Je, huyu Rais wetu wa sasa ni Vasco Da Gama mwingine? Ziara za nje zimekuwa nyingi sana kama enzi za Awamu ya Nne

Baada ya kusimangwa sana kuhusiana na masafari ya kila kukicha ya kwenda ughaibuni, Rais wetu amebuni mbinu mpya.

Sasa hivi anasafiri kimya kimya. Hatoi taarifa kama hapo awali.

Jana tumeshtukia tu yuko Dubai anapiga picha sijui na akina nani wale!

Mwanzoni tulizoea vyombo vyote vya habari vinatangaza kuhusu safari zake. Na akiwa anaondoka wanapanga mstari mnyoofu kumsindikiza. Akirudi pia wanapanga mstari kumpokea.

Vipi kulikoni? mbona ghafla safari zimekuwa za kinyemela? Ni mwendo wa kimya kimya!

Hatujaona ile mistari ya kuagana na kupokeana. Hata ikulu hawatuambii lolote.

Kama safari ni jambo jema, hakuna haja ya kujificha.

Si nimesikia mnafungua nchi sijui?View attachment 2133126
Wewe unaandika ukiwa na maumivu ya moyoni. Samia ndio rais wa awamu ya sita na kazi inaendelea.
 
Long term plan ipi?

Yeye amekuta mega projects za mjomba Magu in progress bila pesa ya kuimaliza kwa wakati kama SGR,na nyingine.Na uwezo wetu ni mdogo mno kufanikisha miradi hiyo mikubwa.Sasa ulitaka afanyeje?

Pili sio kila ziara yake ni mikopo,unajua kwanini alienda kwenye ziara ya EXPO Dubai 2022?

Kazi mmoja wapo ya Raisi ni kukutana na viongozi mbalimbali ulimwenguni ili kukuza mahusiano ya kiuchumi,Usalama,Tekinologia, Biashara, Mazingira,Nishati,Elimu,Afya n.k
Hawa wanaishi na maumivu moyoni sidhani kama unachowaambia wanaweza kukielewa.
 
Mtu 'kwao' bhn... unataka aandae wapi makazi akisusa 2025?

Mkataa kwao mtumwa in Magufuli's voice....

Long live Chato

Long live Gbadolite!!
 
Nadhani mpaka anamliza muda wake Madarakani safari tu Pesa zitakazo tumika zitakuwa na Uwezo wa Kumaliza kabisa matatizo ya Maji safi na Umeme Nchi nzima ,na Atamaliza muda wake hayo matatizo Bado Yapo .
 
Wajanja wameona fursa so ni mwendo wa kusainishwa mikataba....who knows labda hii ziara ya Oman ni zamu ya Kilimanjaro au Serengeti kabisa. Tukae kwa kutulia.
 
Wawekezaji wa kutoka nje hawatatusaidia sisi kujikomboa kitu cha msingi tutafute teknologia tutengeneze vyetu tupate mtaji na huu mtaji yaani fedha zipo ila matajiri hawataki kulipa kodi. Hebu angalia mpaka leo wenye mabasi wamegoma kutumia zile mashine F nini sijui kukata tiketi. Ukituma barua bahasha shs. 5,000.00 risiti hawatoi na serikali ipo
 
Back
Top Bottom