Je, inawezekana kulipa kodi ya ardhi ya Serikali kwa awamu?

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,793
33,164
Ninaomba msaada kujua, kuna ndugu yangu yupo masomoni ughaibuni, yapata mwaka wa sita hajalipa land rent ya Serikali kwa viwanja vyake vitatu, angependa kulipa ila kwa awamu,
  1. Je, serikali ina utaratibu huo?
  2. Kama upo, procedures ni zipi?
Nawasilisha
 
Nenda ofisi ya mipango miji,viwanja au shamba lilipo.Nimewahi kuona mama mmoja,toka baba afariki ni muda mrefu,hajalipa,walimkubalia kwa awamu.
 
Atakuwa na fine nyingi tu kwa kuchelewa kulipa kwa viwanja vitatu kwa hiyo miaka sita. Na sasa tayari land rent ni ya 2021-2022. Kwa kuwa kiasi anachodaiwa kitakuwa kikubwa kidogo, nadhani ataruhusiwa kulipa kwa awamu akienda ofisi ya mipango jiji mahali viwanja vyake vipo. Imewakuta wengine, na wakaruhusiwa kwa awamu mbili au hata tatu wakamilishe
 
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom