Je, inaruhusiwa kisheria kuanzisha chama 'kipya' cha TANU?

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Messages
5,491
Likes
195
Points
160

Companero

Platinum Member
Joined Jul 12, 2008
5,491 195 160
Wanasiasa na Wanasheria, je, inawezekana kuanzisha chama 'kipya' cha kisiasa cha upinzani kiitwacho Jumuiya ya Uzalendo wa Kiafrika, yaani, Tanzania African National Union (TANU)?
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
7,344
Likes
1,151
Points
280

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
7,344 1,151 280
Wanasiasa na Wanasheria, je, inawezekana kuanzisha chama 'kipya' cha kisiasa cha upinzani kiitwacho Jumuiya ya Uzalendo wa Kiafrika, yaani, Tanzania African National Union (TANU)?
Sina uhakika lakini nadhani hairuhusiwi kwa sababu TANU yako itakuwa ni sawa na TANU iliyomo ndani ya CCM kama muungano na ASP, kwa hiyo TANU nyingine itakuwa ni sawa na kuweka CCM mbili ingawa TANU yako inatumia Tanzania wakati TANU ya CCM inatumia Tanganyika. Hata hivyo nadhani si vibaya kuanzisha chama kinachoitwa "Tanzania Nationals Union" na kukipa kifupi cha TaNU.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,820
Likes
333
Points
180

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,820 333 180
Kilichokuwepo kilikuwa TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION, na unachotaka kuanzisha ni TANZANIA AFRICAN NATIONAL UNION. Hayo ni majina mawili tofauti na hakuna utata wowote wa kuanzisha. Hila usitembeze bakuri tu.
 
Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
25,780
Likes
24,388
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
25,780 24,388 280
Sheria ya vyama vya siasa iko wazi kuhusu holo, sio tuu hairuhusiwa kuanzisha chama chenye jina la vyama vya zamani, hairuhusiwi hata kuanzisha chama chenye jina linalofanania. yaani kama TANU ilikuwa Tanganyika Africa National Union, hairuhusiwi hata kuanzisha Taa Angazia Njia Umoja-TANU, hakitasajiliwa.

12. –(1) No party formed or existing in any part the United Republic prior to
the Union of Tanganyika and Zanzibar or prior to 5​
th February, 1977, shall be
revived nor shall the name or acronym of such party be used by any political
party to be registered under this Act.

Joined
Jan 9, 2010
Messages
71
Likes
2
Points
0

American lady

Member
Joined Jan 9, 2010
71 2 0
Chama ni chama tu mzee.Tunachohitaji kutoka kwa watu wenye hicho chama, ni ufanisi tu.siyo chama ndicho kinafanya ufisadi wa kula pesa za watu bali ni watu.chama ni jina tu upo hapo ?kazi kwako mzee piga debe uwezavyo.
 
Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,197
Likes
260
Points
180

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,197 260 180
no........
hairuhusiwi kisheria...
Na Je badala ya kukiita Tanganika kikaitwa Tanzania African Union au kikaitwa kwa Lugha ya kiswahili maana sijui kama katiba ya TANU ilifafanua jina la TANU kwa kiswahili-Jumuiya ya Uzalendo wa Kiafrika?
 
Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
25,780
Likes
24,388
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
25,780 24,388 280
Na Je badala ya kukiita Tanganika kikaitwa Tanzania African Union au kikaitwa kwa Lugha ya kiswahili maana sijui kama katiba ya TANU ilifafanua jina la TANU kwa kiswahili-Jumuiya ya Uzalendo wa Kiafrika?
12. –(1) No party formed or existing in any part the United Republic prior tothe Union of Tanganyika and Zanzibar or prior to 5th February, 1977, shall berevived nor shall the name or acronym of such party be used by any politicalparty to be registered under this Act.Hivi ndivyo sheria inavyosema, sio jina tuu, hata acronym TANU/ ASP etc, hairuhusiwi ni kinyume cha sheria.
 
John Mnyika

Verified User
Joined
Jun 16, 2006
Messages
715
Likes
23
Points
0
Age
37

John Mnyika

Verified User
Joined Jun 16, 2006
715 23 0
Sheria ya vyama vya siasa iko wazi kuhusu holo, sio tuu hairuhusiwa kuanzisha chama chenye jina la vyama vya zamani, hairuhusiwi hata kuanzisha chama chenye jina linalofanania. yaani kama TANU ilikuwa Tanganyika Africa National Union, hairuhusiwi hata kuanzisha Taa Angazia Njia Umoja-TANU, hakitasajiliwa.

12. –(1) No party formed or existing in any part the United Republic prior to
the Union of Tanganyika and Zanzibar or prior to 5th February, 1977, shall be
revived nor shall the name or acronym of such party be used by any political
party to be registered under this Act.
Pasco

Asante sana. Naamini hapa umenukuu sheria ya zamani ya vyama vya siasa. Hii wording tuliipigia kelele sana iondolewe katika Muswada wa Sheria mpya ya vyama vya siasa. Sijui hatma yake ilikuwaje, maana toka ipitishwe na bunge na kupelekwa kwa Rais kusainiwa kuwa sheria sijawahi kuiona tena sheria mpya.

Nakumbuka wakati huo pia kulikuwa na ubishani kuhusu namna sheria inavyobana vyama vya siasa kuungana! Kwamba vyama vikiungana viongozi wote wa kuchaguliwa wa ndani ya vyama hivyo na hata wa kiserikali kama rais, wabunge, madiwani, viongozi wa mitaa, vijiji nk wote wanapoteza nafasi zao na uchaguzi unawajibika kurudiwa kuziba nafasi hizo

JJ
 
mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Messages
3,845
Likes
627
Points
280

mayenga

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2009
3,845 627 280
hatari tupu,nadhani la msingi tafut jina jingine uje na sera nzuri,ruzuku itakuwa halali yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Messages
3,845
Likes
627
Points
280

mayenga

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2009
3,845 627 280
Pasco

Asante sana. Naamini hapa umenukuu sheria ya zamani ya vyama vya siasa. Hii wording tuliipigia kelele sana iondolewe katika Muswada wa Sheria mpya ya vyama vya siasa. Sijui hatma yake ilikuwaje, maana toka ipitishwe na bunge na kupelekwa kwa Rais kusainiwa kuwa sheria sijawahi kuiona tena sheria mpya.

Nakumbuka wakati huo pia kulikuwa na ubishani kuhusu namna sheria inavyobana vyama vya siasa kuungana! Kwamba vyama vikiungana viongozi wote wa kuchaguliwa wa ndani ya vyama hivyo na hata wa kiserikali kama rais, wabunge, madiwani, viongozi wa mitaa, vijiji nk wote wanapoteza nafasi zao na uchaguzi unawajibika kurudiwa kuziba nafasi hizo

JJ

MNyika fuatilia hili utupe majibu yenye kueleweka,kwa sababu inaonekana hujui harakati zenu ziliishia wapi kuhusu hili.
 
Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,197
Likes
260
Points
180

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,197 260 180
12. –(1) No party formed or existing in any part the United Republic prior tothe Union of Tanganyika and Zanzibar or prior to 5th February, 1977, shall berevived nor shall the name or acronym of such party be used by any politicalparty to be registered under this Act.Hivi ndivyo sheria inavyosema, sio jina tuu, hata acronym TANU/ ASP etc, hairuhusiwi ni kinyume cha sheria.
Pasco, do you think wazanzibar wanaiheshimu sheria hii, maana kukitokea kugombania vyeo ktk smz (subiri mchakato wa mrithi wa karume usikie)utasikia habari za kutaka kufufua ASP, ZPPP, HIZB etc....na Je ikiwa upande mmoja wa bara usipoiheshimu sheria hii, automatically kwa upande mwingine nako sheria hii inakuwa dead?
 
Forum statistics

Threads 1,190,668
Members 451,284
Posts 27,679,920