Je, inawezekana kwa mwanamke wa mid 20s kuwa hajawahi kabisa kuona siku zake?

Maskini! Mpe pole sana. Bahati mbaya ni kwamba uwezekano wa yeye kubeba ujauzito pia ni mdogo au usiwepo kabisa.

Kwa sasa aendelee kujisogeza kwa Muumba wake.
Ndicho kinachomkosesha amani
 
unakuta ni issue ya kawaida tuu muumba kaamua asimpe hiyo hali bt kila kitu kipo sawa ikiwemo kupata ujauzito etc...mungu anajua zaidi๐Ÿ™Œ
 
Pole yake

Bora ya mie nilipata na ikastop kwa miaka 2,nikaja pata tena,,,hadi leo kupata inakuwa kwa shida sana,

napambana na hili tatizo,mwanzo nilikuwa nachukulia poa
 
yawezekana ni hari ya kawaida tu na isitoshe akisex mara moja tu kwa siku ambazo ni za hatari anapata ujauzito ila siku za ๐Œ๐, ๐ก๐š๐ญ๐จ๐ค๐ฐ๐ข ๐ง๐š ๐๐š๐ฆ๐ฎ ๐ฐ๐š๐ฅ๐š ๐ฆ๐š๐ฎ๐ฆ๐ข๐ฏ๐ฎ ๐ข๐ฅ๐š ๐ฆ๐ณ๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ๐ค๐จ ๐ฐ๐จ๐ญ๐ž ๐ฎ๐ง๐š๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ค๐š ๐ง๐๐š๐ง๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐ง๐๐š๐ง๐ข, ๐ฒ๐š๐š๐ง๐ข ๐ค๐ข๐ญ๐š๐ง๐๐š ๐ค๐ข๐ฅ๐ข๐œ๐ก๐จ ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐Œ๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐ฎ๐ณ๐š๐ณ๐ข ๐ค๐ข๐ง๐š ๐๐š๐ฆ๐ฎ ๐ค๐š๐ฏ๐ฎ ๐š๐ฆ๐›๐š๐ณ๐จ ๐ก๐š๐ณ๐ข๐ฐ๐ž๐ณ๐ข ๐ค๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฆ๐š๐›๐จ๐ง๐ ๐ž ๐ฆ๐š๐›๐จ๐ง๐ ๐ž ๐ฐ๐š๐ฅ๐š ๐ค๐ข๐ฆ๐ข๐ฆ๐ข๐ง๐ข๐ค๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฆ๐š๐š๐ง๐š ๐ฒ๐š ๐ค๐ฐ๐š๐ฆ๐›๐š ๐ƒ๐š๐ฆ๐ฎ ๐œ๐ก๐š๐Ÿ๐ฎ ๐ณ๐ข๐ง๐š๐ข๐ฌ๐ก๐ข๐š ๐ก๐ฎ๐ค๐จ ๐ก๐ฎ๐ค๐จ ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฎ๐ณ๐š๐ณ๐ข,
Nimtazamo wangu tu,
kama anapata hisia basi achukua mzunguko wa siku 28, aanze kujihesabia kisha siku za hatari zikifika afanye sex aone kama atapata mimba
 
Pole yake

Bora ya mie nilipata na ikastop kwa miaka 2,nikaja pata tena,,,hadi leo kupata inakuwa kwa shida sana,

napambana na hili tatizo,mwanzo nilikuwa nachukulia poa
Naomba ni kuulize je kwa yule ambaye damu ya hedhi humtoka bira ratiba maalum shida inakuwa ni nini,
anaweza kuingia leo damu ikikata baada ya siku 4 siku 6 au akitembea umbali mrefu anapata hedhi tena,
๐๐š๐ญ๐š๐ค๐š ๐ง๐ข๐ฆ๐ฌ๐š๐ข๐๐ข๐ž ๐ฆ๐œ๐ก๐ฎ๐ฆ๐›๐š ๐ฐ๐š๐ง๐ ๐ฎ ๐ฆ๐š๐š๐ง๐š ๐ก๐š๐ฉ๐š ๐ค๐ฎ๐ฉ๐š๐ญ๐š ๐ฆ๐ญ๐จ๐ญ๐จ ๐ค๐ฐ๐š๐ค๐ž ๐ข๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ง๐ ๐ฎ๐ฆ๐ฎ
 
Aisee sitoki JF nikipigwa ban nasajili ID nyingine bab...

Mtoa mada leta maviiituuuuzzzz
 
Naomba ni kuulize je kwa yule ambaye damu ya hedhi humtoka bira ratiba maalum shida inakuwa ni nini,
anaweza kuingia leo damu ikikata baada ya siku 4 siku 6 au akitembea umbali mrefu anapata hedhi tena,
๐๐š๐ญ๐š๐ค๐š ๐ง๐ข๐ฆ๐ฌ๐š๐ข๐๐ข๐ž ๐ฆ๐œ๐ก๐ฎ๐ฆ๐›๐š ๐ฐ๐š๐ง๐ ๐ฎ ๐ฆ๐š๐š๐ง๐š ๐ก๐š๐ฉ๐š ๐ค๐ฎ๐ฉ๐š๐ญ๐š ๐ฆ๐ญ๐จ๐ญ๐จ ๐ค๐ฐ๐š๐ค๐ž ๐ข๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ง๐ ๐ฎ๐ฆ๐ฎ
Asee mwenyewe hii shida ilinitokeaga,hadi nikahisi nimerogwa

Nilienda hospital moja hivi ipo vingunguti inaitwa mtakuja,kuna dr pale wa mnazi mmoja anaitwa dr phio,ndiye aliyenisaidia kuna vidonge alinipa,

Ilikuwa mwaka 2016,sijatokewa tena na hiyo hali hadi leo

Kiukweli kupata ujauzito ni ngumu asee,
 
Habari za wakati huu wanajukwaa, natumai Weekend yenu imeanza poa.

Moja kwa moja kwenye mada swali langu ni, je ni kitu cha kawaida mwanamke aliyeko kwenye mid 20s kuwa hajawahi kabisa kuona siku zake tangu abalehe?

Nina rafiki yangu yeye hajawahi kabisa kuexperience menstrual periods tangu abelehe kwa maana kwamba hajawahi kabisa 'kuvunja ungo', wanasema ni ugonjwa ambao kitaalam unaitwa Amenorrhea. Kwa kawaida inajulikana umri wa msichana kuvunja ungo kwa kizazi cha siku hizi, ni kuanzia miaka 10 hadi 18.

Lakini yeye hadi umri huu akiwa kwenye mid 20s, bado hajapitia hiyo stage. Alipofika miaka 14 alianza kuona mabadiliko kwenye mwili wake ambayo ni mabadiliko ya kawaida yale ambayo msichana yoyote anayaona akiwa anabalehe, isipokuwa hilo tu la kuona siku zake.

Alipojaribu kumuelezea mama yake na baadhi ya waalimu wake wa kike wakamuambia kuwa ni kawaida, wanawake wanatofautiana. Wengine wanaenda hadi miaka 18, hata kama kuna mabadiliko mengine walianza kuyaona kabla ya umri huo.

Akaona siyo kesi life likaendelea ila alipofikisha miaka 18 bado akaendelea kuona kimya, ndipo wasiwasi zaidi ukaongezeka na wanaomzunguka kuanza kulichukulia tatizo lake serious. Amejaribu kuenda mahospitalini na kuonana na madaktari bingwa mbalimbali wa wanawake, na kufanya vipimo mbalimbali kuona kama kuna tatizo lolote.

Kila kitu kiko normal maumbile ni mwanamke kabisa aliyekamilika kizazi kipo na hakina shida yoyote, ila ndiyo hivyo tu hajawahi kuexperience hiyo hali! Aliambiwa shida inaweza kuwa ni hormonal imbalances kwamba atakuwa na low oestrogen levels au high testosterone levels, na alishajaribu kuanzishiwa hormone therapy lakini wapi!

Amezunguka makanisani kuombewa, ikidhaniwa pengine ni tatizo la kiroho au amerogwa lakini wapi. Amejaribu kutumia dawa mbalimbali za mitishamba ila hazijamsaidia kitu, hadi mwisho wa siku amekata tamaa na kuendelea kujipa moyo kuwa pengine siku yoyote tu isiyo na jina atapata.

Mwanzo alikuwa anaogopa kuwasimulia watu kuhusu tatizo lake hasa wenzie aliosoma nao boarding, ambao wengine walikuwa wakimuuliza kuwa mbona mwenzetu hatujawahi kuona ukihangaika na hizi sanitary pads hata kwa bahati mbaya. Akawa anazuga tu kuwa yeye kuna miezi anapata na kuna miezi hapati, hivyo ikawa inamlazimu siku nyingine awe anavaa pads kama geresha tu ili wenzie wasihisi kama ana hilo tatizo.

Sasa ndiyo nimelileta hili kwenu wadau kwa niaba yake kutaka kujua kama ni kitu cha kawaida kwamba je kuna wanawake wengi wenye umri huo au zaidi ambao wana huo ugonjwa, au kama kuna mtu anamfahamu mwanamke mwenye huo ugonjwa. Na kama kuna njia nyingine za matibabu (kasoro kwa waganga tu) tofauti na hizo alizozipitia yeye ambazo zinaweza zikamsaidia, basi wajuvi wengine mnaweza kushare hapa tujue namna ya kumsaidia maana inazidi kumpa stress na kumkosesha amani kadiri miaka inavyozidi kuenda.

Mods nisaidieni kuedit kichwa cha uzi kwa kadiri mtakavyoona inafaa. Ila nilitaka kuuliza kama ni kitu cha kawaida na pia kujua msaada mwingine zaidi wa hilo tatizo.

Jibu ni inawezekana.

Hali hii huitwa primary Amenorrhea (binti/dada/ ambaye amefikia umri taraji kupata mzunguko wa hedhi, lakini hajawahi kupata hata mara moja).

Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha suala husika, ili kuweza kusema nani anahusishwa na sababu ipi, ni pale historia ya muhusika, examination/ukaguzi wa mwili na vipimo huweza kufanyika.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa hili si suala la kwenda siku moja kwa daktari na kupata jibu, bali yaweza kuhitaji ufuatiliaji wa karibu. Kwani hili laweza kuhitaji kwenda ngazi kwa ngazi mpaka kuufikia mwafaka. Na hapa ndo waweza kuhitaji mtoa huduma mtulivu na asiyesukumwa na faida binafsi.
Pia, mpangilio mzuri wa nini kianze na kipi kisubiri kwa uwiano wa gharama na kutokuwa na madhira kwa mwili.

Kutokana na hali halisi nitataja mambo yanayohusishwa na suala hili:

1: Unaweza kufanya vipimo vyote na kukuta hakuna sababu au usipate sababu ya chanzo cha utofauti huu.

2: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.
Hii ni pale ambapo, kabla ya kupata siku zake, muhusika aliweza kutibiwa kwa dawa husika zikilenga kutatua tatizo tofauti na masuala ya uzazi.

3: Lishe duni
Ukamilifu wa mwili hutegemea na kupewa viinilishe vya kutosha ili kutengeneza vichocheo husika na kuweka mwili kwenye mpangilio timilifu.

4: Uzito uliopitiliza
Hii hupelekea mifumo ya mwili baadhi kutokufanya vyema. Mfano: vichocheo vya estrogen kupata ukinzani na kutokufanya kazi yake vyema.

5: Uzito mdogo kupitiliza
Hili huendana pia na kutokuwa na lishe njema na hivyo kupelekea sababu namba tatu hapo juu.

6: Stress/wasiwasi uliopitiliza
Husababisha utoaji wa vichocheo hasi, ambavyo huleta ukinzani kwa vichocheo vingine mwilini. Pia, vichocheo vya aina hii hubomoa zaidi mwili kuliko kuujenga

7: Mazoezi /kazi ngumu
Yote haya huanzisha stress kwenye mwili na kusababisha mwili kujongea kwenye mfumo wa kimazoezi zaidi kuliko kwenye mfumo wa uzazi.

8: Matatizo ya ulaji
Haya ni matatizo ya afya ya akili au ukosefu wa viinilishe ambayo hupelekea mtu kula vitu ambavyo si vya kawaida kwa binadamu. Matatizo kama haya hupelekea tatizo kama lilivyotajwa namba tatu hapo juu.

9: Matatizo ya afya ya akili na dawa zake
Ulaji kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili mara nyingi si mzuri, pia dawa zinazotumika kurejesha mifumo hii sawa huweza kuingilia utaratibu wa kawaida wa mwili kuandaa hedhi.

10: Matatizo ya ovari (polycystic ovarian syndrome).
Haya ni matatizo ya maumbile kwenye ovari, lakini pia huambatana na mabadiliko kwenye mifumo ya homoni na mapokeo yake ndani ya mwili.

11: Kukoma kikazi kwa ovari kabla ya muda wake taraji kufika.
Kwa kawaida hali hii hutakiwa kuonekana kwa wamama kuanzia miaka 40, lakini kwa sababu moja au nyingine huweza kumtokea mama/dada yeyote katika umri wowote.

12: Turner syndrome
Tatizo la kijenetiki ambalo husababisha ovari kutokukua vyema na hivyo kuathiri utendaji wake.

13: Uvimbe kwenye tezi la pituitary
Hili likiwa muhimili wa mifumo ya uzazi, uwepo wa uvimbe huweza kusababisha matatizo kwenye uwezo wa utoaji wa vichocheo/homoni na utendaji kazi wake.

14: Tatizo la kimaumbile kwenye njia/viungo vya uzazi.
Hii huusisha:
-ngozi inayofunga njia ya uzazi/bikra kuwa ngumu na hivyo kutokutoka kwa wakati.
-ngozi inayogawa mji wa mimba katika vipande viwili, juu na chini.
-kufunga au wembamba uliopitiliza wa mlango wa uzazi.
-ukosefu wa mji wa mimba au njia ya uzazi/uke
 
Habari za wakati huu wanajukwaa, natumai Weekend yenu imeanza poa.

Moja kwa moja kwenye mada swali langu ni, je ni kitu cha kawaida mwanamke aliyeko kwenye mid 20s kuwa hajawahi kabisa kuona siku zake tangu abalehe?

Nina rafiki yangu yeye hajawahi kabisa kuexperience menstrual periods tangu abelehe kwa maana kwamba hajawahi kabisa 'kuvunja ungo', wanasema ni ugonjwa ambao kitaalam unaitwa Amenorrhea. Kwa kawaida inajulikana umri wa msichana kuvunja ungo kwa kizazi cha siku hizi, ni kuanzia miaka 10 hadi 18.

Lakini yeye hadi umri huu akiwa kwenye mid 20s, bado hajapitia hiyo stage. Alipofika miaka 14 alianza kuona mabadiliko kwenye mwili wake ambayo ni mabadiliko ya kawaida yale ambayo msichana yoyote anayaona akiwa anabalehe, isipokuwa hilo tu la kuona siku zake.

Alipojaribu kumuelezea mama yake na baadhi ya waalimu wake wa kike wakamuambia kuwa ni kawaida, wanawake wanatofautiana. Wengine wanaenda hadi miaka 18, hata kama kuna mabadiliko mengine walianza kuyaona kabla ya umri huo.

Akaona siyo kesi life likaendelea ila alipofikisha miaka 18 bado akaendelea kuona kimya, ndipo wasiwasi zaidi ukaongezeka na wanaomzunguka kuanza kulichukulia tatizo lake serious. Amejaribu kuenda mahospitalini na kuonana na madaktari bingwa mbalimbali wa wanawake, na kufanya vipimo mbalimbali kuona kama kuna tatizo lolote.

Kila kitu kiko normal maumbile ni mwanamke kabisa aliyekamilika kizazi kipo na hakina shida yoyote, ila ndiyo hivyo tu hajawahi kuexperience hiyo hali! Aliambiwa shida inaweza kuwa ni hormonal imbalances kwamba atakuwa na low oestrogen levels au high testosterone levels, na alishajaribu kuanzishiwa hormone therapy lakini wapi!

Amezunguka makanisani kuombewa, ikidhaniwa pengine ni tatizo la kiroho au amerogwa lakini wapi. Amejaribu kutumia dawa mbalimbali za mitishamba ila hazijamsaidia kitu, hadi mwisho wa siku amekata tamaa na kuendelea kujipa moyo kuwa pengine siku yoyote tu isiyo na jina atapata.

Mwanzo alikuwa anaogopa kuwasimulia watu kuhusu tatizo lake hasa wenzie aliosoma nao boarding, ambao wengine walikuwa wakimuuliza kuwa mbona mwenzetu hatujawahi kuona ukihangaika na hizi sanitary pads hata kwa bahati mbaya. Akawa anazuga tu kuwa yeye kuna miezi anapata na kuna miezi hapati, hivyo ikawa inamlazimu siku nyingine awe anavaa pads kama geresha tu ili wenzie wasihisi kama ana hilo tatizo.

Sasa ndiyo nimelileta hili kwenu wadau kwa niaba yake kutaka kujua kama ni kitu cha kawaida kwamba je kuna wanawake wengi wenye umri huo au zaidi ambao wana huo ugonjwa, au kama kuna mtu anamfahamu mwanamke mwenye huo ugonjwa. Na kama kuna njia nyingine za matibabu (kasoro kwa waganga tu) tofauti na hizo alizozipitia yeye ambazo zinaweza zikamsaidia, basi wajuvi wengine mnaweza kushare hapa tujue namna ya kumsaidia maana inazidi kumpa stress na kumkosesha amani kadiri miaka inavyozidi kuenda.

Mods nisaidieni kuedit kichwa cha uzi kwa kadiri mtakavyoona inafaa. Ila nilitaka kuuliza kama ni kitu cha kawaida na pia kujua msaada mwingine zaidi wa hilo tatizo.
Ajaribu kushika ujauzito Kama itawawezekana. Ajaribu tuu
 
Pole sana kwake .
Je anapata dalili nyingine za ovulation kama
Ongezeko la joto
Mabadiliko katika ute
Joto la mwili kuongezeka
Maumivu katika kiuno Etc
 
Pole yake

Bora ya mie nilipata na ikastop kwa miaka 2,nikaja pata tena,,,hadi leo kupata inakuwa kwa shida sana,

napambana na hili tatizo,mwanzo nilikuwa nachukulia poa
Pole sana asee
 
Back
Top Bottom