juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Sote tunajua namna na jinsi viongozi wetu walivyotuaminisha kwamba Lowassa ni fisadi na hadi kwenye list of shame alitajwa pale Mwembeyanga sote watu wa UKAWA kijumla tukaimba huo wimbo sana takribani miaka 8 ghafla bin vuu Lowassa akawa mgombea wa urais kupitia kwa waliomwita fisadi, eti tumebadili gia angani.
Hadi mzee ninayemheshimu na nitamuheshimu kwenye siasa Dr. Slaa akaondoka kwenye chama kwa kuwa hakuwa tayari kumpaka mtu rangi, anyway niachane na hayo maana ilikuwa ni kukumbushana tu.
Sasa uzi wangu nauliza je ikitokea Lowassa akapelekwa mahakama ya mafisadi ina maana UKAWA wenzangu hamtalalamika kwamba anaonewa kwa sababu yupo upinzani?
Nauliza hivo kwa sababu juzi hapo sheria imefuata mkondo wake kwa Sumaye watu mmelalama kwamba anaonewa kwa kuwa tu yupo upinzani na pia hivi karibuni imekaliliwa kwamba mahakama ya mafisadi imekosa kesi, watu wanapaza sauti na kupiga mayowe kwamba basi Lowassa sio fisadi kwa kuwa hajapelekwa huko na hata mwaka jana wakati wa uchaguzi mtu wa ukawa yeyote ukimwambia Lowassa ni fisadi basi kinga yake kuu ni "mbona hapelekwi mahakamani" hivi leo hii akipelekwa hamtalalamika?
Mi nadhani Rais Magufuli hajaamua kufanya siasa za visasi na ndio maana alisema hafukui makaburi nina uhakika akishitakiwa Lowassa leo hii walewale wanaosema kama ni fisadi apelekwe mahakamani watalalamika sana na kusema anaonewa kwa sababu tu ni mpinzani.
Christmas njema.