earl
Senior Member
- Aug 30, 2012
- 138
- 181
Habari zenu wanaJF,
Naombeni ushauri wenu. Nimekua katika mahusiano na huyu msichana kwa miezi 8 sasa. Ni msichana ambae anajiheshimu na hana makuu. Katika kipindi chote hiki ameweza kutenga muda wake kwa ajili yangu mara nyingi sana ikiwa ni pamoja na kunitembelea kwangu, kunipa company katika sherehe mbalimbali kama harusi, n.k.
Tatizo ni kwamba pamoja na kwamba tunapokua pamoja anakua mwenye furaha, na anafurahia company yangu, ni kwamba kila nikimweleza jinsi gani ninampenda na nina malengo nae huwa anajibu "asante". Hajawahi kunitamkia kwa mdomo, au hata kupitia msg kwamba ananipenda. Huwa anatoa tu shukrani za kawaida.
Wakati ninapokua nimekaa nae, nikijaribu kumshika, n.k, naona kama hakuna hisia zozote kwake.
Najiuliza vitu viwili, kabla ya kuwa na mimi alishawahi kutendewa ukatili fulani, au hanipendi.
Naombeni ushauri wenu.
Asante.