Je, idadi ya viongozi kwenye majimbo inaendana na mahitaji ya wananchi na kazi iliyopo?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Wote tume shuhudia mabadiliko yaliyofanywa na serikali kwenye nyadhifa za wakuu wa mikoa hivi karibuni. Naamini kwa kiasi kikubwa kwamba maamuzi ya serikali mara nyingi huwa yame chambuliwa kwa kina na huwa sahihi.

Jambo ambalo bado sijapata ufafanuzi na kuelewa ni njia zinazotumika kufanya maamuzi hayo na muundo wa viongozi walio katika majimbo mbalimbali. Kwa sasa kila jimbo lina mbunge, madiwani, mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, na wenyekiti wa serikali za mitaa.

Mbunge ni muwakilishi wa wananchi aliye chaguliwa. Hii inamaanisha kwamba hata kama serikali haijaridhika na utendaji wake wa kazi, haiwezi kumuondoa kwenye nafasi yake ya uongozi. Je, ni kweli kwamba serikali inawapa wabunge mamlaka ya kutosha kuleta maendeleo kwa wananchi kwenye majimbo yao? Kama hili ni kweli, majukumu ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wenyekiti wa serikali za mitaa ni yapi?

Siwezi kuongelea suala la gharama ya kuendesha serikali kwasababu mambo kama hayo mara nyingi huwa hayakosewi. Ila ni vyema kufahamu tofauti ya mtumishi anayeteuliwa na Rais na mtumishi aliyepigiwa kura na wananchi. Je, hili lipo kwasababu serikali inaamini kwamba wananchi wanaweza kukosea katika maamuzi yao au ni mpangilio unaotumaliza polepole?

Tafakari,

Jumma Mubarak
 
Back
Top Bottom