkuu ninaamini hivyo yawezekana Ila ubongo huohuo ukiwa na mabadiliko kadhaa,mfano hapa kwetu mwanasiasa akiwa upinzani anakuwa na uwezo Mkubwa wa hoja na kumpigania mwananchi .Ila akienda upande wa watawala anatumia vizuri ubongo wake ukiwa tumboni,
Asanteni nimewakilisha
 
Haha hahah haaa
 
Back
Top Bottom