Je huu ni uungwana Kikwete kutozungumzia zile Bilioni 300 zilizo Uswisi?

Bila Kikwete kuzifanyia kazi ungezijuwa zilipo?
Na aweke wazi basi tujue kinachoendelea. Mbona mambo mengine anakuja haraka kuzungumzia, hata ya Ulimboka?
Watu wanaamini kuwa hiyo Bl.300 ingetosha kabisa kutatua matatizo yanayodaiwa na hawa ma-Dr. sasa kipi kilistahili kuzungumziwa kwanza?
Rais makini angeacha kuzungumzia swala la mtu mmoja na ku-address swala linalowagusa mamilioni ya watanzania haswa watoto na wakina mama. Tuache ushabiki Mkuu!
 
The government established the Financial Intelligence Unit (FIU) in 2007 to tackle money laundering activities
Imeanzisha hicho kitengo na kimesaidia kugundulika hilo je hatua gani zimechukuliwa? Hapa tunachohitaji ni hatua.
 
Baada ya kutafakari kwa muda mrefu ile hotuba ya JK aliyosema kuwa madai ya madakitari na walimu hayatekelezeki kwa sababu serikali haina uwezo imenilazimu leo niulize:
Je, huu ni uungwana kwa mheshimiwa kukaa kimya baada ya kujulikana kuwa kuna bilioni 300 za mafisadi kule Uswisi?
Je, mheshimiwa haoni kuwa kukaa kimya kunadhihirisha kuwa yeye ni mmojawapo wa wamiliki wa hizo pesa?

Naomba tujadili kama ungekuwa wewe ndie rais ungechukua hatua gani?
Inakuwa ngumu kulizungumzia hilo kwani inatakiwa kwanza hatubu kwa wananchi kwa kufanya kosa na yeye la kuhifadhi fedha huko Uswiss na ndo aseme hatua za kuchukua kwa hili inakuwa vigumu kwa mkuu kulizungumzia kwani watanzania hatuna tabia ya kutubu.
 
Zomba una matata kweli kweli, yaani hiyo UNIT mliianzisha ili kuangalia wezi tu na kutupa taarifa..!!!??

Haya tuliyajadili sana humu mwaka 2008 na ikabainika kuwa Kikwete kaanza initiative za kupatia ufumbuzi haya maswala mwaka mmoja tu baada kuingia madarakani (2006) na sasa tunaona matunda yake, nakuhakikishia kama alivyoweza kurudisha fedha za rada zilizoibiwa wakati wa Mkapa basi na hizi na nyingine nyingi msizozijuwa zitarudi:

Fatilia huu mjadala uone jitihada za Kikwete kwenye hili:
zomba Re: Secrets of Swiss Banking - Kitabu
Nyuzi kama hii ndipo nnapopata fursa ya kumsifu Kikwete, kabla Invisible hajatuwekea humu hiki kitabu, Kikwete kaanza kulifanyia kazi zamani sana na nivyema mpaka leo (2008) elimu imewafikia kina Invisible na wanaanza kuwatanabahisha na wengine, ingawa Invisible yupo miaka miwili nuyma lakini hii ni kazi ya kuendelea na nampongeza kwa kuiunga mkono kwa kutowa elimu kama hii aliyotuwekea.

Kikwete hii kazi aliianza na kuifanya kwa kubadilisha sheria humu ndani ya nchi zinazohusiana na utoroshaji wa fedha na rushwa, hakuishia hapo akakazania sana kuhusu sheria ya Umoja wa Mataifa itakaruhusu fedha zilizopo nje ya Afrika za Waafrika ziwekwe wazi na kurudishwa ikigundulika hazijapatikana kihalali, hata juzi juzi alilisemea sana alipokuwa Arusha kwenye mkutano wa majaji wa jumuiya madola.

Alilitilia mkazo pia walipokutana na wakuu wa kuzuia rushwa afrika mashariki.

Sasa japo tunaona manufaa ya kazi yake, angalau tunajuwa ziko ngapi hapo Uswisi tu na bado zipo nje kwingine kwingi na nyingi tu nna uhakika Kikwete haziachi hizo, kama alivyorudisha fedha za rada na hizi zitarudi tu.

Hapo ndipo nnapompendea Kikwete, nyie semeni yeye anafanya.

Kuwakumbusha tu kuwa kazi hii kaianza zamani na leo mna matunda yake nimewawekea links tofauti hapa chini mjikumbushe:

http://www.google.com/url?sa=t&rct=j...vFP36w&cad=rj a

Kenya: Kikwete calls for uniform tax system in East Africa

Zimefichuka » Blog Archive » KIKWETE'S CAMPAIGN AGAINST CORRUPTION PROMISING

Kikwete on money laundering and corruption - Google Search[+Arusha

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/13023-secrets-of-swiss-banking-kitabu-print.html
 
Imeanzisha hicho kitengo na kimesaidia kugundulika hilo je hatua gani zimechukuliwa? Hapa tunachohitaji ni hatua.

Soma post #26 ufate na links utajuwa Kikwete kafanya nini, si leo, si jana. Nakutakia usomaji mwema, hii issue haijaanza leo isipokuwa wachache wenu mmeanza kuijuwa leo, labda wakati huo mlikuwa bado mpo busy masomoni au mlikuwa hamjui mitandao ya kijamii.
 
Rais wetu ni msikivu sana vuteni subira mazuri mengi yanakuja kwa muda wa miaka mitatu iliyobakia ataacha historia ambayo kamwe watz hamtakuja kuisahau
Mijitu mingine bwana inaongea kama imepakatiliwa miaka yote hatujaona ndo itakuwa hiyo mitatu au atakuwa anaandaa mshiko wa kustaafia Uswisi
 
Baada ya kutafakari kwa muda mrefu ile hotuba ya JK aliyosema kuwa madai ya madakitari na walimu hayatekelezeki kwa sababu serikali haina uwezo imenilazimu leo niulize:
Je, huu ni uungwana kwa mheshimiwa kukaa kimya baada ya kujulikana kuwa kuna bilioni 300 za mafisadi kule Uswisi?
Je, mheshimiwa haoni kuwa kukaa kimya kunadhihirisha kuwa yeye ni mmojawapo wa wamiliki wa hizo pesa?

Naomba tujadili kama ungekuwa wewe ndie rais ungechukua hatua gani?

Mkweree will not commit suicide!! Kama kawaida yake anaamini huo ni upepo wa kupita tu!!!
 
Tungepata raisi ambaye anaweza akatunyongea angala mafisadi 10 nchi hii angalau tungepata nafuu.Tuwe kama china tu.
Ukishahisiwa umeiba fedha za watanzania,ni kunyongwa.mbona nchi hii tungekuwa mbali.
 
Baada ya kutafakari kwa muda mrefu ile hotuba ya JK aliyosema kuwa madai ya madakitari na walimu hayatekelezeki kwa sababu serikali haina uwezo imenilazimu leo niulize:
Je, huu ni uungwana kwa mheshimiwa kukaa kimya baada ya kujulikana kuwa kuna bilioni 300 za mafisadi kule Uswisi?
Je, mheshimiwa haoni kuwa kukaa kimya kunadhihirisha kuwa yeye ni mmojawapo wa wamiliki wa hizo pesa?

Naomba tujadili kama ungekuwa wewe ndie rais ungechukua hatua gani?

My take: pattern ya majibu na maelezo yake siku hizi ni rahisi kubashiri atasema nini! majibu yake always ni yale simplistic; majibu rahisi kwa maswala magumu! kwa mfano:-

1. Richmond/Dowans Jibu lake: wenyewe siwajui!!!
2. Epa: wakirudisha pesa tunawasamehe.
3. Rada: Hakuna rushwa!!
4. Wafanya kazi TUCTA: Kura zenu sizihitaji, mkigoma nitwapiga manundu!!!
5. Walimu/Madaktari: Mishahara hiyo hailipiki, tukiwalipa serikali haitafanya kazi nyingine!!
6. Dr. Ullimboka: serikali haihusiki hata kabla ya tume iliyoundwa kuchunguza unyama huo haijaanza kazi yake!!!

Hili la billioni 300 mimi sio Sheikh yahya lakini sitashangaa akisema wamiliki sio Watanzania!! teh teh teh!!

Kwa hiyo haina tija bora ajinyamazie kimya kuliko kutoa maelezo yanayozua maswali zaidi kuliko majibu!
 
SISIEMU ni chama hatari sana sana kinapandikiza udini,ukabila na mauaji Tanzania,Chama hiki 2010 kilikataliwa sana mijini,lakini kwa sasa mpaka vijijini ndani ndani huko Maswa,Meatu,Bukombe,Ukerewe n.k.,wote wazee kwa vijana wamekikataa hawakitaki tena,hawataki hata kukisikia wanasema 2015 lazima wakichinjie baharini.
 
Back
Top Bottom