Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,653
Naomba niulize, kwa mfano Raisi ameona nchi imemshinda hawezi jiuzulu mwenyewe kisheria?
Kwani ni lazima amalize miaka mitano?
Na kwa mfano akijiuzulu nani anakabidhiwa nchi?
Raisi mstaafu wa awamu iliyopita anaweza kupewa nchi kwa muda?
Na kama watanzania tumemchoka hakuna mikakati yoyote iliyopo kisheria ya kumlazimisha Raisi ajiuzulu kisheria na kwa amani?
Kwa mfano kwa kupiga kura za maoni za kumkataa Raisi aliyepo madarakani ili ajiuzulu.!
Mpaka sasa ni Richard Milhous Nixon ambaye alikuwa American politician 37th President of the United States from 1969 until 1974. Huyu alijiuzulu mwenyewe kwa stress na sababu za kisiasa.

Ibara ya 37(5) ya katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania ta mwaka 1977 inasema hivi endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki, KUJIUZULU, Kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yalioelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la MTU atajayekuwa makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitiwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.
Kutokana na nukuu hiyo ya katiba bila shaka Rais anaweza kujiuzulu. Pia kuhusu Rais aliyepita kurudi madarakani hauwezekani pia katiba imesema hivi katika ibara ya 40(2) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 Hakuna MTU atakayechaguliwa zaidi ya Mara mbili kushika kiti cha Rais.