Je, huyu atafufuka kupiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, huyu atafufuka kupiga kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nikupateje, Oct 27, 2010.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Jamani JF ni mtandao bomba kuliko tunavyoweza kufikiri. Wasioijua JF wanasambaziwa kwa message za simu kila linalosemwa hapa.

  Nimepata taarifa kwamba kuna binti alifariki mwaka 2006 na jina lake limo kwenye list ya wapiga kura watakaopiga Jumapili ijayo.

  Binti huyo anaitwa ANNA NELSON MTOWE na namba ya kadi yake ya uchaguzi ni 18361252.

  Ukimuangalia kwenye list ya wapiga kura anaonekana yumo kwenye kituo cha DAR INSTITUTE OF TECHNOLOGY (DIT) kilichopo kata ya Upanga Mashariki jijini D'Salaam.

  Ukitaka kuhakikisha nenda kwenye website ya NEC {http://www.nec.go.tz/?modules=reg_status&sub} halafu ingiza namba ile kisha ubonyeze SEND. Utona details zake kama mpiga kura.

  Solution ni nini? Solution zinaweza kuwa nyingi na mimi niliyofikiri harakaharaka ni kwamba ukigundua kuna mtu amefariki au hatapiga kura. Basi tafuta namba ya simu ya mwanachama yeyote hasa wa upinzani na umpatie details zote.

  Wanachotakiwa kufanya ni kwamba mfano umegundua jina halafu ukaona kituo ni kama hiki yaani DIT. Tuma details zote kwenye simu ya mwana-CHADEMA na yeye mara moja atai-forward message ile kwa mawakala wa kituo hiki cha DIT.

  Ama ikibidi ianzishwe thread humuhumu JF ya list ya wasiotakiwa kupiga kura kama waliofariki hivi. Kisha mawakala wakipewa hata kwa simu basi siku ile wawe na kazi pia ya kuangalia kwa umakini sura za picha ya kitambulisho na picha halisi. Akibahatika kuona namba aliyonayo na tofauti ya sura ni wazi basi mtu huyo atiliwe mashaka na awekwe pembeni.

  Wakala akigundua hivyo basi atume chamani kwamba namba fulani tuliyoihisi tumeikamata. Chamani wanaweza hata kuishirikisha JF au hata mitandao mingine kuwa namba fuani tayari imeshakamatwa.

  Zikishapigwa kelele hivi jamaa watakuwa na nafasi finyu ya kubuni mbinu mpya. Vilevile wengine watakuwa wanasambaziana kwenye simu za mkononi hasa wasioakaa sana kwenye computer. Maana hata baada ya hii thread wataona kuwa wameshang'amuliwa mbinu zao.

  Vilevile kuna suala la kulinda kura ukiwa umekaa zaidi ya mita 100 toka kituoni ama sheria inavyosema. Lakini vilevile baadh ya wana JF wasisite kwenda na camera zenye picha kupiga kura na wakati wa kulinda kura ili tupate matukio live. Chochote kitokeacho basi kirushwe online.

  MOD kama hujajiandaa kuongeza quota ya server yako basi ujue Jumapili taarifa ni nyingi.
  Sijui mnasemaje wanandugu, boresheni wazo hili ikibidi kwani nimeandika nilipopata wazo tu na sijafikiri mengi zaidi.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhhhh yah na njia nyingine wanayofanya jamaa ni kuwamisha na kutoa majina ya vijana wengi
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona kama hao wako wengi
   
 4. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  mkuu bora huyo alikufa na jina lake lipo, kuliko hawa wazima ambao majina yao hayapo. mkuu inauma sana watu wengi wa kituo cha stend kuu hapa iringa hawajayaona majina yao, walipania mno kuleta mabadiliko lakini hawawezi tena. kituo hiki wamekiogopa sana kwa sababu HAPO CHADEMA wana wafuasi wengi. hainashaka kitaeleweka tu.
   
Loading...