Je, huyu anaesemwa na Wema Sepetu kwenye tangazo hili la dawa za Mkongo, anaweza kushitaki kwa udhalilishaji kwa manufaa ya kibiashara?

Exorcist

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
1,236
1,257
Nimekutana na tangazo la dawa za nguvu za kiume huko Instagram lililotolewa na Wema Sepetu. Katika tangazo hilo lenye lengo la kujiingizia kipato kupitia biashara hiyo ya dawa za nguvu za kiume, kuna mtu ametolewa kama mfano, wanamuita CK wa ikulu sijui kwa jinsi nilivyosikia humo, lengo likiwa ni kunogesha tangazo hilo la biashara.

Sasa je, endapo mtu anadhalilishwa kwenye umma kwa malengo ya kibiashara, hawezi akatumia sheria ya defamation ili walau faida iliotokana na mauzo ya dawa hizo za nguvu za kiume waweze kugawana nusu kwa nusu au pengine pawe tu na fidia lumpsum ya walau bilioni kadhaa ili kumpooza machungu? Wataalam wa sheria, hii imekaaje?

NB: Sisemi kwamba Wema Sepetu amedanganya, la hasha, ila tu, kuna udhalilishaji umefanyika kwa malengo ya kibisahara.
Video ipo chini.

Mara amuulize mama kanumba,NANI KAKUULIA MWANAO? Mara aseme EX ALIKUWA HASIMAMISH!! Nazid kuamin kuwa na watoto ni sehem ya faraja maishani.Anastress za kutozaa tumsamehe
Mimi ningekuwa yeye najiadaptia zangu mtoto maisha yanaenda.

Sema shida inakuja kaweka maisha yake public kupitiliza hivo itakuwa ngumu kwa huyo mtoto na kwake pia mana watanzania tunajijua kuzaa asizae wema tunateseka sisi.

Akajichimbie sehemu hata three years akiibuka anakuja na mtoto halafu hasemi chochote anawaacha tu wajitaftie majibu wenyew na anakuwa serious na ujinga anaacha analea familia huku mbele Mungu akimjaalia wa kuzaa mwenyew maisha yanaenda asipopata tayari anaye.
 
Hii ni ngumu sana, suprises za namna hiyo kwenye maisha hazitakiwi, ni bora kufuata BINARY system, rejea tahadudi(sijui kama nimepatia) ya Domo, mama'ake na baba aliyemu-adopt, umesikia zile kelele, sasa yule mzee ndo anateseka mara elfu zaidi kwasasa.

BTW CK hakuwahi kufanya kazi IKULU wala kwa wazee, alifanya kazi taasisi iliyohusika na viongozi wakubwa kwa namna fulani.
 
Mimi ningekuwa yeye najiadaptia zangu mtoto maisha yanaenda.
Sema shida inakuja kaweka maisha yake public kupitiliza hivo itakuwa ngumu kwa huyo mtoto na kwake pia mana watanzania tunajijua kuzaa asizae wema tunateseka sisi.
Akajichimbie sehemu hata three years akiibuka anakuja na mtoto halafu hasemi chochote anawaacha tu wajitaftie majibu wenyew na anakuwa serious na ujinga anaacha analea familia huku mbele Mungu akimjaalia wa kuzaa mwenyew maisha yanaenda asipopata tayari anaye.
Kama JOLIE( uko sahihi) 100%
 
Back
Top Bottom