Je ilikuwa ni kosa kuruhusu Bodaboda na Bajaji kuhudumu kama usafiri wa umma??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Wadau Heri ya Mwaka Mpya.
Ikiwa hili ni andiko langu la kwanza katika huu mwaka mpya 2019.
Nimajaliwa yetu kuwa wote mu buheri wa afya njema.

Nirudi katika maudhui ya hili andiko nikweli kichwa cha habari kinajieleza lakini naongeza nama kidogo. Katika kipindi cha hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 tuliona ongezeko la hivi vyombo vya usafiri kama Bodaboda na Bajaj na ukweli vimesaidia katika kufubisha safari pia kufupisha maisha ya vijana wetu kuvunjika na wengine kuwa wezi,majambazi na uharifu mwingi ni wa bodaboda katika mabenki,mitaani Je tukirudi nyumba kuruhusu huu usafiri utumike kama wa umma serikali aikupotea??
Je ni rahisi kuuzuia na kuja na mbinu mbadala maana nasikia kuna nchi walipiga marufuku kuingiza bajaj na bodaboda kama usafiri wa umma.
Na dhani hata hapa tunatakiwa kufanya hivyo bila kujali hawa niwapiga kura wetu.
 

Attachments

  • Bajaj.JPG
    Bajaj.JPG
    65.3 KB · Views: 35
  • boda1.jpg
    boda1.jpg
    36.6 KB · Views: 28
Ni usafiri mzuri.Tatizo lipo kwa watumiaji na matumizi yake.Madereva walio wengi ni vijana.Na wengi wao(si wote)hutumia vilevi ambavyo huwaondolea umakini na hapo ndipo hutokea dhahma.Yawezekana akaendesha kwa mwendo mkali na kusababisha au kusababishiwa ajali kwa kukosa umakini.
Vilevile kuna abiria huwa wanajidai wana haraka na kuwahimiza waendeshaji kwenda mwendo mkali.Mwishowe ni ajali.Na tena kwa waendeshaji huwa wanatumia muda mwingi kuwa barabarani.Hivyo basi wanachoka na hatimaye kukosa nguvu,umakini na kusababisha ajali.
Na nyakati zingine unakuta bodaboda moja wamepanda watu wanne(mshikaki).Jambo hilo humkosesha kumudu uendeshaji wa bodaboda kwa dereva na kusababisha ajali hasa sehemu zenye kona kali na miteremko mikali.
USHAURI.
-Madereva wafuate sheria za barabarani
-Madereva waache kutumia vilevi halafu wakaendeshe vyombo vya moto
-Uvaaji wa kandambili hasa kwa madereva bodaboda uachwe.Wanaweza kunasa au kujikwaa kama siyo kuteleza kwenye pedali wakati wa safari
-Abiria waache kuhimiza au kushabikia mwendo mkali.
-Abiria wasikubali kupanda mishikaki.
-Dereva na abiria waamue kwa hiyari kuvaa kofia ngumu/helmets
ONYO:Mwendokasi unaua lakini uzembe barabarani ni zaidi ya kupenda kujiua kwa hiyari.
 
Back
Top Bottom