Je, Imefika wakati serikali kukiangamiza kikundi cha watu wasiojulikana?

KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000
Yawezekana watawala wa dunia (CIA, ICC, NSA, MI6, nk.) ambao sasa unaweza kuwaita watawala wa dunia, wana taarifa kamili za watu wasiojulikana kwenye database zao. Awe jiwe ama yeyote yule, tayari yupo, na chochote kinachoagizwa na kufanywa kinaangaliwa kila saa iendayo kwa Mwenyezi Mungu.

Somalia, Iraq, Libya, Syria, Kongo, nk, ni mifano ya nchi zilizochezea nguvu za hawa watawala wa dunia, zikaonja cha moto. Endapo serikali hii haitachukua tahadhari sana kwenye vikundi hivi vilivyobatizwa "wasiojulikana", basi taifa hili ipo siku tutaliingiza katika mtego wa kujitegea wenyewe. Katika mtego huu wa kujitega wenyewe, taifa litaenda kuangamzwa na kurudishwa zero.

Endapo serikali haitajinasua kwenye mtego huu wa kujitegea wenyewe, basi tufanye maandalizi mapema kabisa. Tufanye maandalizi ya kuzalisha vikundi vya kufanya mauaji vinavyomilikiwa na serikali na vya kupandikizwa na wale wanaotaka tusipige hatua yoyote ya maana. Hata akina Kagame wanaweza kututumia majasusi wao (kufanya mauaji) ili kuivuriga nchi yetu kwa maslahi ya nchi yake.

Serikali isipoangamiza vikundi hivi, ninaona dalili zilizo wazi kwa maadui wenye hadhi ya mataifa na wale wenye chuki tu na nchi yetu kutuingizia vikundi vya kupandikia vya majasusi wabobezi na kuvipatia mafunzo kwa ajili ya kufanya "political assasinations" kwa jina lile lile la wasiojulikana ambao jamii itaelewa kuwa ni wametumwa na serikali.

Tuseme kwa mfano, ikitokea kiongozi anayeonekana kuwa atalifaa taifa akashambuliwa kwa staili ile ile ya "wasiojulikana" serikali itajiteteaje kuwa siyo(au wakubwa ndani ya serikali) iliyoamuru aangamizwe? Ninachelea kusema ila hata kwa mfano akiibuka assasin ndani ya mfumo na kufanya uhaini (kwa jina la hao wasiojulikana) nchi itabaki salama?

Njia pekee ya kutoka kwenye hili giza ni kukiangamiza hiki kikundi cha wasiojulikana na kusitisha shughuli zake haraka kabla havijaibuka vikundi vinavyodanana vya wasiojulikana kweli. Ninafahamu kuwa wanaoongoza hivi vikundi wanazo siri na maangamizi ya vikundi vya aina hii ni lazima roho za watu wengine tena zirudi kwa mola. Mtawala mwanasiasa hatapenda kuacha "signature" ya mambo ambyo kesho yataweza kumuandama. Kutokana na ugumu wa kukiangamiza kikundi cha aina hii, ni muhimu ikaundwa tume maalum ya kibunge ikachunguza na ikawawajibisha baadhi ya watu kisiasa na wengine wakafukuzwa kazi. Aina hii ya accountability angalau itaonyesha kuwa kuna will ya serikali kuondokana na vikundi vya aina hii.

Altenatively, serikali iendelee kushupaza shingo na kuendekea kulea vikundi hivi. Hata utawala wa Taleban ulikuwa unaona fahari kumlea Osama bin Laden na kikundi chake cha Al-qaida mpaka walipofikishana kwenye hatua ya kushindwa kumtoa Osama kwenye mfumo wa utawala yao, wakaishia kuangamia kwa pamoja.
 
bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,391
2,000

Magu take care of this.Tanzania used to be most peaceful country.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom