Je, inawezekana kwa mwanamke wa mid 20s kuwa hajawahi kabisa kuona siku zake?

Jibu ni inawezekana.

Hali hii huitwa primary Amenorrhea (binti/dada/ ambaye amefikia umri taraji kupata mzunguko wa hedhi, lakini hajawahi kupata hata mara moja).

Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha suala husika, ili kuweza kusema nani anahusishwa na sababu ipi, ni pale historia ya muhusika, examination/ukaguzi wa mwili na vipimo huweza kufanyika.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa hili si suala la kwenda siku moja kwa daktari na kupata jibu, bali yaweza kuhitaji ufuatiliaji wa karibu. Kwani hili laweza kuhitaji kwenda ngazi kwa ngazi mpaka kuufikia mwafaka. Na hapa ndo waweza kuhitaji mtoa huduma mtulivu na asiyesukumwa na faida binafsi.
Pia, mpangilio mzuri wa nini kianze na kipi kisubiri kwa uwiano wa gharama na kutokuwa na madhira kwa mwili.

Kutokana na hali halisi nitataja mambo yanayohusishwa na suala hili:

1: Unaweza kufanya vipimo vyote na kukuta hakuna sababu au usipate sababu ya chanzo cha utofauti huu.

2: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.
Hii ni pale ambapo, kabla ya kupata siku zake, muhusika aliweza kutibiwa kwa dawa husika zikilenga kutatua tatizo tofauti na masuala ya uzazi.

3: Lishe duni
Ukamilifu wa mwili hutegemea na kupewa viinilishe vya kutosha ili kutengeneza vichocheo husika na kuweka mwili kwenye mpangilio timilifu.

4: Uzito uliopitiliza
Hii hupelekea mifumo ya mwili baadhi kutokufanya vyema. Mfano: vichocheo vya estrogen kupata ukinzani na kutokufanya kazi yake vyema.

5: Uzito mdogo kupitiliza
Hili huendana pia na kutokuwa na lishe njema na hivyo kupelekea sababu namba tatu hapo juu.

6: Stress/wasiwasi uliopitiliza
Husababisha utoaji wa vichocheo hasi, ambavyo huleta ukinzani kwa vichocheo vingine mwilini. Pia, vichocheo vya aina hii hubomoa zaidi mwili kuliko kuujenga

7: Mazoezi /kazi ngumu
Yote haya huanzisha stress kwenye mwili na kusababisha mwili kujongea kwenye mfumo wa kimazoezi zaidi kuliko kwenye mfumo wa uzazi.

8: Matatizo ya ulaji
Haya ni matatizo ya afya ya akili au ukosefu wa viinilishe ambayo hupelekea mtu kula vitu ambavyo si vya kawaida kwa binadamu. Matatizo kama haya hupelekea tatizo kama lilivyotajwa namba tatu hapo juu.

9: Matatizo ya afya ya akili na dawa zake
Ulaji kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili mara nyingi si mzuri, pia dawa zinazotumika kurejesha mifumo hii sawa huweza kuingilia utaratibu wa kawaida wa mwili kuandaa hedhi.

10: Matatizo ya ovari (polycystic ovarian syndrome).
Haya ni matatizo ya maumbile kwenye ovari, lakini pia huambatana na mabadiliko kwenye mifumo ya homoni na mapokeo yake ndani ya mwili.

11: Kukoma kikazi kwa ovari kabla ya muda wake taraji kufika.
Kwa kawaida hali hii hutakiwa kuonekana kwa wamama kuanzia miaka 40, lakini kwa sababu moja au nyingine huweza kumtokea mama/dada yeyote katika umri wowote.

12: Turner syndrome
Tatizo la kijenetiki ambalo husababisha ovari kutokukua vyema na hivyo kuathiri utendaji wake.

13: Uvimbe kwenye tezi la pituitary
Hili likiwa muhimili wa mifumo ya uzazi, uwepo wa uvimbe huweza kusababisha matatizo kwenye uwezo wa utoaji wa vichocheo/homoni na utendaji kazi wake.

14: Tatizo la kimaumbile kwenye njia/viungo vya uzazi.
Hii huusisha:
-ngozi inayofunga njia ya uzazi/bikra kuwa ngumu na hivyo kutokutoka kwa wakati.
-ngozi inayogawa mji wa mimba katika vipande viwili, juu na chini.
-kufunga au wembamba uliopitiliza wa mlango wa uzazi.
-ukosefu wa mji wa mimba au njia ya uzazi/uke
Shukrani sana mkuu
 
Back
Top Bottom