Je, inaruhusiwa askari polisi wa kiume kuwa na rasta?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,713
45,096
Nimemuona askari huyu wa mkoani Kigoma akiwa na rasta kabisa, je taratibu za jeshi la polisi zimebadilika siku hizi? Maana zamani hata ndevu walikuwa hawaruhusiwi

IMG_1497.JPG
 
Hao ni kikosi cha CID hawavai uniform ili wajichanganye na raia kirahisi kupata habari za intelijensia. Lakini siku hizi ni vurugu tupu maana wanashiriki matukio kama haya wakiwa na silaha na kujionyesha waziwazi. Hata lengo la kufanya wasivae uniform limepotea, maana hawa ndio wanatakiwa kutumiwa kama "undercover police" na pengine hata kujifanya ni wahalifu ili kukamata wahalifu.

Niliwahi kusema katika tukio la ujambazi wakiwa na silaha namna hii wanaweza kuuwawa na raia wakidhaniwa ndio majambazi. Lakini polisi wetu uwezo wao wa kufikiri si mkubwa kiasi hicho. Siku hizi mambo yanafanyika kienyeji sana, hasa Polisi. Utii kwa chama tawala umewaharibu sana, maana sasa wanasiasa ndio wanaongoza jeshi la polisi na kulipa amri za oparesheni. Polisi wana spend muda wao mwingi ku monitor twita account za wanasiasa na magazeti ili kujua viongozi wa CCM wamesema nini dhidi ya upinzani wakatekeleze haraka, na wanasahau hata kuangalia ukiukwaji wa taratibu za kipolisi. IGP anatia sana aibu.

Angalia hii thread

IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia? - JamiiForums
 
Wanaruhusiwa ila ndevu bado hawaruhusu.. . Naona washakjai kibao hawana ndevu ila madem wana rasta
 
Mtoa mada anazungumzia , Upande wa wanaume kuwa na Rasta
Wanaume wengi ni wapelelezi aka askari kanzu...hata wanawake wengi wapo kisela au kawaida kumbe ni police..... Kwenye operation ndo utawakuta na silaha kabisa... Ila kawaida wanakua hawana silaha ila wapo kazin
 
Hao ni kikosi cha CID hawavai uniform ili wajichanganye na raia kirahisi kupata habari za intelijensia. Lakini siku hizi ni vurugu tupu maana wanashiriki matukio kama haya wakiwa na silaha na kujionyesha waziwazi. Hata lengo la kufanya wasivae uniform limepotea, maana hawa ndio wanatakiwa kutumiwa kama "undercover police" na pengine hata kujifanya ni wahalifu ili kukamata wahalifu.

Niliwahi kusema katika tukio la ujambazi wakiwa na silaha namna hii wanaweza kuuwawa na raia wakidhaniwa ndio majambazi. Lakini polisi wetu uwezo wao wa kufikiri si mkubwa kiasi hicho. Siku hizi mambo yanafanyika kienyeji sana, hasa Polisi. Utii kwa chama tawala umewaharibu sana, maana sasa wanasiasa ndio wanaongoza jeshi la polisi na kulipa amri za oparesheni. Polisi wana spend muda wao mwingi ku monitor twita account za wanasiasa na magazeti ili kujua viongozi wa CCM wamesema nini dhidi ya upinzani wakatekeleze haraka, na wanasahau hata kuangalia ukiukwaji wa taratibu za kipolisi. IGP anatia sana aibu.

Angalia hii thread

IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia? - JamiiForums
Naona weledi umekuwa zero kabisa. Sijui akili zao wamezitupa wapi?
 
Back
Top Bottom