Je, huu ni ulaghai wa CCM kuhusu hospitali ya rufaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, huu ni ulaghai wa CCM kuhusu hospitali ya rufaa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by babu M, Sep 21, 2010.

 1. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Jakaya Kikwete wakati akifanya kampeni mkoa wa Kilimanjaro aliahidi kuboresha hospitali ya Mawenzi kama inavyoelezea kwenye nyekundu hapo chini
  Siku mbili baadae akiwa anafanya kampeni mkoani Manyara alitoa ahadi ya kuzipandisha hospitali saba kuwa za rufaa lakini hospitali ya Mawenzi haikuwa kwenye list kama alivyoahidi mkoani Kilimanjaro.
  Mwezi uliopita nilisoma ufafanuzi wa kamanda wa vijana wa UVCCM Moshi Mjini Aggrey Marealle kuhusu maneno aliyoyasema wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM mkoani Kilimanjaro. Katika utetezi wake niliguswa na sehemu moja, nina mnukuu “Nawahisi wasifanye hivyo na badala yake wamchague Bw Justin Salakana kwa kumpa kura ili aweze kufanya kazi na serikali ya Chama tawala kinachoongozwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
  Niliwasihi wananchi wa Moshi kuwa wasipofanya hivyo, BASI LA MAENDELEO HALITASIMAMA MOSHI NA BADALA YAKE LITAENDA KATIKA MIKOA JIRANI KAMA VILE ARUSHA,TANGA, MANYARA NA MIKOA MINGINE JIRANI”.

  Kauli hiyo ya kamanda wa vijana ilifanya niifananishe ccm sawa na baba ambaye ana mtoto wa kambo na watoto wengine wa kuwazaa, wote kwa pamoja wanalitumikia shamba la familia lakini mazao yanapovunwa baba anawagawia watoto wake wa kuwazaa na kunyima mtoto wa kambo.


  Asilimia kubwa ya pesa zinazotumika kuleta maendeleo zinatokana na kodi tunayotozwa sisi wananchi wakiwemo wana Chadema pia.Kutumia pesa za kodi hizo kuleta maendeleo kwenye majimbo ya ccm tu na kubagua ya upinzani ni UFISADI WA HALI YA JUU.


  Kutokana na hizo ahadi za Mwenyekiti wa CCM taifa na kamanda wa vijana UVCCM Moshi Mjini. Je, Kikwete baada ya kumaliza kampeni zake mkoani Kilimanjaro aligundua washabiki wa upinzania ni wengi na baadhi ya majimbo ya ccm yatachukuliwa na wapinzani akaamua BASI LA MAENDELEO LISISIMAME MKOANI KILIMANJARO?

  Au alidanganya kwa ajili ya kura huku akiwa hana mpango wowote wa kuipandisha hadhi?
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Usalama wa taifa ndio wanamwandalia taarifa aseme nini, afanye nini na kwa wakati gani, wamekuwa wakijishughulisha sana kumbomoa bwana mkubwa kwa taarifa za udanganyifu, kuanzia leo tutasikia makubwa tena mikoa ya kusini.

  Hospitali ya mawenzi inatakiwa kujengwa upya kabisa na shilingi 1.6 bilioni ni pesa za kutosha kujenga vyoo peke yake, kwa taratibu za serikali ya ccm.

   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Usanii!
   
 4. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa JK anafanya usanii tu, anaahidi tu ili mradi apate kura, ikumbukwe kwamba hiki ni kipindi chake cha mwisho hivyo hatakuwa na wa kumuuliza. Akiwa mkoani Mbeya aliwaahidi wakulima serikali kupitia wakala wa ununuzi wa mazao ya chakula itanunua mazao ya wakulima, wakulima wakapeleka mazao yao kwenye maghala ya serikali, sasa mwezi umeisha bado zzziiiiiiiii! ni usanii tu wa JK na genge lake la wahalifu
   
 5. m

  mkenda1000 Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 6. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Kama alidanganya,Lazima kuna mtu atakuwa na audio, kwa nini vyama vya upinzani wasitumie kama mtaji wao wa kiasisa kuonyesha jamaa ni msanii?
   
 7. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Hospitali ya Mawenzi inaitaji ukarabati mkubwa kama sio kuanza from scratch.Juzi nimeingia baadhi ya wards zimechakaa kupita kiasi ni risk sana kufanyiwa upasuwaji kwenye hospitali iliyoko kwenye mazingira kama yale,unaweza kwenda kutafuta matibabu ukaondoka na magonjwa mengine.

  Niliposoma ahadi ya Kikwete kuipandisha hadhi, ilinipa moyo kiasi fulani na serikali kwa sababu nilijua wataifanyia ukarabati wa hali ya juu, vile vile niliamini CCM imeamuwa kuondokana na ile dhana "ukitaka mambo yako ya kunyooke jiunge na sisi" baada ya siku mbili unapojua ilikuwa ni ulaghai inatia kichefu chefu kweli.
   
 8. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Safi sana! Wana Kilimanjaro ni sawa na "maskini jeuri".Bado wapo baada ya kuambiwa wakiendelea kushabikia upinzani BASI LA MAENDELEO HALITASIMAMA MOSHI.Ni vizuri kuona baadhi ya wapiga kura wanasimamia Principles.
   
Loading...