Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Kwanza nikurekebishe kidogo wewe mwandishi binafsi unaonekana sio Mwalimu..kwasababu Kwa elimu ya msingi kipindi hiki cha mitihani wapo likizo, na jambo lingine wanafunzi wengine wasio wa darasa la mitihani hawaruhusiwi kufika shule..sasa Mwalimu umepataje fursa ya kutoa zoezi kipindi cha mitihani
Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
 
Kwanza nikurekebishe kidogo wewe mwandishi binafsi unaonekana sio Mwalimu..kwasababu Kwa elimu ya msingi kipindi hiki cha mitihani wapo likizo, na jambo lingine wanafunzi wengine wasio wa darasa la mitihani hawaruhusiwi kufika shule..sasa Mwalimu umepataje fursa ya kutoa zoezi kipindi cha mitihani
Kisingizio chake darasa la 4 hawajafunga
Kiukweli Huyo mleta mada sio mwalimu,na Kama Ni Mwalimu Basi anachofanya shuleni NI KUDUMAZA UPEO WA WANAFUNZI ANAO WAFUNDISHA!!!!
 
Back
Top Bottom