Je, huwezi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi mpaka uwe Balozi?

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
476
962
Wasalamu!

Leo Mheshimiwa Rais Magufuli amemteua Dkt Bashiru Ally Kakurwa kuwa katibu kiongozi lakini hapo hapo amemteua tena kuwa balozi.

Sijaelewa mantiki ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu na hapo hapo kuteuliwa kuwa balozi

Atatumikia kipi kati ya hivi viwili?

Wataalaamu wa mambo mtupe darasa hapa.

Maendeleo hayana chama.
 
Nafikiri amepewa title ya "balozi" ili kila jina lake linapotajwa lisound vizuri masikioni mwa watu
 
Si lazima awe balozi. Lakini kuwa balozi hakumzuii kufanya kazi zake.

Ubalozi ni hadhi, si lazima iwe kazi kwamba balozi wa Tanzania nchi fulani.

Mathalani, mtu mwenye hadhi ya ubalozi anatambulika kimataifa kwa itifaki za Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 na kupewa kinga za kibalozi (diplomatic immunity).
 
Katibu mkuu ni lazima awe na hadhi ya kidiplomasia, akiwa kama msimamizi mkuu wa watumishi wote wa serikali.
Siyo Kweli; Timothy Opiyo hakuwa Balozi, lakini nadhani ni kati ya makatibu wakuu waliokuwa wanaheshimiwa na kuogopwa sana; mwulize mzee Msekwa stori ile!
 
Siyo Kweli; Timothy Opiyo hakuwa Balozi, lakini nadhani ni kati ya makatibu wakuu waliokuwa wanaheshimiwa na kuogopwa sana; mwulize mzee Msekwa stori ile!
Timothy Apiyo sio Opiyo hakuheshimika Ila aliogopewa. Ndio maana alivyostaafu walimtupilia mbali mshenzi yule. Aliwatenda watu sana alipokua anaongoza SCOPO. (Standing committee on parastal organizations)
 
Ukiheshimika utatunzwa hata baada ya utumishi wako, nje ya hapo ni kusaga meno wakati wako upitapo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom