JE HUYU NDIYE NITAOANA NAYE, Nitajuaje ni Yeye? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JE HUYU NDIYE NITAOANA NAYE, Nitajuaje ni Yeye?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Aug 23, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Uchumba ni mtamu acha kabisa, ila kumbuka ndoa ni kitu halisi!
  Kumekuwa na maswali mengi sana naulizwa na vijana wengi wa kike na wakiume ambao wanataka kujua ni yupi anaweza kuwa mchumba halisi ambaye atakuwa mke au mume wake.
  Ukizingatia kwamba kuoa au kuolewa ni uamuzi ambao unaweza kupelekea kuwa mtu wa furaha katika maisha yako au mtu huzuni na kujuta siku zote katika maisha yako.
  Mambo ya msingi kuangalia ni haya:

  MAHUSIANO HUWA RAHISI TANGU SIKU YA KWANZA:
  Tangu siku ya kwanza nilipojikuta naonana uso kwa uso upendo uliokuwa kati yangu na yeye ulikuwa natural, nilijihisi nimemuona mwanamke ambaye namfurahia kila kitu, namkubali kama alivyo, nilihisi kama tulizaliwa tuishi pamoja na sasa nimempata mtu ambaye nimekuwa namtafuta, nilijiona atanitosheleza kimwili na kiroho, ninapoongea nayenaridhika kwa mvuto alionao.
  Kila kitu katika mahusiano na urafiki wetu kilikuwa natural na kutupa hisia mpya kabisa hapa duniani.
  Wapo ambao katika safari ya uchumba hadi ndoa hufikia kuzipiga na kugombana mara nyingi sana, leo wanazipiga au kununiana au hugombana na kesho wanapatana tena na kurudiana.
  Wanaendelea na kasheshe hizo hizo mara kwa mara hadi wanaoana.
  Inawezekana unarudiana naye labda kwa kuogopa ukiachana naye hutapata mtu mwingine wa kuoana naye, au umri unaona umeenda sana, au unataka kuondoa nuksi ili na wewe ujulikane uliolewa, au rafiki zako watakucheka au una hamu sana na sex, Kumbuka ni busara kuachana wakati wa uchumba kuliko kuachana ikiwa ndoa.
  Ukiingia kwenye ndoa utakumbana na storm ambayo itakuja kupima kama sababu zako za kuoana zilikuwa strong kuliko storm yenyewe na kama zilikuwa weak storm itakuchukua bila huruma.

  UHUSIANO MZURI NA FAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI:
  Inaweza kuwa tofauti kidogo hasa linapokuja suala la dini, kabila, nk kwani mara nyingi wazazi na familia nyingi huwa na lao kuhusu kabila au dini.
  Ikitokea kwamba mchumba wako ni kabila moja, dini moja na bado ndugu zako, familia yako au marafiki zako hawaelewani naye ni vizuri kufikiria upya.
  Wewe umelelewa na familia na kutokana na hayo malezi ndivyo ulivyo na umempata huyo mchumba kutokana na tabia yake aliyokulia au kulelewa na hiyo familia na kama bado hakubadilika maana yake hapo kuna bendera nyekundu inawaka na inaashiria kuna kitu hakipo sawasawa.
  Kawaida ukishaingia kwenye mapenzi (fall in love) huweza kupunguza uwezo wako wa kuamua na kuona kasoro ndiyo maana wanasema love is blind.
  Hii haina maana kwamba unatakiwa kuvunja mahusiano eti kwa sababu ya ndugu, familia au marafiki hawakubaliani na huyo mchumba wako ila ni kawaida kwamba inawezekana kuna kitu ndugu zako na familia yako wanakiona na wewe hukioni ambacho mbele ya safari mkiwa kwenye ndoa unaweza kukumbana nacho na bahati mbaya umewakana wazazi ndugu na marafiki.
  Utaenda kwa nani kuomba ushauri maana umekuwa kichwa ngumu.
  Jaribu kuchunguza kile ambacho ndugu zako au familia au marafiki wanasema vibaya kuhusu huyo mtu wako inawezekana ni kweli.
  Ni kawaida kama umepata mtu wa kufanana na wewe basi huweza kujichanganya kirahisi sana na ndugu zako, familia yako na marafiki zako.

  HUTAONA KITU KIKUBWA CHA KUMBADILISHA:
  Kawaida, hata kama mnapendana kuliko binadamu yeyote chini ya jua, bado tofauti ndogondogo zitakuwepo; hata migogoro itajitokeza pia.
  Ila kama kuna jambo kubwa sana unaona ni muhimu sana yeye abadilike basi hiyo ni ishara kwamba fikiria kwa makini.
  Tatizo ukishashambuliwa na chemicals za love unaweza kujikuta unadhania kwamba haina shida kwa tatizo au kasoro alizonazo na utavumilia.
  Ukiingia kwenye ndoa chemistry ya mapenzi hushuka na kupanda kutokana na jinsi mnavyojitahidi kuimarisha ndoa yenu; hapo ndipo sasa utagundua kwamba ulichemka and too late.
  Usiingie kwenye ndoa ukidhania utambadilisha mtu sana sana wewe ndo utabadilishwa.
  Kama umegundua kuna kitu ambacho ni tatizo kubwa sana mbele ya safari na hutaweza kuishi nacho ni vizuri ku move out kuliko kupoteza muda wako na kujifariji na baada ya miaka 3 ya ndoa ujikute upo kwenye jehanamu yako mwenyewe na upweke uliokithiri.
  Watu hupata upweke lakini upweke wa kwenye ndoa ni mbaya kuliko upweke mwinghine wowote duniani.

  NI RAFIKI
  Mvuto wake ni kitu muhimu sana katika mahusiano.
  Ndani ya mahusiano lazima kuwa na mzizi mkuu wa urafiki ambao hata mkiwa wawili sehemu yoyote duniani bado mnajiona hamjapungukiwa na pia bado mnajiona ndiyo marafiki bora duaniani.
  Je, unajiona unahitaji kutumia muda na yeye tu?
  Je, unajisikia raha kuwa na yeye wawili tu?
  Je, unahisi yeye ndiye anastahili wewe kumwambia siri zako na kwamba ni yeye tu anakufahamu kuliko mtu yeyote duniani, kama ni NDIYO, basi mshike vizuri.
  Kuwa best friends hata baada ya kuoana ni raha sana, na ndoa hudumu, maana hakuna anaye bore mwenzako.

  UNAPOFIKIRIA KUOANA NAYE HAIKUPI SHIDA:
  Kama unajikuta unapofikira kuoana naye huna wazo lingine la kuhisi ndoa inaweza kuwa na matatizo na unajisikia amani ya kweli moyoni na kwamba future yako na yeye itakuwa sawa basi umepatia.
  Mwisho Kumbuka Kumuomba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mtu wako maana yeye ndiye anajua liubavu lako lipo wapi.
  “Marriage is not about finding a person you can live with, it’s about finding the person you can’t live without.”

  AMEN.......!!!!
   
 2. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,355
  Likes Received: 2,360
  Trophy Points: 280
  Kumbe na wewe huwa una Focus? Nilijua matani mengi kuliko maarifa
   
 3. c

  christmas JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,608
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  true dat, ukizingatia all those you have mentioned utaenjoy mbona
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Thanks. Nimeipenda zaidi hii part ya mwisho ....
   
 5. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Minaona chamsingi nikumuomba Mungu akujalie mwenye kheir na wewe muishi kwa salama na amani,manake unaweza mpata
  mchumba kabla ya ndoa ukasema mungu usinipe mwengine zaidi ya huyo,mkisha oana hivyo visa vyake unajuta kumfahamu au bora usingeolewa maisha.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  "Marriage is not about finding a person you can live with, it's about finding the person you can't live without."  Mkuu kibweka hii hapa ndo inatoa summary ya hayo hapo juu yote uliyoyaandika
  Nimeipenda sana aise na asante sana kwa uzi wako huu
  Nilijua wewe ni mtu wa yale mambo tuu kumbe sometime unaweza kaa ukatoka na kitu kama hiki
  Asante sana mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  "Marriage is not about finding a person you can live with, it's about finding the person you can't live without."  Mkuu Kimbweka hii hapa ndo inatoa summary ya hayo hapo juu yote uliyoyaandika
  Nimeipenda sana aise na asante sana kwa uzi wako huu
  Nilijua wewe ni mtu wa yale mambo tuu kumbe sometime unaweza kaa ukatoka na kitu kama hiki
  Asante sana mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kimbweka, hAPO KWENYE NYEKUNDU UMESEMA SAWA, NIMEIPENDA HIYO
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mkuu unatisha, mie huwa mvivu kusoma post ndefu, lakin hii nimeisoma na badhi ya paragrafu nimezirudia.
  nataman mtu ambae nitamwoa asome hapa
   
 10. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,861
  Likes Received: 1,137
  Trophy Points: 280
  well said Kimbweka hasa hapo kwenye red ndo shina la ndoa imara. . . remain blessed
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Amen...........................!!!!
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu " UKUBWA DAAUWAAA"
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kimbweka, na wewe umeoa au una mpango wa kuoa? Mke lazima akupende maana umebobea eneo hilo, teh teh teh
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hahahaha acha utani bhana...... mie nananiliu tu......
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  We mtaalamu bwana...na ukimaliza lazima unachukua foto ya ukumbusho...teh teh teh. nakuaminia lazima mama akukubali.
   
 16. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,297
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  duh!asante
   
 17. mjombo's

  mjombo's JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  umetisha mkuu
   
 18. M

  Mtaftaji JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ilo nalo neno,ila jitihada ziendane na vitendo naisi mungu ndo hutoa usaidizi wake.
   
 19. M

  Mtaftaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ww ndo km mm,natamani atakaekuja nioa asome na ayaelewe haya.mungu akuzidishie mkuu,elimu c mpk chaki na kalamu.
   
Loading...