Je, huu ni uungwana? Trafiki wanaandika faini ya makosa ambayo huna halafu siku nyingine wanakudai

MZALENDO NO.1

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
302
134
Hivi umesimamishwa na traffic, akakuomba akukague, ukaridhia bila shida. Akakagua vibali vyote viko sawa,Akakuomba Leseni ya udereva ukampa, akauliza reflect ukampa, fire extinguisher ukampa, ila katika kukagua fire extinguisher akasoma akakuta imesha expire, ukamuomba samahani sikujua kama imesha expire naenda kupita dukani kununua nyingine sasa hivi. Akakuruhusu ukaondoka.

Kumbe huku nyumba traffic alibaki akikuandikia kosa, wewe unatembea na Gari ukiwa hujui kama umeandikiwa kosa, wiki ya kwanza inapita fine inaanza kuongezeka. Siku nikiwa nimesimama kwenye mataa mbele kulikuwa na askari akawa anaingiza plate namba kwenye simu yake, akakuta Gari inadaiwa 52,000 akaniweka pembeni. Akaniambia Gari linadaiwa nikamwambia sijui, nikakumbuka siku ambayo nilisimamishwa na traffic halafu akaniruhusu inawezekana aliniandikia.

Nikamwambia Basi nitakwenda kulipa, akaniambia liache Gari hapa ukalipe ndo uje kuchukua Gari lako. Bahati nzuri kulikuwa na salio kwenye Tigo nikalipa wakaliachia Gari langu.

Sio Mimi peke yangu !! Kuna madereva wanaandikiwa makosa bila kujulishwa, anambiwa ondoka kumbe huku nyuma anaandikiwa kosa, JE HUU NI UUNGWANA?
 
Watakuandikiaje notification wakulipishe bila wewe kuisaini? Au wewe ulisaini kisha ulipoambiwa nenda ukadhani yamekwisha?
 
Back
Top Bottom