Je,inawezekana mkaazisha huusiano wa kimapenzi kwa kupitia cm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je,inawezekana mkaazisha huusiano wa kimapenzi kwa kupitia cm?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by twenty2, Jul 29, 2011.

1. twenty2

twenty2 JF-Expert Member

#1
Jul 29, 2011
Joined: May 20, 2011
Messages: 296
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
watu wengi nikiwauliza kuhusu kujenga huusiano kwenye cm kama inawezekana,wanajibu ndio,je na nyinyi washilika wenzangu mnaionaje?

2. Elia

Elia JF-Expert Member

#2
Jul 29, 2011
Joined: Dec 30, 2009
Messages: 3,442
Likes Received: 3
Trophy Points: 135
Why not mydear? hata kwa wrong number!

3. BADILI TABIA

BADILI TABIA JF-Expert Member

#3
Jul 29, 2011
Joined: Jun 13, 2011
Messages: 30,873
Likes Received: 6,226
Trophy Points: 280
yap yap!

4. A

Ave Ave Maria JF-Expert Member

#4
Jul 30, 2011
Joined: Apr 22, 2011
Messages: 10,757
Likes Received: 34
Trophy Points: 0
Inawezekana lakini inabidi uwe makini sana coz kwenye simu watu wengi huwa wanapretend sana kuwa na characters ambazo si zao. I have a friend of mine ambae alipata boyfriend kupitia kwenye simu. Kabla hajamkubalia alinidokezea kidogo mi nikamwambia amkubalie tu kama rafiki wa kawaida mpaka pale watakapokuja kuonana na kila mtu akaridhika na mwenzake ndo waanzishe huo uhusiano wao. Ye akachagua kutokusubiri coz alikolea kwelikweli. Sasa kimbembe kimetokea pale walipoonana live, mwenzangu jitu si hilo! Yaani pande la baba alafu limemzidi sana kiumri adi mi mwenyewe nilishangaa kwakweli, jinsi alivokuwa anaongea kwenye simu na nilivyomuona ni tofauti kabisa. Zimepita siku mbili rafiki yangu akamtosa huyo jamaa, wee nusura amuue, alimkaba koo huku akisisitiza eti kwanini amempotezea mda kiasi hicho? Ni mengi yaliendelea ila nataka kusema kuwa unapoamua kumdate mtu kwenye simu ni lazima uwe mwangalifu sana kwa sababu unachokitarajia unaweza usikipate. Hivyo vimaneno vitamu vitamu na vivocha visikudanganye!

5. Maayo

Maayo JF-Expert Member

#5
Jul 30, 2011
Joined: Jul 21, 2011
Messages: 319
Likes Received: 0
Trophy Points: 33
Inawezekana. Ila inabidi kuwa makini unaweza kuta ni jambazi at! Mwisho wa siku inakula kwako.

6. Gaga

Gaga JF-Expert Member

#6
Jul 30, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 4,565
Likes Received: 20
Trophy Points: 135
Kuna rafiki yangu alikutana na mumewe kwenyee kukosea namba, aliita taxi, yaani ikachelewa,akatuma msg unanichelewesha Aport,ikaenda kwa mkaka mtanashati, akamwambia pole umekosea namba, ila mie pia naelekea aport, akamuuliza unakaawapi? Msichana akajibu tangi bovu,kijana anakaa tegeta,ndege wanasafiria moja kwenda mwanza, looo wakapitiana, kilichoendelea huko ni historia,wameoana na wana mtoto mmoja, kwa hiyo wakati mwingine huwa ina work out,ila sio nara nyingi,ni golden chance

7. Gagurito

Gagurito JF-Expert Member

#7
Jul 30, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 5,610
Likes Received: 25
Trophy Points: 135

Mkuu hiyo hutokea sana tu! Mimi kuna swaiba yangu mkubwa ana Gf wake ambaye mwanzo wao wa kimapenzi ni kupitia simu! Wamewasiliana kwa miezi 6 pasipo kujuana sura, na mpaka sasa wanaishi vyema!

8. A

Ave Ave Maria JF-Expert Member

#8
Jul 30, 2011
Joined: Apr 22, 2011
Messages: 10,757
Likes Received: 34
Trophy Points: 0

Ni kweli kabisa huwa inatokea watu wanapendana kupitia simu na hatimae wanatengeneza maisha mazuri, kwani huwezi jua mpenzi wako wakweli utakutana nae wapi. Ila sometimes pia ni full magumashi!!

9. Pdidy

Pdidy JF-Expert Member

#9
Jul 30, 2011
Joined: Nov 22, 2007
Messages: 33,457
Likes Received: 5,705
Trophy Points: 280
Samahani kuna neno lakiswahili""koma"" cheki kwenye kamusi
nakupenda sana usifike huko

10. B

Bajabiri JF-Expert Member

#10
Jul 30, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
If it weks its gud

11. Mabagala

Mabagala JF-Expert Member

#11
Jul 30, 2011
Joined: Nov 27, 2009
Messages: 1,465
Likes Received: 42
Trophy Points: 145
Si kwa simu tu hata hapa Jamii Forum waweza pata ndoa

12. Preta

Preta JF-Expert Member

#12
Jul 30, 2011
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 24,113
Likes Received: 3,036
Trophy Points: 280
kabisaaaaaaaaaaa.........nakubaliana na wewe

13. Vin Diesel

Vin Diesel JF Gold Member

#13
Jul 30, 2011
Joined: Mar 1, 2011
Messages: 8,402
Likes Received: 737
Trophy Points: 280
ni pata potea...omba usikutane na kimeo tu.

14. Chimunguru

Chimunguru JF-Expert Member

#14
Jul 30, 2011
Joined: May 3, 2009
Messages: 9,843
Likes Received: 270
Trophy Points: 180
Mwenzenu Mwaka 2000 Shemeji yangu alipewa simu aina ya Ericcson a1018s kama zawadi kwenye harusi, simu ikuwa kubwa flani hivi. Shemeji akaiweka ikawa inatumika kama simu ya pale nyumbani sababu hakupenda kutumia ule MSHINDI. Ikawa ile simu usiku mie nabaki nayo asubuhi inarudi sebuleni. Kuna siku jioni nikakuta miscall km mbili namba siijui! nikaandika sms "mambo" ikajibiwa ya kwanza ya pili...... kumbe walikuwa wanafunzi wa kike wawili, majina yao nayahifadhi, Mmoja Msomali mwingine Mtoto wa Kichaga bana! walikuwa form five wakati huo, tulichat sana usiku tunapigiana simu kila siku usiku tunaongea lkn hatukuweza panga kukutana. wakamaliza form six, Mtoto wa kisomali akaenda kusoma Ulaya, huyu ndo alikuwa mstari wa mbele sana kchat na mimi. alipoondoka ikawa ndo mwisho wa mawasiliano naye. Huyu aliyebaki tukaendelea kuchat naye na baadaye yeye kaingia University of Dar es salaam campus ya Muhimbili. ilikuwa kila asubuhi, mchana, jioni ni Hi!!/mambo hapo sijamtongoza wala nini ni km friend tuu. Mwaka 2002 nikapata kazi!! tukaendelea kuwasiliana naye, tunataniana kila mmoja anamwambia mwenzie mipango yake ya baadaye!! hii iliendelea mpaka 2003 ndo kwa mara ya kwanza tukapanga tukutane!! mitaa ya Posta nikamwona tukaongea sana mtoto alikuwa mzuri rangi ya chocolate, hana makuu!! nikawa namtania Doc mtarajiwa ukiwa doctor ntakuja unichome sindano ya MOYO hahaha

Mwanzoni Kwa kweli sikupenda kumuumiza huyu dada sababu tayari nilikuwa na mtu ambaye alinibana vilivyo, huyu dada ni mstaarabu sana na tuliendelea kuchat kwa sana. mwaka 2004 nikahamia gheto hapa ndo mambo yakaanza kuharibika, huyu mpenzi wangu akawa anakuja kupiga mbonji gheto sometimes a week nzima. Kuna siku nikamtania huyu dada kwa sms kwamba it has been long enough just chatting lets try have a date! ooops she was so excited! hakuamini, the next day akapiga simu km saa moja jioni nipo gheto na huyu mchumba wangu, tukaongea vizuri huku mchumba wangu akisikiliza kwa makini, hatukuongea vitu vibaya kwa kweli, na nikamwambia ukweli kwamba huyu ni rafiki yangu yupo chuoni muhimbili anasoma, kumbe mwenzangu hakupenda akaiba ile namba siku ya pili alipoondoka akampigia yule dada akamtukana sawa sawa! dah kwa kweli iliniuma sana!! alipokuja kuniuliza mbona GF wako ananitukana wakati sina kosa? she was a good friend!! nikamwomba msamaha basi akawa not happy at all!! akawa sasa anapiga muda anajua niko job ananisalimia. Mawasiliano yakawa yanapungua na baadaye akabadilisha na namba kabsaaa!! saasa hivi ni DOc kabsaa na huwa namuona kwenye baadhi ya matangazo ya madaktari wa MEWATA! nahisi sikumtendea jema! lkn ntafanyaje? na nimeshaoa, na nadhani na yeye keshaolewa, basi km yupo JF anisamehe tuu, shughuli za ujana si mchezo, SIMU ILITUKUTANISHA lkn haikuwa Mpango wa mungu!!!!

15. Mwache77

Mwache77 Senior Member

#15
Jul 30, 2011
Joined: Jun 3, 2011
Messages: 175
Likes Received: 45
Trophy Points: 45
Inawezekana,ila inakuwa shida pale mwenzio anapokuwa kapewa namba na m2 anayekujuwa au yeye mwenyewe anakujuwa akatafuta namba yk.Hata kuendesha,tuwe wa angalifu xna

Loading...