Je, huwezi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi mpaka uwe Balozi?

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
315
500
Wasalamu!

Leo Mheshimiwa Rais Magufuli amemteua Dkt Bashiru Ally Kakurwa kuwa katibu kiongozi lakini hapo hapo amemteua tena kuwa balozi.

Sijaelewa mantiki ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu na hapo hapo kuteuliwa kuwa balozi

Atatumikia kipi kati ya hivi viwili?

Wataalaamu wa mambo mtupe darasa hapa.

Maendeleo hayana chama.
 

bituu Kaskas

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
221
250
Martin Lumbanga wakati wa Mkapa, na Philemon Luhanjo wakati wa Jk hawakuwa Mabalozi

Ombeni Sefue na Kijazi ndio Mabalozi

Sio Lazima awe Balozi, nadhan kuna nafasi ya Kisiasa anaandaliwa baadae
Huyo anapitishwa tu hapo si mnajua hakuna kama Kijazi hivyo huyo muhaya ni temporary nasema uongo ndugu zangu
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,196
2,000
Si lazima awe balozi. Lakini kuwa balozi hakumzuii kufanya kazi zake.

Ubalozi ni hadhi, si lazima iwe kazi kwamba balozi wa Tanzania nchi fulani.

Mathalani, mtu mwenye hadhi ya ubalozi anatambulika kimataifa kwa itifaki za Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 na kupewa kinga za kibalozi (diplomatic immunity).
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,593
2,000
Katibu mkuu ni lazima awe na hadhi ya kidiplomasia, akiwa kama msimamizi mkuu wa watumishi wote wa serikali.
Siyo Kweli; Timothy Opiyo hakuwa Balozi, lakini nadhani ni kati ya makatibu wakuu waliokuwa wanaheshimiwa na kuogopwa sana; mwulize mzee Msekwa stori ile!
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,471
2,000
Siyo Kweli; Timothy Opiyo hakuwa Balozi, lakini nadhani ni kati ya makatibu wakuu waliokuwa wanaheshimiwa na kuogopwa sana; mwulize mzee Msekwa stori ile!
Timothy Apiyo sio Opiyo hakuheshimika Ila aliogopewa. Ndio maana alivyostaafu walimtupilia mbali mshenzi yule. Aliwatenda watu sana alipokua anaongoza SCOPO. (Standing committee on parastal organizations)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom