Je, inawezekana kwa Mwalimu kumuwekea dhamana mtuhumiwa dhidi ya mwanafunzi kwa kesi ya mapenzi

Mwailongola

Member
Nov 29, 2018
29
38
Habari wana JF,

Naomba msaada wa kisheria kuhusu dhamana. Kuna mtu kakamatwa kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi. Katika mashariti ya dhamana ni kwamba anatakiwa awe na wadhamini wawili watumishi, sasa swali langu; Je, mwalimu anaweza kumuwekea dhamama mtu kama huyo?

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muacheni tu huko kama ni mtu mzima. Kufanya mapenzi na mwanafunzi sio tabia nzuri ukiwa mtu mzima wa miaka kuanzia 30.
 
Mwailongola, Salama mkuu,

Tambua kuwa mtuhumiwa ana haki nyingine zote mbali na haki zizuiliwazo kulingana na makosa ya wakati hio.

Mwalimu kwa jina lake mfano "John" anaweza kumwekea dhamana mtuhumiwa.

Nielewavyo mimi, dhamana huwa haiwekwi kwa kutumia wadhifa wa mtu "mwalimu" isipokuwa ni mtu kwa jina lake kwanza, wadhifa unafuatia baadaye.

Hata mfano mdhaminiwa akiruka dhamana basi atakayetafutwa ni "john" na sio "mwalimu".

Kwa kifupi ni hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom