Je huu ni ubaguzi au ubinafsi?

BroJay4

JF-Expert Member
Aug 27, 2007
236
16
Safari ya Kapuya India yazua jambo

na Mwandishi Wetu


UAMUZI wa kumpeleka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, nchini India kwa ajili ya matibabu kufuatia ajali aliyoipata jimboni kwake hivi karibuni, umelalamikiwa na baadhi ya watu.

Watu kadhaa waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa uamuzi huo unaonyesha sura ya ubaguzi, wakihoji kwa nini Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Urambo, Twaha Ngoso, ambaye alipata majeraha makubwa kuliko Kapuya, asifikiriwe naye kupelekwa nje ya nchi?

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), walisema uamuzi wa kumpeleka India Profesa Kapuya, na kumwacha Ngoso, inadhihirisha jinsi ambavyo serikali isivyowathamini baadhi ya watu.

Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo ambao waliomba majina yao yasiandikwe gazetini, walisema wameshangazwa na hatua hiyo ya kumpeleka kiongozi huyo wakati hali yake ilikuwa inaendelea vizuri ukilinganisha na mwenyekiti huyo ambaye alifikishiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi akiwa hajitambui.

“Kama tungefuata usawa na utaalamu, aliyestahili kupelekwa nje ya nchi kwanza ni huyu mwenyekiti wa CCM… huyu ndiye aliyejeruhiwa sana ukilinganisha na Kapuya, alikuwa amepoteza fahamu kwa siku kadhaa… hali hii inaonyesha mgawanyiko kati ya viongozi na wananchi wa kawaida,” alisema mmoja wa wauguzi kwenye taasisi hiyo.

Habari nyingine zinaeleza kuwa hata uamuzi wa kumpeleka nje Profesa Kapuya ulitokana na shinikizo la watu wengine ambao si wataalamu wa afya waliokuwa wanamtibu.

“Kulikuwa na kazi kubwa ya kukubaliana kwani hata mmoja wa madaktari aliyekuwa karibu na Waziri Kapuya alitoa ushauri wa kuendelea kutibiwa hapa hapa,” kilisema chanzo chetu.

Baadhi ya wanachama wa CCM kutoka mkoani Tabora wakizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, walisema wamesikitishwa na uamuzi huo kwani Ngoso ni mmoja wa waliompigia kampeni Kapuya katika uchaguzi mkuu uliopita na kufanikisha kupata ubunge.

Walisema hawapingani na uamuzi wa kumpeleka Profesa Kapuya kwa ajili ya matibabu nje ya nchi lakini tatizo lao ni kwa nini mtu aliyeonekana kuwa ameumia sana anaachwa bila matibabu kama hayo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Brigedia Jenerali Alfred Mbowe, ilithibitisha kuwa Waziri Kapuya amepelekwa India kwa ajili ya matuibabu.

Hata hivyo, Brigedia Jenerali Mbowe hakuweza kueleza hospitali ambako Profesa Kapuya anatibiwa au msafara wake ulikuwa na watu wangapi.

Waziri Kapuya alipata ajili ya gari Septemba 24 akiwa kwenye ziara ya kikazi katika Jimbo la Urambo Magharibi, mkoani Tabora, baada ya gari lake kupasuka gurudumu na kupinduka.

Watu watatu walifariki dunia katika ajali hiyo na Waziri Kapuya pamoja na majeruhi wengine wawili walisafirishwa hadi Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.


Source:Tanzania Daima.


Ni lini hawa viongozi wetu wataacha huu mchezo mchafu wa kutibiwa nje?Akili ni nywele kila mtu ana zake,waafrika tumezidi ujinga.
 
mbona madaktari walisema hatapelekwa kutibiwa nje pindi tu alipofikishwa hospitali? au ndiyo fasheni ya kila kiongozi kwenda nje pindi anapo umwa? Naje hizo fedha zinatoka kwenye mgodi wake au kwenye fedha zetu sisi walipa kodi? mbona serikali haichangii wagonjwa wa moyo wanaopelekwa India kwa matibabu na Lions club akishiriana na bwana Mengi? kweli nakumbuka ule msemo kwenye kitabu cha Animal Farm uliosemwa na sijui Napoleon au Snoble kama sijasahau kuwa, "All animals are equal but some are more equal than others"
 
Back
Top Bottom