Je, inawezekana Rais wa Tanzania akajiuzulu kisheria?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,652
Naomba niulize, kwa mfano Raisi ameona nchi imemshinda hawezi jiuzulu mwenyewe kisheria?

Kwani ni lazima amalize miaka mitano?
Na kwa mfano akijiuzulu nani anakabidhiwa nchi?
Raisi mstaafu wa awamu iliyopita anaweza kupewa nchi kwa muda?

Na kama watanzania tumemchoka hakuna mikakati yoyote iliyopo kisheria ya kumlazimisha Raisi ajiuzulu kisheria na kwa amani?

Kwa mfano kwa kupiga kura za maoni za kumkataa Raisi aliyepo madarakani ili ajiuzulu.!

Mpaka sasa ni Richard Milhous Nixon ambaye alikuwa American politician 37th President of the United States from 1969 until 1974. Huyu alijiuzulu mwenyewe kwa stress na sababu za kisiasa.

Ibara ya 37(5) ya katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania ta mwaka 1977 inasema hivi endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki, KUJIUZULU, Kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yalioelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la MTU atajayekuwa makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitiwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.

Kutokana na nukuu hiyo ya katiba bila shaka Rais anaweza kujiuzulu. Pia kuhusu Rais aliyepita kurudi madarakani hauwezekani pia katiba imesema hivi katika ibara ya 40(2) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 Hakuna MTU atakayechaguliwa zaidi ya Mara mbili kushika kiti cha Rais.
 
1481691562089.png
 
Naomba niulize, kwa mfano Raisi ameona nchi imemshinda hawezi jiuzuru mwenyewe kisheria?

Kwani ni lazima amalize miaka mitano?

Na kwa mfano akijiuzuru nani anakabidhiwa nchi?

Raisi mstafu wa awamu iliyopita anaweza kupewa nchi kwa muda?

Na kama watanzania tumemchoka hakuna mikakati yoyote iliyopo kisheria ya kumlazimisha Raisi ajiuzuru kisheria?

Kwa mfano kwa piga kura za maoni za kumkataa Raisi aliyepo madarakani!

Soma KATIBA
 
Rais akijiuzulu inakabidhiwa na makamu wa rais au wanajeshi kwa muda mfupi adi atakapopatikana atakayeshika kiti hicho
 
Ibara ya 37(5) ya katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 inasema hivi endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki, KUJIUZULU, Kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yalioelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la MTU atajayekuwa makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitiwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.

Kutokana na nukuu hiyo ya katiba bila shaka Rais anaweza kujiuzulu. Pia kuhusu Rais aliyepita kurudi madarakani hauwezekani pia katiba imesema hivi katika ibara ya 40(2) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 Hakuna MTU atakayechaguliwa zaidi ya Mara mbili kushika kiti cha Rais.
 
Ikiwa mngejifunza kutumia vema kura zenu msingalikuwa na mawazo haya hivi sasa. Poleni sana popote mlipo kwazika ahsanteni ndugu
 
Back
Top Bottom