Je inawezekana kutenganisha dini na siasa?

Boko haram

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
3,253
1,229
Kuna kauli zinazozungumzwa kila siku kwamba watu wanatakiwa kutenganisha dini na siasa na ugomvi mkubwa kati ya kikundi cha uamsho na serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni suala la kutenganisha dini na siasa, katika mihadhara ya uamsho sheikh farid alisema kwa mujibu wa dini ya uislamu huwezi kutenganisha kati ya dini na siasa kwasababu dini ya uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya binadamu ;1 kwamfano masuala ya hukumu mwizi anapoiba hukumu yake nini nini 2 masuala ya mirathi 3 masuala ya biashara na hata mitume wote walitumwa kwa wafalme ambao kwasasa ni kama unavyowazungumzia maraisi hata suleiman alikua nabii na mfalme kwahiyo na yeye alichanganya dini na siasa?
 
Hii thread yako ya kipumbavu Hebu ipeleke radio Imaam na kwenye lile gazeti lenu la Al-queda ohoooo!!!!! Nimekosea Al-Nuur
 
Mkuu Boko haram .....kwa majibu rahisi kwa mazingira tuliyonayo ninadhani ni vigumu vitu hivi kuvichanganya....tuna dini mbalimbali ambazo tuliletewa na wageni.....wengi wetu zimetukuta kama ajali tu....hatujui tuliingiaje....tumerithishwa huku walioamua kuingia kwenye dini hizo (wazee wetu) waliamua kwa sababu zao tusizo zijua kama ulimbukeni...kupata ahueni ya maisha...kuoa/kuolewa nk...Ndiyo maana tukajiwekea uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria tulizojiwekea......sasa kama tunataka tukopi mifumo ya wengine wenye mazingira halisi tofauti na yetu tujaribu kuitumia naamini tutaishia kujichanganya tuu.....mifano iko lukuki
 
Hii thread yako ya kipumbavu Hebu ipeleke radio Imaam na kwenye lile gazeti lenu la Al-queda ohoooo!!!!! Nimekosea Al-Nuur
Hapa sijazungumza kuhusu radio imaan hayo ni mawazo yako mgando jibu hoja wacha ushabiki wa CCM na CHADEMA
 
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha. Ukristo ni mfumo kamili wa maisha. Uhindu ni mfumo kamili wa maisha. Upagani ni mfumo kamili wa maisha. JE! TUFUATE UPI NA TUACHE UPI Boko Haram?. Nashauri kwa wasioridhika na mfumo wa maisha uliopo wahamie huko kwenye nchi zilikotoka dini zao(Madina/Maka au Vatican/Yerusalem).
 
Maneno hayo hutumiwa na wanasiasa interchangeably na kwa matakwa yao kutegemeana na wakati na matukio ya kipindi husika. Kwanza, which is which. Kuchanganya siasa na dini ndiyo tatizo au kuchanganya dini na siasa? Mfano, Kuna padre aliwahi kusema J K ni chaguo la Mungu na serikali haikusema padre amechanganya dini na siasa. Lakini maaskofu walipoonyesha kumtetea Slaa wakati wa uchaguzi 2010 wakasema maaskofu wanaanza kuchanganya dini na siasa. Dhana ya kuchanganya dini na siasa inatumiwa vibaya na tabaka la watawala.

Nyerere alijaribu kutenganisha siasa na dini kwa nia njema tu kuondoa migongano ya kimaslahi na kimoja kunyang'anya nafasi ya kingine. Tujadilikuali!
 
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha. Ukristo ni mfumo kamili wa maisha. Uhindu ni mfumo kamili wa maisha. Upagani ni mfumo kamili wa maisha. JE! TUFUATE UPI NA TUACHE UPI Boko Haram?. Nashauri kwa wasioridhika na mfumo wa maisha uliopo wahamie huko kwenye nchi zilikotoka dini zao(Madina/Maka au Vatican/Yerusalem).

Natumia simu......hesabu hii nimeipenda
 
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha. Ukristo ni mfumo kamili wa maisha. Uhindu ni mfumo kamili wa maisha. Upagani ni mfumo kamili wa maisha. JE! TUFUATE UPI NA TUACHE UPI Boko Haram?. Nashauri kwa wasioridhika na mfumo wa maisha uliopo wahamie huko kwenye nchi zilikotoka dini zao(Madina/Maka au Vatican/Yerusalem).
Mkuu hapa ninamaanisha Zanzibar kwasababu tunaambiwa waislamu ni asilimia 98 je inashindikana na hatakama itakuwa inatumia sheria za dini wakristo watakuwa na haki zao za kuishi bila kubugudhiwa kama ilivyo Saudi arabia
 
Back
Top Bottom