Je, huyu binti alikuwa sawa kupanga mauaji ya mama yake kwa kosa alilomtendea?

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,040
Gypsys Rose Blanchard alikuwa akiishi na mama yake aliyejulikana kama Dee Dee Blanchard, ambaye alikuwa akidai ya kwamba Gypsy alikuwa na matatizo ya kiafya ambayo yameathiri ukuaji wake. Watu wote kuanzia madaktari, familia na jamii kwa ujumla walikuwa wanaamini madai haya, ila ukweli ni kwamba Gypsy hakuwa mgonjwa kama mama yake alivyokuwa anadai. Wataalam wa mambo ya magonjwa ya akili wanadai Dee Dee alikuwa ana tatizo la kiakili llijulikanalo kama Munchausen Syndrome by Proxy, na ndilo lilimfanya Dee Dee awe na shauku ya kuwa kama mhudumu wa wagonjwa, hivyo kumlazimishwa binti yake kuigiza kama mgonjwa.

Kwa miaka Zaidi ya 19, hakuna aliyejua kuwa Gypsy hakuwa mgonjwa ila ukweli ulikuja kujulikana mwaka 2015 baada ya Dee Dee kuawa na rafiki wa kiume wa Gypsy waliokutana katika mtandao wa inteneti.

Je, Dee Dee aliwezaje kudanganya kila mtu kuwa Gypsy ni mgonjwa?

Gypsy Rose alizaliwa mwaka 1991, na akiwa na umri wa mwaka tu Dee Dee alianza kudai ya kwamba mwanae ana tatizo la kukosa usingizi. Haikuishia hapo, Gypsy akiwa na umri wa miaka nane, Dee Dee alidai kwamba mwanae ana Mkanda wa jeshi na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa misuli. Akadai kwamba mwanae alihitaji kiti cha magurudumu kwa sababu hawezi kutembea, na pia alihitaji mpira kwa ajili ya kumlisha. Huyu mama hakuishia hapo aliendelea kila mara kuja na madai mapya juu ya magonjwa mbalimbali ya mwanae ikiwemo, athma, kifafa, matatizo ya kusikia na kuona pia.

Lakini ukweli ni kwama Gypsy hakuwa na tatizo lolote, kwani alikuwa na uwezo wa kutembea, kula bila kutumia mpira na wala hakuwa na mkanda wa jeshi. Kichwa chake kilikuwa hakina nywele, kwakuwa mama yake alihakikisha anamnyoa kila mara ili kumfanya Gypsy aonekane kama mgonjwa anayesumbuliwa na mkanda wa jeshi inayomfanya asiote nywele. Lnego kubwa alitaka aonewe huruma kama mama anayehangaika kumtunza mtoto mwenye magonjwa makubwa.

Mbele ya jamii Dee Dee alionekana ni mama aliyejitolea kumlea mwanae mwenye matatizo makubwa, na watu walimpenda na kumhurumia wakimuona ni mfano wa kuigwa.

Mara nyingi vipimo vya madaktari vilionyesha matokeo ambayo yalikuwa yanapingana na madai ya Dee Dee au matokeo ambayo hayaeleweki, lakini Dee Dee alikuwa harudi kwa daktari yoyote aliyehoji kuhusu ugonjwa wa mwanae. Dee Dee alikuwa na elimu ya utabibu hivyo alikuwa anajua dalili za magonjwa mengi, na hilo lilimsaidia katika kudanganya madaktari na watu juu ya ugonjwa wa mwanae.

Gypsy alipokuwa mkubwa akawa na uwezo wa kuzungumz,a Dee Dee alimzuia kutosema chochote hasa wakiwa kwenye mahojiano ya TV au wawkiwa mbele ya hadhira, na pia alimlisha maneno ya kuzungumza.

Dee Dee alienda mbali Zaidi kwa kumdanganya baba yake Gypsy kwao mtoto wao alikuwa na tatizo la chromosomes na ndilo lilipelekea yeye kuwa na matatizo hayo. Hata baba yake Gypsy alikuwa akimpongeza mzazi mwenzake kwa kujitoa katika kumtunza mtoto wao. Lakini kuna wanafamilia waligundua kwamba Gypsy alikuwa na uwezo wa kutenmbea na hakuhitaji kiti cha magurudumu. Walipojaribu kuhoji, Dee Dee alijitenga nao kabisa na kuhama hilo eneo.

Dee Dee alidai yeye ni katu ya wahama wa kimbunga cha Katrina, hivyo yeye na mwanae walipewa msaada na kupewa makazi mapya Missouri mwaka 2005. Pia akiwa huko Dee Dee aliendelea kumpeleka mwanae kwa madaktari.

Uongo wa Dee Dee uliendelea hata baada ya Gypsy kuvunja ungo. Nyumba yao mpya waliyopewa huko Missouri na shirika la Habitat for Human, ilikuwa imejengwa ili kumwezesha Gypsy kuwetumia kiti chake cha magurudumu kwa urahisi. Pia Dee Dee aliendelea kupokea msaada wa kifedha na chakula kutoka kwa wahisani pamoja na Disney World.

Akiwa na umri wa miaka 14, kuna mtaalam wa mishipa ya fahamu huko Missouri ambaye alipompima aligundua kuwa alikuwa hana tatizo ila ajabu hakuwahi kutoa taarifa kwa wahusika. Baadae alikuja kudai ya kwamba hakuwa na ushaidi wa kutosha ndiyo maana hakutoa taarifa. Mwaka 2009, mtoa taarifa asiyejulikana alijulisha mamlaka kuwa madai ya Dee Dee hayana ushahidi wa kitaalam. Ripoti hii iliwafanya wafanyakazi wa mamlaka kutembelea nyumba ya Dee Dee kumtazama Gypsy lakini aliweza kuwaongopea nao wakaridhika kuwa ni kweli mtoto anaumwa.

Baada ya Gypsy kuzidi kukua, Dee Dee alianza pia kudanganya kuhusu umeri wake kwa kubadili tarehe za cheti cha Gypsy. Lakini Gypsy alikuwa ameanza kujitambua jambo lilikuwa linamwekea ugumu Dee Dee na kuanza kuhisi itakuwa vigumu kwake kumcontrol.

Jinsi Gypsy alivyokutana na mpenzi mtandaoni

Mwaka 2011, Gypsy alijaribu kutoroka ili awe mbali na mama yake, na alitaka kukimbia na mwanaume aliyekutana naye katika kongamano lijulikanalo kama Science Fiction. Lakini Dee Dee aliweza kuwafuatilia na kuwanasa, na aliweza kumdanganya huyo mwanaume kuwa Gypsy bado mtoto japokuwa Gypsy ni kwamba alikuwa na umri wa miaka 19 tayari. Kutokana na maelezo ya Gyspy, anadai mama yake alivunja computer yake na akampiga marufuku toka nje ya chumba chake. Pia anadai kuna wakati mama yake alikuwa akimpiga na kumnyima chakula.

Lakini Gypsy alifanikiwa tena kupata computer na kuanza kuwasiliana na watu mtandaoni. Alijiunga na mtandao wa kutafuta wachumba, ambapo aliweza kukutana na Nicholas Godejohn. Alimweleza ukweli wa maisha yake na kuhusu mateso anayopata kutoka kwa mama yake, na kumwomba amsaidie kumuua mama yake ili wapate kuwa wote. Mwaka 2015, Nichlas alikuja nyumbani kwa Dee Dee usiku, akamwambia Gypsy ajifiche bafuni aizbe masikio wakati yeye akimchoma mama yake visu mfululizo.

Baada ya hapo walifanya mapenzi kabla ya kuondoka wote kwenda kwenye maazi ya Nicholas huko Wisconsin na baadae kukamwa na askari. Gypsy kabla ya kukamatwa aliweka ujumbe Facebook akiandika kwamba Yule Malaya amekufa. Alikuja kudai aliandika vile ili kuwaarifu watu wapate kwenda nyumbani kwao ili wajue kuwa mama yake kafariki na watoe mwili wake.

Baada ya hili tukio watu wengi walishangaa ni kwanini alishindwa kuongea mpaka akaamua kupanga mauaji ya mama yake. Ila yeye alidai alikuwa hamuamini mtu na alihisi itakuwa vigumu kuaminika. Pia anadai anafurahi kuwa mamake amefariki sasa.

Gypsy alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela huku Nicholaus alihukumiwa kifungo cha maisha.

image.jpg

Hii ni picha yake before akiwa ana act ugonjwa na after akiwa ashafungwa
 
Back
Top Bottom