Je huu ndio ukweli kuhusu BOT?

BroJay4

JF-Expert Member
Aug 27, 2007
236
17
Nimepata mail iliyo na tuhuma kuhusiana na BOT.Je kuna ukweli wowote kwenye mail hii|?

Hii ni habari halisi na ya uhakika kutoka ndani ya BOT. Je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa.

Nakutajia kwanza wachache ili wewe na watanzania wenzetu watafakari kama kweli ndege yetu itaweza kupaa kama bwana Lowasa alivyosema, au tutabaki ombaomba kama Balali anavyodai!!!. Ama tunageuzwa kuwa wadanganyika!!!

Ndani ya Mtungi wa BOT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BOT ni pamoja na hawa wafuatao:-


Pamella Lowassa, Filbert Frederick Sumaye, Zalia Kawawa, Harieth Lumbanga,Salama Ally Mwinyi, Rachael Muganda, Sylvia Omari Mahita, Justina James Mungai, Kenneth John Nchimbi, Blassia Blassius William Mkapa, Violeth Phillemon Luhanjo,Liku Irene Katte Kamba, Thomas Mongella,Jabir Abdallah Kigoda etc. Hii ndio success team, hapa nani atamuwajibisha Dalali alas Balali?

Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO?

Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na serikali ya Tanzania (kumbuka hapo juu nimesema serikali maana yake ni...?) , wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya(mere coincidence).

Bwana Mpayukaji, ni shauri la watanzania kuamua kuendelea na viongozi wabovu na wenye ubinafsi au kuwaambia ukweli hata kama utawauma na kwa vile wao ndio miungu basi watatoa adhabu za kukufukuza katika bustani ya Eden.

Rhuksa kupayuka utakavyoona inafaa, na kama kuna cha kuongeza na kiko ndani ya uwezo wangu, nitakuongezea.


Onyo.

Mpayukaji alizaliwa akiwa mbwi.
Kama akikupayukia ukajisikia kumshitaki
jua unapoteza muda wako wa thamani.
Maana mtu mwenyewe ukimuona
hata waokota makopo wana nafuu.
Ila anayopayuka yana ukweli.
Muhimu siyo kuchukia mipayuko yake.
Bali wale wanaosababisha apayuke.
Usipoiba polisi utamuona wapi?
 
Kwa kweli hapa watoto wa wakulima kazi ipo, sasa hata mkisema mshindanishe vyeti yeye tena anavyo vya Uingereza na America (ingawa wengi ni community college hizo hizo, though wakija wanatudanganya akina sisi Masanja!)! sasa jamani twende wapi? Hii list naikubali maana kuna watu kama watatu nawafahamu hapo walikuwa wanahangaika mjini na sisi ila wameshalamba kazi BOT! hapa swala siyo competence, swala ni fair distribution, unajua nafasi kwenye sehemu sensitive kama hizi ingebidi jamaa wafikirie mara mbili mbili maana inaleta manung`uniko yasiyo ya lazima.

Ila ukweli BOT imekuwa Usalama wataifa, kama hujui mtu wa juu basi wewe ukipata humo you are more than lucky!
 
Obviously they're the most qualified candidates going by the responses ellicited from JF.
 
Nyerere tu ndo hakujua namna ya kuitafuna nchi hii,watu wanatafuna mpaka makombo wanapatia hata mbwa wa jirani zao...sie ambao baba zetu wanamwaga jasho lao na kuvunja migogngo yao kuzalisha mali inayoliwa na wakubwa hawa tulie tu...ila saa ile inawadia,hatutawaachia hata hawa waendelee kuifilisi nchi yetu...hasira ya umma itakapoanza kumwagika (kwa sasa boiling point iko 60C) we'll leave no stone unturned...
 
Wewe Ibambasi,

Mkapa akikusikia atasema una uvivu wa kufikiri na pia kuwa wewe kama watanzania wengine mmejaa wivu dhidi ya viongozi wenu!
 
Wabongo bwana! Kwahiyo wasipewe kazi simply kwasababu baba yake ni waziri au mtu popular?!?

Amkeni, angalieni kama ana qualification ya hiyo kazi, na anaiweza?, hivyo ndivyo vitu muhimu!

Acheni wivu
 
Wabongo bwana! Kwahiyo wasipewe kazi simply kwasababu baba yake ni waziri au mtu popular?!?

Amkeni, angalieni kama ana qualification ya hiyo kazi, na anaiweza?, hivyo ndivyo vitu muhimu!

Acheni wivu

Watu wanaanza kuogopa hata unyasi baada ya kuumwa na nyoka.

Tatizo liko kwenye kuanguka kwa elimu Tanzania. Hao mawaziri na wenye pesa wanasomesha watoto zao shule za maana, matokeo yake hata kazi za maana zote watachukua wao. Ni makosa kuwalaumu watoto maana huenda wamepata hizo kihalali kwa kufuata ujuzi wao.

Tunachotakiwa kufanya ni kuwalaumu wanasiasa, kuwanyima kura wanasiasa wanaoua shule zetu, hospitali zetu nk. Lakini Watanzania tulivyo tukihongwa beer basi tayari tunawachagua viongozi wabovu.

Ukisoma hizo shule za Lowassa kweli utaweza kupambana na hao wanaosoma shule za maana?
 
Wabongo bwana! Kwahiyo wasipewe kazi simply kwasababu baba yake ni waziri au mtu popular?!?

Amkeni, angalieni kama ana qualification ya hiyo kazi, na anaiweza?, hivyo ndivyo vitu muhimu!

Acheni wivu

Hta mimi nilijua yatakuwa haya
 
Wabongo bwana! Kwahiyo wasipewe kazi simply kwasababu baba yake ni waziri au mtu popular?!?

Amkeni, angalieni kama ana qualification ya hiyo kazi, na anaiweza?, hivyo ndivyo vitu muhimu!

Acheni wivu

Hata mimi nilijua yatakuwa haya
 
Watu wanaanza kuogopa hata unyasi baada ya kuumwa na nyoka.

Tatizo liko kwenye kuanguka kwa elimu Tanzania. Hao mawaziri na wenye pesa wanasomesha watoto zao shule za maana, matokeo yake hata kazi za maana zote watachukua wao. Ni makosa kuwalaumu watoto maana huenda wamepata hizo kihalali kwa kufuata ujuzi wao.

Tunachotakiwa kufanya ni kuwalaumu wanasiasa, kuwanyima kura wanasiasa wanaoua shule zetu, hospitali zetu nk. Lakini Watanzania tulivyo tukihongwa beer basi tayari tunawachagua viongozi wabovu.

Ukisoma hizo shule za Lowassa kweli utaweza kupambana na hao wanaosoma shule za maana?

Mtanzania,

Good points. Nilikuambia kuwa tunakubaliana zaidi ya tunavyotofauitiana. Hapa umesema ukweli kabisaaaa. Kama vigogo wanasomesha watoto wao na kuwapatia elimu yakutosha. Ni vigumu sana kushindanisha watoto wa vigogo na walalahoi.

Asante kwa hili.
 
Kuwa na uwezo peke yake haitoshi kumfanya mtu apate kazi mahali fulani. Jinsi gani mtu amepata kazi hiyo ndiyo swali la msingi. Kama kwa namna yoyote ile kuna njia za mkato zimetumiwa ni halali watu kuhoji. Binafsi kuona majina ya kina Sumaye, Mkapa n.k hilo halinisumbui mbona tulikuwa na kina Mwamunyange tangu Uhuru na watoto wao nao wanapanda vyeo jeshini?

Hapa US miaka michache iliyopita wakati Collin Powell yuko State Department mtoto wake alikuwa ni mwenyekiti wa FCC.. so tusiangalie majina tu, tuangalie ni jinsi gani watu wamepata nafasi hizo.

Hata hivyo, inajulikana kwa baadhi ya watu jinsi gani watoto wa wakubwa wanapata habari ya nafasi za kazi na ni jinsi gani maombi yao ya kazi yanapatiwa "kipaumbele".

"Mzee A, mwanao K anaendeleaje bwana" anauliza Kibosile M ambaye alikuwa ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

"Ah, anaendelea vizuri ndio amerudi toka masomoni". anajibu Mheshimiwa Mbunge Utata wa jimbo la Ukata. Mkononi ameshikilia ufunguo wa gari lake la Kibunge, Toyota Prado.

"Hivi alienda kusomea nini" Anauliza tena Waziri wetu huku akiweka gilasi yake ya kinywaji baridi cha Serengeti Lager. Anamuangalia Mbunge akijikalisha vizuri kwenye kiti kile kirefu cha pale Kaunta ya Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi Oysterbay. Kwa mbali mawimbi yalikuwa yakisikika yakigonga ukingo wa bwalo hilo maarufu, huku upepo wenye harufu ya chumvi ukipulika kama kwa zamu.

Upande wa pili, kulikuwa na kikundi cha watu kama watatu hivi ambao na wenyewe walikuwa wanapata "mbili tatu". Tetesi zilisema hao walikuwa ni makomandoo wapya wa Tanzania waliorejea hivi karibuni toka Fort Bragg huko Marekani.

Kibosile anakohoa kidogo kusafisha koo, baada ya kupiga fundo moja la kinywaji baridi, "alienda kusomea mambo ya biashara, sasa hivi ana Masters bwana". Anajibu kwa fahari.

"Safi kabisa, sasa ameshaanza kutafuta kibarua bwana?" Anauliza tena Waziri mpendwa.

"hamna lolote yupo yupo tu, ila mheshimiwa kama unaweza kunisaidia nitashukuru, maana hawa vijana kukaa nyumbani tu kunawafanya wawe wavivu" Anajibu Kibosile M.

"Hamna neno, kuna kijana wa Waziri Malimau ya Konde, yuko kule Benki Kuu Human Resources ngoja nicheki halafu nitakupatia habari, nina uhakika wanaweza kupata nafasi ya mtu mmoja" Anasema kwa kujiamini.

"Nashukuru sana mheshimiwa, na wewe yule binti yako aliyekuwa Muhimbili Medicine yuko wapi sasa?" anauliza Kibosile M. Anauliza hivyo ili angalau kuonesha shukrani na uungwana.

"Nani Ndimu? au Bolibo?, maana wote wameenda Udaktari" anajibu kwa fahari.

"Yeah Ndimu" Anajibu Kibosile wetu kwani kwa sababu zake anazozijua hakutaka kulikisikia jina la "Bolibo".

"Ndimu, yeye amemaliza hapa Muhimbili, na sasa hivi ameenda mapumzikoni kwa kaka yake kule Detroit, kwenda kumsaidia wifi yake kidogo amejifungua. Atarudi kama baada ya mwezi hivi" Waziri anajibu huku akimalizia kinywaji chake kwa fundo moja. Wale jamaa watatu "makomandoo walikuwa wanaangalia TV ambapo kulikuwa na habari ya tetemeko la ardhi kule India.

"Vizuri sana Mheshimiwa, itakuwa vizuri tuwakutanishe hawa vijana wetu bwana maana wana urafiki wa zamani sana" Kibosile anasema huku ujumbe ukitumwa kwa Waziri. Waziri aliupata.

"Bila ya shaka, nina hakika watafurahi kupata muda kukumbushana vituko vyao pale Shaaban Roberts" anajibu, na wote wawili wanaangua kicheko.

Baada ya porojo za hapa na pale, wanaagana. Waziri anajiondokea taratibu hapo Bwaloni wakati Kibosile M, aliyekuwa amevaa bukta na tsheti nyeupe anachukua vifaa vyake na kwenda kwenye chumba cha kucheza squash. Moyoni amefurahi kwani kabla ya kuagana Waziri alimwambia ampatie kijana wake namba yake na kijana huyo ampigie simu kesho yake jioni.

* * *

Miezi michache baadaye, kijana wa Kibosile alikuwa ni Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Ukaguzi katika Idara moja nyeti serikalini. Alishangaa kujikuta anakutana na watoto wa "wakubwa" wengine kwenye ofisi hiyo. Hakuna anayemuuliza mwenzie "umefikaje hapa". Miezi sita baadaye Uchumba ulitangazwa kati ya Mtoto wa Kibosile M na binti ya Waziri Ukata.

Mahali iliyotolewa ni Shilingi milioni 20 na ng'ombe wawili, mashuka, mablanketi na mbuzi mmoja.

MWISHO
 
FD
At least inabidi kuwe na a sort of "affirmative action"; chukua sample ya wenye hizo qualifications walio nazo, Kama ukisema hivyo basi usawa kielimu au kuajiriwa; tungepangana wenyewe na nyie hamngegusa kitu!!! Ahaaaaaaaaaa!

Si unakumbuka wakoloni walipenda kuwasomesha watu gani, na nyerere akaja na "affirmative action" wote tusome? Wote tugawane hizo nafasi kisawa sawa? Kwa hiyo sample ya hapo juu, it is too much! What is at the BOT?
 
Mimi binafsi nimesoma na Thomas Mongela pale UDSM na kumaliza 1998 B.com in accounting. Thomas alikuwa mmoja wa wanafunzi wenye uwezo mkubwa kimasomo na alipata upper second with a GPA of 4.1. Juzi (3 monts ago)alipita hapa London akitokea Scotland alipokwenda for his graduation at University of Strathclyde MSc Finance. Pia Tom akeshafanya kazi Stanchart for more than 2-3 years kwa hiyo inaonesha kuwa anasifa za kufanya kazi hapo BOT.

Kwa hao wengine sijui sifa zao ila naona sio vizuri kuanza kuwasema watu kwa vile tu wazazi wao ni watu wenye madarka. Kama mtu ana ushahidi kuwa kuna mmoja wao hana sifa basi aziweke hapa
 
FD
At least inabidi kuwe na a sort of "affirmative action"; chukua sample ya wenye hizo qualifications walio nazo, Kama ukisema hivyo basi usawa kielimu au kuajiriwa; tungepangana wenyewe na nyie hamngegusa kitu!!! Ahaaaaaaaaaa!

Si unakumbuka wakoloni walipenda kuwasomesha watu gani, na nyerere akaja na "affirmative action" wote tusome? Wote tugawane hizo nafasi kisawa sawa? Kwa hiyo sample ya hapo juu, it is too much! What is at the BOT?

Kweli kabisa IO,

hiki ndicho amesema Mkjj hapo juu. Inawezekana kuwa watoto wa vigogo wanasomeshwa vizuri (ingawa baadhi yao wanapeta kwa kuiba mitihani na upendeleo). Lakini pia kuna watoto walalahoi kibao wamesoma vizuri tu na kufaulu vizuri tu kama hao wa wakubwa.

Tatizo inapokuja wakati wa kuajiriwa. Wadosi wanapeta na walahoi wanatoswa. Na baadae inakuwa vigumu kulalamika sababu hao wa wadosi nao unakuta vyeti vyao vinaonyesha mambo safi.

Nadhani inabidi pia kuwe kunafanyika uchunguzi wa namna watoto wa wadosi wanavyopata kazi kubwa serikalini. Nadhani walioko marekani watakumbuka Howard Stern alivyomshikia bango mtoto wa Collin Powel kuwa amepewa kazi kwa kupendelewa (ingwa mtoto yule shule imepanda) na uchunguzi ukaonyesha kweli the kid alikuwa amependelewa na ikabidi aresign kabla mambo hayajaharibika!

Kazi ipo bongo, siku mkiona watu wameandamana hadi ikulu na BOT on foot na wakakataa kutoka huko hadi kieleweke ndio itakuwa issue zaidi!
 
Nafikiri hapa tuwe wakweli. Haya mambo kwa TZ yapo kila sehemu, mfano mdogo nenda pale SUA utakuta vijana wengi wanaoajiliwa ni watoto wa ma-prof. either wako kazini au walishastaafu, tena sio kazi za kufundisha tu hata kazi za kugawa mishahara. Kama sio mtoto wa mkubwa ni based on kabila--angalia MSOLLA muda aliokaa SUA na watu wa IRINGA walivyoongezeka pale--kwanza unaambiwa kuwa uki-contest kazi na mtu wa IRINGA wakati wa MSOLLA elewa kuwa umeshashindwa. I think waswahili wanasema mkono unajikuna unapoweza--so kama SUMAYE alikuwa PM anaweza kujikuna BOT ni kama kushika tumbo. So mimi sioni kipya hapa otherwise kama hawa vijana hawajasoma lakini kwa ELIMU ya TZ hawa watakuwa wamesoma shule zilizo bora ambazo baba zao kwa kutumia pesa walizoziiba serikali waliweza ku-afford kulipa FEES.

Ieleweke kwanza siku serikali hata kama wakitangaza kazi, hakuna system ambayo ni transparent inayojali fair competition. Na bora hizo kazi wanafanya watz, je nafasi walizonazo wanyarwanda/warundi na wengine mbona hizo vipi.
 
Wabongo bwana! Kwahiyo wasipewe kazi simply kwasababu baba yake ni waziri au mtu popular?!?

Amkeni, angalieni kama ana qualification ya hiyo kazi, na anaiweza?, hivyo ndivyo vitu muhimu!

Acheni wivu


FD, Wasiwasi wetu ni hayo majina kuwa na uhuiano na vigogo. Hii haiingii akili kuwa ni coincidence hata kidogo (iwapo hayo majina ni kweli yapo BOT). Hatukatai kuwa watu hao wana vigezo vyote vya kuwa pale walipo, ila hatuna imani na namna walivyoingia pale.
Tunaomba ufafanuzi tafadhali.
 
Back
Top Bottom