Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,672
Mambo yanaanza kujifunua taratibu kwamba kuna kaliba zimejazwa na uoga na kutojiamini, kukataa kukosolewa na kutaka kujifanyia na kufanya kila kitu mwenyewe bila tafakuri ya kina wala athari za mbeleni.
Mkakati unajaribu kupangwa kiufundi sana lakini kukiwa na makosa na mapungufu mengi
1. Kujaza vijana wengi kwenye maeneo muhimu huku wazee wakitupwa nje au pembeni kwa kisingizio cha kwamba vijana hawapendi rushwa
Vijana hawa ni wale wa kuitikia ndio mzee wapenda sifa na wasio na tafakuri ya kina
2.Kuviinua vyama dhaifu vya upinzani ambavyo vitapiga kelele za kawaida zisizo na madhara I mean vyama joka la kibisa, hivi ni vyama visivyojua uchaguzi ndani yake ni kitu gani...ni vyama vinavyoendeshwa kama NGO binafsi huku vikiibuka wakati wa chaguzi za nchi vyama vya msimu
3. Kudhoofisha na kuubana upinzani wa kweli kupitia vyama vyenye nguvu vinavyounda umoja wa UKAWA, kwa mbinu mbalimbali nyingi Zikiwa chafu na zisizosadifu demokrasia
4. Kununua watu muhimu kutoka vyama vyenye nguvu na kwenda kuwapandikiza kwenye vyama dhaifu kwa matumizi ya baadae
Mikakati ipo mingi lakini kwasasa inayoonekana wazi ni hii michache.
Swali la kuogofya sana. Je, huu ni mwanzo wa maandalizi ya utawala wa kidikteta?
Time will tell