Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

mkuu " zitto asante kwa hii ithibati" Mimi mwenzenu " nilishajitoaga kabisaaa kwenye imani ya hizo ngano za wazungu na waarabu" naishi kivyangu vyangu"kabisaaa.. sidhani kama kuna ambacho nitakuwa ninakipoteza
Hongera sana , nami nipo mbioni
 
Nashukuru kwa majibu mazuri mkuu, ila naomba kufahamu juu ya aina ya watu alikutana nao CAIN baada ya kuwekewa alama na kuondoka EDEN kwa kuwa biblia ya hivi sasa haikuwafafanua watu hao.
Mkuu tufahamu kwamba Adam hakumzaa tu Cain na Abel bali alizaa watoto wengine zaidi ya 50!!! hivyo Cain alipohama alipoishi kuna uwezekano alikutana na vizazi vya watoto wengine wa Adam ambao waliishi maeneo tofauti na yeye hivyo watu wa NOD (ingawa inamaanisha kuzurura tu) ni WATOTO wengine wa Adam

SOURCE
1st book of Adam and eve
Life of Adam and Eve
Book of jasher
Biblia (Mwanzo 5)
 
Asante sana kwa majibu yako mkuu. Naomba uwe unani_tag ili nisipitwe na elimu hii uiletayo kwa wana jamii forum
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita
View attachment 828516
Mada ya leo ni kuhusu ukweli wa mzazi halisi wa Cain ama tuseme kizazi cha nyoka na kizazi cha Adam. Ikumbukwe nyoka anyeongelewa hapa sio nyoka huyu wa sasa anayetambaa naongelea yule wa kabla ya tunda kuliwa.

Reference yangu itakuwa vitabu vya dini kadhaa kuanzia uyahudini,biblia,apocrypha,pseudipigraphi, maandishi ya wanatheolojia na vitabu vya kihistoria.

UTANGULIZI
Kupitia nadharia hii, yote yanaanzia kwenye bustani ya Eden ambapo tunaona shetani kupitia nyoka akimshawishi Hawa "kula tunda" na katika tunda hilo inaaminika linahusianisha ngono ambapo nyoka alimlala Hawa na kumpachika mimba ambayo baadae alikuja kuzaliwa Mtoto wa uzao huo yaani kizazi cha nyoka yaani Cain ili shetani aweze kuharibu uumbaji wa Mungu.

KWANINI NADHARIA HII?
Ili tuamini Nyoka alilala na mwanamke tunaweza tumia vigezo vifuatavyo

1. Adhabu kubwa ya Mungu kwa mwanamke ilikuwa ni kwenye sekta ya ngono sababu ndipo alipoanguka ndio maana Mungu akamhukumu sababu ya tendo la ndoa na mimba aliyobeba pia.

Mwanzo 3:
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala

Pia shetani tukisoma kwenye kitabu cha biblia (madhehebu kadhaa hukitumia) cha Apocalypse of moses 26:1-4 tunaona hukumu ya Mungu kwa shetani kuwa atamtoa masikio,mabawa na UUME!!!!

Hivyo nadharia hii kuwa ngono ilihusika inapatiwa nguvu kupitia mistari hii

NANI BABA WA CAIN?
Biblia ya kiswahili inasema

Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA

Lakini tafsiri iliyofanyiwa uhakiki kupitia New jerusalem Translation inasema hivi kwa kiswahili

...... Nimepata mtoto kutoka kwa malaika wa Bwana

Hivyo kama tafsiri hii ya NJT ina maanisha Adam alikiri kuwa mtoto sio wake ila wa MALAIKA ambaye kwa muktadha huu ni lucifer.

Kwenye biblia ya kiebrania neno lililotumika kwa KUMJUA ni Yada na Eth ambapo Yada baada ya kufanyiwa utafiti mpya limeonekana haimaanishi tu ni kumlala mwanamke bali inamaanisha KUTAMBUA KITU na Eth ina maanisha ALAMA FULANI(mabadiliko) hivyo tukiuandika mstari huu upya kutumia tafsiri ya maneno haya itakuwa hivi;

Adamu akatambua alama/ishara ya mabadiliko juu ya Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa malaika wa BWANA

Kwahiyo mpaka hapa tumeshapata maana tofauti kabisa ya mstari huu si ndio wakuu??

JE KWANINI NASEMA CAIN SIO MWANA WA ADAM
1. Biblia huko mbele inamtaja Cain kama alitokana na ''yule mwovu'' yaani shetani

1 Yohana 3:12
12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
View attachment 828519

2. Biblia inamtambua seth kama mtoto pekee wa Adam maana inadai Henoko alikuwa mtu wa 7 baada ya Adam na ukihesabu utagundua imetaja uzao wa seth peke yake na imemuacha Cain peke yake hivyo ikimaanisha Cain hakutambuliwa kma mwana wa Adam

Yuda 1:14
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao
View attachment 828520

3. Tunaona hata seth ndio biblia inaonyesha alizaliwa kwa mfano wa sura na mfano wa adam

Mwanzo 5
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi

Hii yote ikimaanisha Cain hakuwa uzao wa Adam ndio maana hakufanana naye Adam kwa lolote hivyo muandishi hakuona sababu ya kujumuisha jambo hilo alipozaliwa cain.

4. vitabu vinavyotambuliwa na dini ya kiyahudi kama Zohar Pekudei 21:5 kinakubali hoja hii.

Baada ya adam na mke wake kufanya dhambi, na shetani kumjua Hawa na kumnajisi, Hawa alimzaa Cain. Alikuwa na umbo la duniani na kuzimu. Hivyo,alikuwa wa kwanza kuleta kifo duniani,iliyosababishwa na upande wake wa kuzimu,sababu alitokana na uchafu wa najisi ya nyoka (kwa hawa). Asili ya nyoka(shetani) ni udanganyifu,mauaji,na Cain,alijifunza nyendo zake. (Utafsiri binafsi)

HITIMISHO
Kupitia hayo maandiko machache nlioweza kupata ninaweza kufikia hitimisho kuwa kuna uwezekano tumefichwa kwa muda mrefu kuhusu uhalisia wa kilichotokea Eden nikaona nilete nadharia hii JF ili tuweze kufikiri pamoja na kupata ukweli wa jambo hili.

NB: Naomba Moderator msiunganishe nyuzi hii na zingine juu ya bustani ya edeni maana hii imejikita zaidi kwa Cain na sio maisha ya bustanini

Naomba kuwasilisha
Mada ni fikirishi na ina kila namna ya ukweli.
Huu ukweli wa mzazi halisi wa Kaini na kweli nyingine nyingi zilizofichika katikati ya mistari ya maandiko matakatifu ziko wazi kwa wana halisi wa Mungu katika zama zote. Kile tunachoona ni mkang'anyiko ni kwa walio nje na bado wataendelea kujichanganya na kweli za maandiko hadi mwisho wa wakati. Ni kwa nini imekuwa hivyo? Sababu ni kutoka katika msingi wa Imani na kujikita katika hoja. Kweli ya Mungu hapatikana kwa kuamini tu na sii vinginevyo. Adamu alimwamini Mungu , Eva aliweka mjadala wa kihoja na nyoka na ndio sababu pekee yule nyoka aliyetajwa kuwa mwerevu kuliko hayawani wote Mungu alioumba akapata pa kupitia kuvuruga kanuni za uumbaji.
Jambo moja na la msingi ambalo ninaliona la kuwa mzazi wa Kaini ni nyoka na kwamba kilichofanyika pale katika bustani ya Eden ni ngono ni yale maneno ya Mungu kwa nyoka baada ya lile tendo.
Mwanzo 3
15nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, [na kati ya uzao wako na uzao wake]; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
.
Hapa inathibitisha bila shaka kwamba baada ya lile tendo imesababisha zao mbili tofauti duniani. Yaani uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke. Uzao wa mwanamke ndio huo unatajwa katika biblia yaani mfuatano wa vizazi kutoka Adamu hadi kwa Bwana Yesu.
Huumwingine wa Kaini ndio huo pia uliokuja kusababisha gharika ya Nuhu kwani hasira ya Mungu iliwaka juu ya watoto wake(wana wa Mungu) kujichanganya kwa kuoana na ukoo wa kaini(binti za wanadamu#manafeli?#) na kusababisha chotara lililojulikana kama majitu- giants.
Watu wanaweza kusema uzao wa nyoka ni suala la kiroho tu kwamba hakukua na uzao halisi kibaologia wa nyoka.
Ukiingia katika kukubaliana na hii nadharia ni lazima basi ukubali kuwa Yesu nae anaetoka katika huu uzao wa mwanamke hakuwa ni wa mwili wa nyama na damu kitu ambacho sii kweli.
Kuna mengi sana ya kuthibitisha ila kwa leo niishie hapa kwanza.
 
Asee mkuu una reasoning kubwa sana kiufupi umemaliza kila kitu maana umerelate scenario nzima nayoiongelea na ukaoanisha na matukio ya baada ya Eden yanayoweza support nadharia hii.

Respect kwako mkuu this is what we call a GREAT THINKER
 
Barikiwa mkuu!
 
Mkuu hii mada ngumu...najaribu kuchunguza biblia yangu kitabu cha mwanzo napata mkanganyiko.... Kwa nn hv Mwanzo 4:1 Adam akamjua Hawa mkewe naye akapata mimba akamzaa Kaini......Akaongeza akamzaa ndugu yake Habili alikuwa ......Mwanzo 5:1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adam..... 3 Adam akaishi miaka 130 akamzaa mwana kwa sura yake ,kwa mfano wake akamwita jina lake Seth... Apa biblia haikuwataja Kaini wala Habili why??! Tena wasiwasi wangu hata Habili sio mwana wa Adam..!! Kuna namna biblia inaacha maswali yenye shaka kuu kwa wasomaji wake.
Mkuu Habili ni mwana wa Adamu ila katika genealogy ya uzaowa kutoka Adamu hatajwi kwa sababu yule mwana wa nyoka yaani kaini alikatiza uhai wake kabla ya kuwa na uzao. Ndio maana maandiko kwa Habili yanasema "Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili"
.
Mwanzo 4
25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.'
Kulingana na haki ya uzaliwa wa kwanza kama Kaini angelikuwa ni wa Adamu basi kauli isingelikuwa kuwekewa uzao badala ya Habili bali kuongezwa maana tayari Kaini mzaliwa wa kwanza yupo.
Yaani hapo ni ushahidi mwingine wa Kaini kutupwa nje na mzao wa Adamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom